TheMnyonge
JF-Expert Member
- Mar 25, 2022
- 739
- 1,869
Juzi ijumaa nilimtembelea mpwa wangu shule ya sekondari MGULASI, hii ni shule ya kata ya CHAMWINO iliyopo Manispaa ya Morogoro!
Nilienda kupata ufafanuzi wa maendeleo mabovu ya huyo mpwa wangu, nilipofika nikaona msingi uliochimbwa na kutelekezwa (inaelekea ilikuwa ujenzi wa madarasa, lakini uliishia kuchimbwa na kuachwa) japo ujenzi unaendelea eneo la uwanja wa mpira wa miguu, inamaana shule hii haitakuwa na uwanja wa mpira kwa wanafunzi wa shule hii?
Kubwa zaidi, nilishangazwa na idadi kubwa ya wanafunzi ukilinganisha na idadi ya walimu, mwalimu alinifahamisha kwamba shule ina wanafunzi zaidi ya 1600, lakini ina walimu 57 tu, najiuliza watu wenye dhamana ya kusimamia elimu yetu wanaona sawa? Hivi watoto wao wangekuwa kwenye hizi shule wangeacha watoto wao wajazane namna hii?
Niliambiwa kwamba madara yanayojengwa ni kwa ajili ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza 2023, wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 800!
Katika maandalizi hayo, hakuna ongezeko la walimu, hii ina maana kwamba Mwl. Mmoja wa somo X atawajibika kufundisha watoto 800! Hivi kuna muujiza gani unaweza kufanya wanafunzi wajifunze na kuelewa? Hivi Mwl gani ataweza kutoa kazi na kuzisahihisha ipasavyo kwa wanafunzi 800 pèke yake?
Naamini Kuna uwezekano mkubwa hali ikawa hivyo kwenye maeneo mengine mengi nchini, kama ndiyo watoto wetu wanapata elimu ya namna gani?
Au zikishakuwa shule za sisi masikini basi inakuwa bora liende? Kwa kadri muda unavyokwenda matokeo ya shule za umma hasa za kata, yanazidi kuzorota, sio kwa sababu yoyote, isipokuwa mlundikano mkubwa wa wanafunzi bila kuwa n'a idadi ya kutosha ya walimu.
Walimu wapo wengi sana mtaani, waajirini wasaidie kusukuma gurudumu la elimu nchini, nina hakika MGULASI SEKONDARI itakuwa na matokeo mabovu mno, kwa nilivyoona kutokana na sababu nilizozisema hapo juu.
Wenye dhamana mkumbuke, hata sisi masikini tunastahili elimu bora, tungeweza kuwapeleka watoto wetu huko mnakowapeleka nyie, ila kwa kuwa mnatukamua kodi n'a tozo kubwa kubwa bila huruma, tunashindwa!
Walau basi tupeni walimu wengi, kukidhi mahitaji ya watoto wetu, vinginevyo inakuwa dhuluma kubwa sana mnapotumia pesa nyingi kununua magari ta kifahari, na kutumia kodi zetu kulipia watoto wenu shule kubwa kubwa na za ghali, huku sisi tukiendelea kutopea kwenye umasikini!
Viongozi wetu, iangalieni elimu kwa jicho la kipekee, kwani ndiyo mkombozi wa familia nyingi masikini!