Duniani hakuna haki! Nimeibiwa simu na pesa na kupigwa chupa ila bado nikashitakiwa

si kila kitu kutumia akili huku uswazi kuna manunda ukiweka busara mbele utalia kila siku
kwahiyo hapo wewe uliyetumia nguvu na bado kibano ukala bado tu hujaona kuwa wewe ni mpumbavu .siku nyingine fikiri kabla ya kutenda
 
Nenda tu kwenye mahakama ya mnyonge a.k.a kwa sangoma ukaloge maana ukirudi polisi utaenda kuchezea rungu siyo chupa tena
 
Sca
Aaah kubabake yani hiyo nisingekubali ikalala ushindi ukiwa kwao, kama wamenidhibiti kwasababu ya wingi hilo sio swala

Huku mtaani kuna wana ukiwapa 20k wanakichafua, hao mabaunsa wanapoteana na hicho kioski hapo kinakua mbuga
Nitafute inbox
 
Habar wadau najua humu kuna watu BIGGER THINKER mtanishauri vyema jana ndo nimeamini dunian hakuna haki dunia hii ione hvhv tambala bovu duh !!!! namshukuru mungu sikuumia sana japo nilipata uvimbe sehemu ya taya kwa nje kwenye shavu hii ni baada ya kupigwa na chupa nne za kichwa duh haya maisha haya unajua nn chanzo twende pamoja

WEMA NDIO ULINIPONZA

Miezi kadhaa nyuma nililetewa habar nzur tu na rafik yangu kuwa dada yake kafungua kioks ivo niende kumuunga basi bwana kidume nikatinga ili kuweka mambo sawa km mchango ili baa ionekane kubwa aiseeee ile nafika pale mm sinywi bia nakunywa grand malta kwanza nikashangaaa unakunywa bia bili hazielewek chengi hawarudish kila ukiomba chenj basi unaingia kwenye mjadala mzito huku uyo sista akijifanya km anakuelewesha vile nia yake kuu ni kukuchosha upotezeee io chenji

Nikiwa nataka nisepe dada akaniomba elfu 10 nimuazime ili aweke vinywaji store kapungukiwa pesa atarudisha nikampa toka siku io ni chenga tu kila nikimkumbusha kesho kesho kesho mwisho akasema kampa mdogo wake anipe nikamtafuta mdogo wake anipe akaniambia hajapewa hela siku zikapita sasa jana ndio balaa limeanzia hapo

Jana nilikuwa nimefulia nina elfu 14 tu mfukon alafu mambo yangu kibao hayako sawa dili zimebuma sijala kuna vidonge pia apo sijamumua aiseeee nikaona tu leo ngoja tu niifate elfu 10 yangu najuta kuchukua uamuzi huu

Nikafika kwenye baa nikamkuta uyo dada nikamwambia nipe pesa yangu akasema kampa bahat nikamwambia bahati mm simjui nakujua wewe wewe ndio nimekuazima kukatokea mzozo ebwana eeeh dada kanyanyua chupa kanipiga nayo ya kichwa dah hasira zilinipanda nami nikachukua chupa nirudishe kuna jamaa sijui ni bwana wake akaniwah kanikumbatia nikashindwa kurusha ile chupa sasa kipindi jamaa kanikumbatia dada kachukua chupa nyingine nikapigwa chupa ya pili tena kichwan hasira ziliongezeka vurugu ikazid kuwa kubwa nikakamatwa na midume km mitatu hv ili nisilete vurugu dah wakanipeleka mpaka nyuma upande wa nyuma wa baa wakaniuliza shida nini bro nikawa naelezea ile sijakaa sawa nikapigwa chupa nyingine tena kichwan

