Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,227
- 26,047
1. Wakati wa harakati za kupinga ubaguzi wa rangi Afrika ya Kusini ni watu wachache sana wenye ujasiri walioongoza harakati zile. Wengi wakiwemo waliokuwa wanafanya kazi kwenye mashamba na makampuni ya wazungu waliona sio sawa na walipinga harakati za kina Mandela na Walter Sisulu. Wengi waliona ingawa wanafanya kazi na kupata mishahara basi hakuna shida kumbe hawakujua harakati zile zingewanufaisha wao na vizazi vyao Leo hii harakati zimeisha na wao na vizazi vyao wanaona mabadiliko makubwa.
2. Wakati wa harakati za uhuru kwenye nchi za Africa ikiwemo Tanzania, sio watu wote waliunga mkono. Wengi waliona ni sawa kutawaliwa na wazungu. Ila baada ya Uhuru wengi walijitokeza kuwapongeza kina Nyerere na watu waliopigania uhuru na walifaidika wao na vizazi vyao.
3. Wakati wa mapinduzi ya Ufaransa, kuna wengi ambao waliunga mkono utawala wa kifalme ufaransa na waliona wapigania mapinduzi Kama watu wanaopoteza mda na wangepigwa na kuumizwa na askari na wasingepata kitu. Ila Leo hii baada ya Mapinduzi ya ufaransa, vizazi vyao vinafurahia maisha.
4. Wakati Martin Luther King wa Marekani anapigania haki za weusi pamoja na kina Malcom X kuna watu waliwaona kama watu wanaopoteza muda na kukataa kuwaunga mkono wakifikiri kuwa wangeuliwa na kukatizwa maisha ya duniani. Ila baada ya harakati za Martin Luther King na Malcom X Kufanikiwa vizazi vya wale waliokuwa wakiwakebehi ndio hawa leo wanafurahia maisha mazuri Marekani.
Tunajifunza nini?
Chadema na ACT watakebehiwa sana na watanzania ( baadhi) kuhusu kuandamana, wataambiwa andamaneni nyie, nendeni na wake zenu na watoto wenu. Mara sie hatutaki kupigwa risasi. Ila siku madai yanayodaiwa na Chadema na ACT yakifanikiwa ni watanzania hawahawa na vizazi vyao ndio watakuja kufaidika na mabadiliko yanayodaiwa Leo na watakuja kuwasifu sana Chadema na ACT kwa hizi harakati zao za leo.
Rai yangu kwa Chadema na ACT.
Endeleeni kupigania mnaloliamini, Tupo watanzania tunaowaunga mkono. Kwa wale ambao hawawaungi mkono na wanawakebehi, wala msijali, watakuja kuwashukuru siku moja. Mlilolianza wala msirudi nyuma hadi likamilike.
No Hate No Fear!