Duniani: Humu mitaani, Hatupo peke yetu. Hali inatisha sana

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,274
23,050
Jana Maulid alinambia mambo mazito ambayo sikuwahi yafikiria. Jamaa last week alitoka kwao maeneo ya Ilala akawa ameingia mtaani akielekea Magomeni. Jamaa anasema kabla ya kutoka alikuwa na mjadala mkubwa na Ami yake kuhusiana na mambo ya Kiimani.

Maulid amesoma pale DIT ana elimu yake nzuri tu. Alibishana sana na Ami yake ambaye alimwambia Duniani humu na mitaani tunapotembea tunapishana na viumbe vya ajabu na maviumbe makubwa makubwa.

Anasema walibishana sana mpaka Ami yake alipoamua kumsomea kitabu fulani na kumwambia anawe maji ambayo yalisomewa na kumwagiwa unga fulani ndani yake.

Maulid hakujali sana maana alijua Ami yake ambaye ni Sheikh atakuwa tu anamwonesha mbwembwe zake za kila siku.

Anasema alipotoka akapanda gari ndo akaanza kuona kama maruwe ruwe. Alimwona msichana mmoja mzuri akikatiza barabarani na wenzie wawili nao wazuri sana lakini alipowatizama vizuri aliona kama chini wana kwato.

Hakuamini.alitizama watu wengine akaona wao wanatembea wala hawashtushwi na jambo hilo.na wengine wakawa wanasema hao mbuzi hawaogopi kuvuka barabara yaani wengine wanaona ni mbuzi.

Maulid anasimulia kuwa kilichosababisha akapata ajali ni kuwa akiwa barabarani aliona jitu kubwa sana akalikwepa ndo kwenda gonga nguzo na kuingia mtaroni.

Alikuja shtuka yupo Hosp. Ami yake akiwa pembeni na watu wengine. Baadaye ndo ami yake akamuuliza uliona nini Mau. Mau akaelezea na sasa amerudi home lakini anasema sometime anahisi akili yake kama haipo sawa kapewa mapumziko ya week 1.

Maulid ananambia ni kweli Duniani Hatupo peke yetu. Nashindwa kuelewa je, yupo sahihi au amepata tatizo kwenye Ubongo?
 
Vitabu vyote vya dini vinasema Mungu aliumba vinavyoonekana na visivyoonekana so sishangai hii.
Tena ufunuo 12 inasema Ibilisi akatupwa na malaika zake, ina maana mambo ya kiroho yapo.

Kama Mungu anatambua uwepo huo, why mwanadamu upinge?

Uchawi na uganga vyote vinatambulika kiroho, hakuna cha ajabu hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom