Lukwangule
Senior Member
- May 25, 2009
- 157
- 2
Kuna majanga mengi yanatokea duniani hasa yanayohusiana na mabadiliko ya tabia nchi, matetemeko na milipuko ya volkano.Maelezo haya yanayokuja chini ni matokeo ya maneno na maulizo niliyokutana nayo na washiriki wenzangu ndani ya JF wakizungumzia Haiti na Chile na Japan pia. lakini kuna tetemeko kubw ala China na nikasema ngoja namie niwapatie watu mambo niliyosoma katika kitabu kimoja kilichopandikwa 2004 Hercolubus or Red Planet.
Kitabu hiki niliomba niletewe baada ya kukisoma katika mtandao na kweli watu hao waliniletea. Ukikisoma kitabu hiki walahi unaweza kupatwa na wazimu.
Lakini siku zote wanadamu ndio chanzo cha wazimu wa wanadamu wenzao. Kitabu hiki hakiingiliani na imani zako ingawa unatakiwa kwenda na akili katika kukisoma.
Ni kitabu ambacho kinaelezea kinagaubaga kwa mfumo wa akili tambuzi kuhusu maangamizi ya dunia hii.
Kitabu hiki hakina uhusiano wa wazi na Biblia ambayo ninajenga mazoea ya kuisoma.Lakini ndani ya kitabu neno upendo na utunzaji wa mazingira ni kitu kinachozungumzwa sana. Kitabu hiki kinaitwa Hercolubus or Red Planet.
Kwa mujibu wa mwandishi, kitabu hiki ni onyo kwa wanadamu kuhusu maangamizi ya dunia wanaoishi kutokana na kuwa sayari Hercolubus kuendelea kuikaribia dunia.
Imeelezwa kuwa sayari hii kubwa ina nguvu kubwa ya mvutano ambayo itasababisha matetemeko ya ghafla yaliyo makubwa na yanayoweza kutokea kwa mkupuo mmoja pamoja, mawimbi makubwa ya bahari, milipuko ya volkano na mambo mengine ambayo ni tishio kubwa kwa sayari hii ya wanadamu.
Kitabu kimeelezwa kuwa matukio yatazidi ukubwa na ukali wake kwa jinsi sayari hiyo inavyozidi kuiakribia dunia na hali itaendelea mpaka dunia itakapomezwa na kuangamizwa kabisa.
Mwandishi V.M. Rabolú anaelea kwa undani majanga yanayoikabiuri dunia ikiwa na pamoja na yale ambayo tayari yameshaanza kutokea yakiwa ni ishara ya uharibifu mkubwa duniani.
Pia katika kitabu chake kuna kitu alichodai ni fomula ya kuepuka maangamizi.
kwa maelezo zaidi ingia http:lukwangule.blogspot.com