Duniani kote, amani Huvurugwa Na Watawala na Sio vyama Mbadala au pinzani!

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
10,945
28,401
Siku zote,

Aliepo madarakani ndio huvuruga amani ya nchi au eneo husika. Mwananchi wa kawaida kwa nchi kama Tanzania ni ngumu kuanzisha uasi au kuingia porini aanzishe vita ili atimiziwe madai yake.

Serikali zote duniani ndio zilikua sababu ya machafuko kwenye nchi zao na machafuko hayo huzaa vita isiyokwisha na baadhi ya sababu ni kama ifuatavyo
1. Kunyanyasa na kuonea raia bila sababu ya msingi.

2. Kutotimiza wajibu wake kwa Raia, serikali inapaswa ikusanye mapato, isimamie upangaji wa matumizi sahihi ya mapato.

3. Ugandamizaji wa haki za msingi mfano kujieleza, kusafiri, kuabudu kwa mfano watu wanadai katiba mpya hawana hata silaha lakini wanaonekana wahalifu ukumbuke kuna siku watadai katiba mpya wakiwa na silaha inaweza isiwe leo, kesho au mwaka huu lakini wakichoka ni mbaya sana waruhusu wapige porojo wewe walinde mwisho watachoka tu.

4.Rushwa zilizokithiri yaani wananchi wanasikia tu kiasi fulani kimepotea halafu baada ya muda kiasi fulani kimepotea mwisho wanaona hawa viongozi ni wezi wa mali yetu ya umma hivo wanaamua kubadilika.

5.serikali kutofahamu ugawanaji wa rasilimali kwa usawa yaani inageuka watu fulani wanapelekewa kila kitu huku wengine wakisuasua kama sio walipakodi hii huwachosha wananchi na kuamua kugeuka rasmi.

Itarndelea na sababu hizi ni za kidunia hasa kuzingatia vurugu za maeneo mbalimbali duniani.
 
Naunga mkono hebu fikiria katiba ya Sasa inasema mtu akishatangazwa na tume ya uchaguzi kuwa ameshinda kiti Cha urais matokeo hayo hayatapingwa na mahakama yoyote lakini Cha kushangaza kura zinaibiwa Kama kawaida na wasimamizi wa uchaguzi wanalazimishwa kubadili matokeo kulinda ajira zao. Sasa swali kwani tusipinge mahakamani matokeo ya namna hii? Hapa watu wakitaka katiba mpya polisi wanawakamata je chanzo Cha vurugu ninani?
 
..Interahamwe wa Rwanda walikuwa vijana wa chama tawala.

..Manazi wa Ujerumani walikuwa vijana wa chama tawala.

Umeelezwa ni matokeo ya serikali zilizokua madarakani kama wangetenda haki unadhani vita au waasi wangejikusanya na kuleta vurugu, unapowafanyia watu mabaya kama mtawala ujue kuna siku watu haohao watatafuta njia sahihi ya kufikia muafaka na wewe
 

Kuna nchi watu wanakusanyika bila kiberiti, risasi, wala mapanga lakini wanakatazwa wanavunja amani huku wenzao wanaachwa wakusanyike kila muda wanaotaka unadhani watu hao wakichoka utawafanyaje?
 
Umeelezwa ni matokeo ya serikali zilizokua madarakani kama wangetenda haki unadhani vita au waasi wangejikusanya na kuleta vurugu, unapowafanyia watu mabaya kama mtawala ujue kuna siku watu haohao watatafuta njia sahihi ya kufikia muafaka na wewe
Hujamuelewa jokakuu amekusapoti hoja yako kwa mifano halisi
 
Back
Top Bottom