Kumbe wale watu wa upande ule kule demu hata hawamshiki wanamgusagusa tu demu akipata uwazi anarusha chupa mm huku nimeshikwa siwez hata kurusha ngumi kuja shtuka na simu samsung galaxy a12 nshaibiwa na jamaa mmoja kati ya walionishika nawaambia watu nimeibiwa simu hamna anayenisikiliza sijakaa sawa nikapigwa chupa nyingine apa saa nikatumia nguvu zangu zote nikawasukuma walionishika nikamshika demu nikamkunja japo kuna mtu alikuwa kati tukasukumizana apo mpaka chini yule jamaa wa kati ndio yule jamaa yake nikawa nataka nimsukume ili nibaki na yule dada man to man aisee sikupata uwazi wa kurusha hata ngumi moja

Yule jamaa akaubeba ugomvi nikianza kupigana na yule jamaa jamaa linasema “ weweeeeee unapigana na demu tukatwangana makonde kadhaa apo wale jamaa wengine wakaja kunishika tena hapa nilichomolewa zile elfu 14 live bila chenga wakawa wananipiga wanasema naleta vurugu ngumi ziliendelea apo hamna hata njia ya kupita baa imekuwa ndogo wahuni wangu walikuwa wapo mbali sikuwa na mtu wa kunitetea mpaka alipokuja dada mmoja hv anayenijua apo nmekunjana na lile jamaa ambalo sijui ndio demu wake washikaji wanamuita mwarabu jamaa linaniambia nikae chini nikamwambia sikai kwan wewe ni polisi mpaka uniamlishe nikae chini

Nikapiga hesabu yule dada kashika chupa nyingine anatafuta upenyo huku mm na mwarabu tumekunjana wale vibaka nao wananichangia mm nikasema nikiiita mwizi hapa nakufa mimi ngoja nisepe nikaita boda boda nikaenda adi kituo cha polisi niliwa polisi natoa maelezo akaja yule dada na wapambe wake wakasema nimeleta fujo baa nimefika na kumwaga bia zote bia zote chini nimemchania sidiria nimemtegua mkono nimempiga na chupa za kichwa na wapambe wakawa wanajazia na mimi nikajielezea polisi wakaona mm ndio mtuhumiwa nikaamrishwa nikae chini nikataka kulinzisha tena apo kituon ila nikajua ningepokea dozi NO MATTER WHAT IKABID NIWE MPOLE HATA WALE MAPOLISI AMBAO nawafahamu ajabu wamenichunia

Nikawa nasali kimoyo moyo uko nje wadau wangu walifika wakaliua so sijui walimalizana vipi mm nikakuta so lishaisha nikafungua kesi nyingine nimeibiwa simu na pesa aiseee mpemba nae anasema kaibiwa kali sita mmh kimoyo moyo nikasema mwongooooooo

APA NINA HASIRA SANA UNASAIDIA WW UNAPIGWA WW UNASHITAKIWA WEWE YAANI BALAA TUPU NIFANYEJE WADAU

Mnisamehe kwa mwandiko nimevurugwa
.
images%20(19).jpg
 
kwahiyo hapo wewe uliyetumia nguvu na bado kibano ukala bado tu hujaona kuwa wewe ni mpumbavu .siku nyingine fikiri kabla ya kutenda
Eti fikiri kabla ya kutenda ngoja nucheke kwanza muda wa kufikir uuotoe wapi tafuta watu ambao haijakufika huwa mnajiona much know
ww ndio mpumbavu kabisa tena ungekufa kifo kitakatifu chupa zisharushwa bado unataka utumie akili vita ikishaanza usitafute aman utakuwa wa kwanza kufa apo unadai eti nimepokea kibano uwezi kusema umenipiga ilihali niko unarmed tena nimeshikiliwa mikono yangu ilipata nafasi chache sn lkn uyo dada alienda chini embu waza km ningepata uwanja 100 percent bila kushikwa na yoyote yule nn kingefuata
 
Umenikumbusha mbali Sana! Story kidogo zifanane Ila Mimi Moto niliowasha hawatakaa wasahau na heshima ipo mpaka leo!
Kwenye swala la pesa yangu hata Kama Ni shilingi 100 unirushi kibabe uwe mwanamke sijui pisi Kali au Nani!
Bora unieleze ukweli au unipige saundi hata nikupotezee
 
Back
Top Bottom