Dunia itakuwaje ikiwa Trump akiingia msituni kwa kutokubaliana na mambo yanayotokea Marekani?

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,011
6,542
wafuasi wa rais donald Trump wakiwa capitol hil

Polisi imethibitisha kuwa mwanamke mmoja aliyepigwa risasi wakati wa vurugu zilizotokea baada ya wafuasi wa Trump kuvamia bunge, amefariki dunia kwasababu ya majeraha aliyopata.

Bado maafisa hawajataja jina la mwanamke huyo lakini polisi wanasema alikuwa raia wa kawaida.

Aidha, mtu mwingine amepigwa risasi wakati wa vurugu zilizotokea ndani ya bunge la Marekani, kulingana na shirika la habari la Associated Press.

Lindsay Watts, mwanahabari wa shirika lenye kuhusishwa na Fox News, ameandika ujumbe kwenye Twitter kuwa wahudumu wa afya wa Washington DC walisema juhudi za kumuokoa mwanamke mmoja aliye kwenye hali mahututi zinaendelea baada ya kupigwa risasi kifuani.

Wafuasi wa Trump waliokuwa na hasira waliandamana huku wakiimba, "Tunamtaka Trump" huku mmoja wao akipigwa picha akiwa ameketi kwenye kiti cha rais wa bunge la Seneti.

Polisi Washington imesema kuwa ni wazi waandamanji hao walikuwa tayari kutumia nguvu yoyote ile kuingia katika majengo ya bunge.

Huku akiwa ameketi katika kiti cha spika wa bunge la wawakilishi Nancy Pelosi mmoja ya waandamanaji hao aliwacha ujumbe uliosema hatutakubali

Maelezo ya picha,
Huku akiwa ameketi katika kiti cha spika wa bunge la wawakilishi Nancy Pelosi mmoja ya waandamanaji hao aliwacha ujumbe uliosema hatutakubali

Inasemekana hadi kufikia sasa watu 13 na silaha tano zimenaswa na polisi wakati ghasia zinaendelea bungeni.

Maafisa polisi wa Washington DC wamesema wamepata bunduki tano ikiwemo za mkononi na ndefu.

Mkuu wa polisi Robert Contee amewaambia wanahabari kuwa waliokamatwa sio wakazi wa eneo la DC.

Vitoa machozi vilitumika kuwatawanya waandamanaji hao

Maelezo ya picha,
Vitoa machozi vilitumika kuwatawanya waandamanaji hao

Baada ya uvamizi huo uliochukua saa kadhaa, afisa anayesimamia mipangilio ya bungeni alitangaza kuwa sasa jengo hilo limenusuriwa na vikosi vya usalama.

Wakati mmoja Bwana Trump alilazimika kurekodi ujumbe kwenye video na kuutuma katika mtandao wa Twitter akitoa wito kwa wafuasi wake kuondoka katika majengo ya bunge lakini naye akawa anaendelea madai yasiokuwa na ushahidi wowote kuwa Democrats waliiba kura.

Lakini kukawa na ishara kidogo zinazoonesha kwamba waandamanaji hao wanatii wito wa Trump unaowataka warejee nyumbani licha ya kwamba mji huo wote unatekeleza hatua ya kutoka nje kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi kumi na mbili asubuhi.

"Najua machungu yenu, najua mumevunjika moyo," Trump alisema. "Lakini lazima sasa murejee nyumbani, lazima tuwe na amani ... hatutaki yeyote ajeruhiwe."

Bwana Biden kwa upande wake amesema maandamano hayo "yamesababishwa na uchochezi na ni lazima hilo likome sasa", amesema.

Wanajeshi na maafisa wa polisi pia wamepelekwa katika majimbo jirani huku maafisa wa shirika la ujasusi FBI wakipelekwa katika majengo ya bunge kusaidiana na maafisa wa polisi.

Mwandamanaji mmoja aruka kutoka juu na kuingia katika bunge la seneti

Maelezo ya picha,
Mwandamanaji mmoja aruka kutoka juu na kuingia katika bunge la seneti

Pia amethbitisha kuwa baadhi ya maafisa wanapata matibabu baada ya kujeruhiwa.

Wafuasi wa Donald Trump wenye hasira wamevuka mipaka ya usalama iliyowekwa na kusimama kandokando ya bunge huko Washington, wakati wabunge wanakutana kumuidhinisha rais mteule Joe Biden kama mshindi wa uchaguzi uliofanyika Novemba mwaka jana.

