Dunia isiyokuwa na mipaka ya nchi au dini.

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,346
45,702
Duni ingekuwa sehemu ya aina gani kama kusingekuwa na nchi na mipaka yake? Yani fikiria unatembea bara zima la Africa na dunia yote bila kuhitaji passport au visa!

Hakuna majeshi ya kulinda mipaka au watu kufa kwa sababu wanazipigania nchi zao.

Pia dunia ingekuwa ya aina gani kama kusingekuwa na dini kabisa? Yani hakuna watu wanaobishana kuhusu dini ya kweli ni ipi au wanaopigana kwa sababu ya dini.

John Lennon, Muingereza mwanamuziki alipata kuuliza maswali haya na akajijibu Dunia ingekuwa sehemu salama sana isiyokuwa na vita.
 
Hata tukiifuta leo mipaka bado mipaka itakuja tu. Maana binadam anataka madaraka. Huyohuyo kiongozi wa dunia angepata upinzani ambao ungesababisha mipaka na utengano.
 
Unaambiwa jamii haiwezi kuwa sawa kwa 100%. Yaan dini na mipaka vikiondolewa, bado kitaibuka kitu kingine tena cha kutenganisha watu. Mfano: kuna baadhi ya nchi zinapigana kisa dini, lakin kuna nchi zinafuata dini moja ila kinachowapiganisha ni ukabila, pia kuna nchi ni kabila moja lakini kinacho wapiganisha ni unyonyaji uliopo baina ya maskin na tajiri, pia kuna nchi za matajiri ila kinachowagombanisha ni madaraka, hivyo hivyo kunawengine kinachowagombanisha ni ubaguzi wa rangi, wengine wanafarakana kisa Elimu baina ya wasomi na wasio soma. Nakadhalika yaan jamii haiwezi kuwa sawa 100%. Huu ni mtizamo wangu lakini
 
Binadamu ni social impafect creature, kuna baadhi ya viumbe wanaishi kwenye harmony kuliko binadamu, they don't kill each other
 
Back
Top Bottom