Katika matukio ya kutatanisha, waandamanaji walizunguka jengo la bunge huku wabunge nao wakisindikizwa kutoka bungeni humo na polisi.

Bwana Biden alisema huo ni "uasi", huku Bwana Trump kwa upande wake akatoa ujumbe kwa njia ya video akiwataka wafuasi wake kutoka bungeni na kurejea nyumbani.

Maafisa wa polisi walikabiliana na wafuasi wao huku baadhi yao wakijeruhiwa

Maelezo ya picha,
Maafisa wa polisi walikabiliana na wafuasi wao huku baadhi yao wakijeruhiwa

Kikao cha pamoja cha bunge kuidhinisha ushindi wa Bwana Biden kimeahirishwa na bunge limelazimika kwenda mapumzikoni.

Kuna taarifa kuwa watu walitumia bunduki kwenye jengo hilo .Pia mabomu ya kutoa machozi yametumika kutawanya waandamanaji.

Viongozi duniani walaani uvamizi wa bunge Marekani​

Boris Jonhson

Kitendo hicho kimelazimisha kuahirishwa kwa muda kikao maalum cha kumuidhinisha Biden mshindi.

Viongozi wengi wametoa wito wa amani na ubadilishanaji wa madaraka kwa njia ya utulivu, wakielezea uvamizi uliotokea kama wenye "kuogofya na uvamizi wa demokrasia".

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, amelaani kitendo hicho na kusema ni "aibu".

"Marekani inasimamia demokrasia kote duniani na ni muhimu sana kuwa na ubadilishanaji wa madaraka kwa njia ya amani na wenye mpangilio," ameandika kwenye mtandao wa Twitter.

Viongozi wengine wa kisiasa Marekani wamekosoa ghasia hizo huku kiongozi wa upinzani Sir Keir Starmer akitaja kitendo hicho kama "uvamizi wa moja kwa moja wa demokrasia".

Wazriri wa kwanza wa Scotland Nicola Sturgeon ameandika kuwa kinachotokea bungeni "kinatia hofu mno".

Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sánchez amesema: "Nina imani na demokrasia ya Marekani. Uongozi wa rais mpya Joe Biden utakabiliana na kipindi hiki kigumu, kuunganisha watu wa Marekani."

Bunge la Marekani

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian amelaani kitendo hicho na kusema ni "uvamizi mbaya dhidi ya demokrasia", huku mwenzake wa Ujerumani, Heiko Maas, akisema bwana Trump na wafuasi wake "lazima wakubali uamuzi wa wapiga kura wa Marekani na waache kutatiza demokrasia".

Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel amesema kuwa aliamini sana Marekani "katika kuhakikisha ubadilishanaji wa madaraka kwa njia ya amani" kwa Bwana Biden, na Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen amesema ana matarajio makubwa ya ushirikiano na chama cha Democrat.

Katibu Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg aliungana na wale waliosema matokeo ya uchaguzi ni lazima yaheshimiwe.

Waandamanaji waliingia na kutawala jengo la bunge

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema raia wake "wamehuzunishwa sana na kitendo hicho cha uvamizi wa demokrasia".
 
Marekani yeye anasema wenzake wasibinye democracy.
Lakini wao pia wanabinya democracy vilevile.
Now na wao wameonyesha udhaifu wao waliokuwa wanaouficha.

Still kuna watu Africans wanadhani wazungu wote ni demigods.
Walichotuzidi ni wao kuanza kujitambua na kufikiria nje ya box sio wazungu wote lakini tuseme 10 percent ndio waliofanya yote.

Ona sasa wanavyojitia aibu hii inaonyesha africans tunaweza kudevelop kushinda wao.
 
Ndo matokeo ya kumpa mcheza mieleka nchi. Huyo Trump ni muhuni tu! wazungu nao sometimes wanakuaga hawana akili
Kwani unadhani wazungu wote wana akili?
Marekani imekuwa powerful kwa akili za watu wachache na sio wananchi wote wa marekani.
Hao wengine wapo kwenye reli tu.

Hata wao wanapiga stori za tunda kimasihara ila huwaoni.
Au wasingefanya huo ujinga wa kujitia aibu.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom