Dunia inazungukaje?

Wa huwa lladhi khalaqa allailia wa nnahaara washhamsa waalqamara kullu fii FALAKIN YASHBAHUUN. (21:33).

Soma tarjama ya aya hiyo hapa chini.

Anasema Allah aliye juu :

33. Na Yeye ndiye aliye umba usiku na mchana na jua na mwezi, vyote katika anga vinaogelea. (al Anbiyaa : 33 )

Sijaona hapo dunia iko wapi ?
 
Nakuuliza swali,vipi Sayansi inapooingana na Qur'aan unachukua lipi ?

Qur'an ndiyo ya kufuatwa kwanza, na wanasayansi wote walioifuta Qur'an siku zote waliibuka kidedea, kumbuka Sayansi inahusisha tafiti mbalimbali, lakini misingi yake inaweza kupatikana kutoka ndani ya Qur'an. Qur'an inaweka misingi tu.

Mfano, "the Big bang"--- Qur'an ilishaieleza kabla ya hao wanasayansi, na labda huyo mwanasayansi alisoma kwanza Qur'an ndipo akaja na hiyo theory.
 
Soma tarjama ya aya hiyo hapa chini.

Anasema Allah aliye juu :

33. Na Yeye ndiye aliye umba usiku na mchana na jua na mwezi, vyote katika anga vinaogelea. (al Anbiyaa : 33 )

Sijaona hapo dunia iko wapi ?

Neno "yashbauun" pia lina maana ya kuzunguka, (revolve/orbiting).
 
Mfano, "the Big bang"--- Qur'an ilishaieleza kabla ya hao wanasayansi, na labda huyo mwanasayansi alisoma kwanza Qur'an ndipo akaja na hiyo theory.

Haya ni makosa ambayo wanayafanya wengi katika wama harakati wa Kiislamu katika kuifasiri Qur'aan.

Qur'aan haizungumzii Big Bang sababu ule ni uumbaji ambao aliufanya Allah aliye juu kwa kutoa amri. Ukiisoma nadharia ya "Kishindo kikubwa" (Big Bang) huelezwi nani alisababisha hilo,kwahiyo unaposema Qur'aan imeelezea "Big Bang" kwanza unaonyesha huijui nadharia hiyo pili,unaikosea adabu Qur'aan.
 
Neno "yashbauun" pia lina maana ya kuzunguka, (revolve/orbiting).
Jitahidi uwe unaandika matini yenyewe ya kiarabu au tarjama yake,ili kuepusha makosa ya kiandishi.

Hapo ukisoma inaonyesha umeweka "Shiin" badala ya "Siin" kama ilivyokuja katika aya. Yaani ni " يَسْبَحُونَ ". Pia naona kwenye " Haau" umeweka "Hamza".

Sasa hapo vinavyozunguka katika vituo vyake ni dunia au jua na mwezi ? Aya iko wazi inazungumzia Jua na Mwezi. Nataka unionyeshe wapi Qur'aan imesema Dunia inazunguka ?
 
Qur'an ndiyo ya kufuatwa kwanza, na wanasayansi wote walioifuta Qur'an siku zote waliibuka kidedea, kumbuka Sayansi inahusisha tafiti mbalimbali, lakini misingi yake inaweza kupatikana kutoka ndani ya Qur'an. Qur'an inaweka misingi tu.

Mfano, "the Big bang"--- Qur'an ilishaieleza kabla ya hao wanasayansi, na labda huyo mwanasayansi alisoma kwanza Qur'an ndipo akaja na hiyo theory.

Kwa kukusaidia sababu unaonekana unapenda kusoma vitabu,tafuta kitabu kiitwacho " Big Bang Cosmology And The Qurʾān " kilichoandikwa na Abuu Iyadh,kitakusaidia sana katika suala hilo.
 
Jitahidi uwe unaandika matini yenyewe ya kiarabu au tarjama yake,ili kuepusha makosa ya kiandishi.

Hapo ukisoma inaonyesha umeweka "Shiin" badala ya "Siin" kama ilivyokuja katika aya. Yaani ni " يَسْبَحُونَ ". Pia naona kwenye " Haau" umeweka "Hamza".

Sasa hapo vinavyozunguka katika vituo vyake ni dunia au jua na mwezi ? Aya iko wazi inazungumzia Jua na Mwezi. Nataka unionyeshe wapi Qur'aan imesema Dunia inazunguka ?

Samahani, nimefanya makosa ya kiuandishi, ni "yasbahuun" key pad yangu ya karabu haina option ya kuwekea irabu,

Nilikuwa naangalia ndani ya kamusi la kiarabu (Lane &Aqrab) neno Yasbauun, mzizi wake ni "sabah" na masna yake ni kuogelea/ kuelea (glide along) na siyo kama nilivyosema hapo awali kwamba inaweza pia kuwa na maana ya kuzunguka/revolve hapo nilikosea. Neno lenyewe hasa ni lililopo katika hiyo aya ni "falakin", sasa tuangalie neno hilo (Lane & Aqrab) wanasemaje, hapo kuna (Mzungu na Muarabu);-

فلك (orbit) is derived from فلك (falaka), they say فلك ثدى الجارية ie the breast of the girl became round. فلك means the place of revolving of the stars ie the celestial sphere, the vault of heavens or the firmanent.

Hapa point ni hii "the place of the revolving of the stars ie the celestial sphere " ni mahali ambapo nyota huzunguka yaani ni mduara wa angani.

Kwakuwa usiku na mchana vivyotajwa kwenye hiyo aya hutokea hapa duniani na tafiti za kisayansi zimethibitisha hilo kwamba dunia inajizungusha kwenye yenyewe na kuzunguka jua basi Wanadayansi wapo sahihi kwa mujibu wa hii aya 21:33.

Huo ni ushahidi kwamba Qur'an ni kitabu kutoka kwa Mungu aliyeumba huu ulimwengu na hakuna kitabu chochote cha dini yoyote kilichosema jambo hilo ila ni Qur'an pekee na Sayansi imethibitisha jambo hilo hivyo Qur'an ni Maneno ya halisi ya Allah.
 
Nimeishia form four ila napenda kujua haya mambo,hivyo ukija na porojo ooh huna shule kasome utapoteza muda tu,tujadili hili suala.

Kuhusu jua na mwezi hivi bila shaka vinazunguka na nadharia yake iiko madhubuti kueleweka.lakini hii ya dunia kuzunguka imekaaje mbona inakanganya sana wadau?

Hii dunia kama inazunguka tena kwa spidi kubwa sana inakuwaje wale ambao wanatoka nje ya dunia wakirudi hurudia pale pale tu hata hawatui pengine?

Yaani muweke sisimizi kwenye tufe alafu jaalia pale alipo ndo anatoka duniani anaenda mbali katika sayari zinginee.jaalia umempaisha sasa alafu alipotoka katika anga ya dunia ile dunia(tufe)likawa linazunguka kwa spidi kali sana.umepata picha?.
Sasa je ili arudi na ile kasi ya dunia yenyewe kuzunguka naweza kutua pale pale kweli?

Hawa wanaopaa wannafanyaje mpaka wanaarudi pale pale walipotokea?

Naomba tueleweshane nipo hapa kujifunza wadau.sitaki kejelii

Mokaze
Shark

AL - ANBIYAA - 33
Na Yeye ndiye aliye umba usiku na mchana na jua na mwezi, vyote katika anga vinaogelea.

YA-SIN - 39
Na mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa kama karara kongwe

YA-SIN - 38
Na jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kijana Jua halizunguki hili weka akilini.

On average, the sun rotates on its axis once every 27 days. However, itsequator spins the fastest and takes about 24 days to rotate, while the poles take more than 30 days. The inner parts of the sun also spin faster than the outer layers, according to NASA.
 
Kwakuwa usiku na mchana vivyotajwa kwenye hiyo aya hutokea hapa duniani na tafiti za kisayansi zimethibitisha hilo kwamba dunia inajizungusha kwenye yenyewe na kuzunguka jua basi Wanadayansi wapo sahihi kwa mujibu wa hii aya 21:33.
Kaka naona unapata tabu sana,kwa kulazimisha mambo sio kweli,kwanza aya tunayo ijadili haionyeshi ya kuwa Dunia inazunguka,hapa hata nikupe miaka mia.

Nikikuuliza huo usiku na mchana unatokeaje,nalo litakuwa swali gumu kwako.

Allah aliye juu anasema :

5. Ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Hufunika usiku juu ya mchana, na hufunika mchana juu ya usiku. Na amefanya jua na mwezi vitumike. Kila kimojapo kinakwenda kwa kipindi kilicho wekewa. Jueni mtanabahi! Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe! ( az Zumar : 5 )

Sasa kazi ninayo kupa sasa hivi ni utuwekee hizo ithibati za kisayansi zinazo onyesha Dunia inazunguka.
 
Kaka, kabla sijakuwekea hizo ithibati za kisayansi ningependa kujua katika elimu ya kimazingira (secular education ) ulifika wapi, shule ya msingi, shule ya sekondari o/A level, au kiwango cha chuo ??, samahani kwa kukuuliza hilo swali kama litakuchukiza, lengo ni kwamba kwa kujua kiwango cha elimu yako nitajua nianze wapi kukufahamisha kwamba Dunia inajizungusha na pia inazunguka jua kupitia "falaki" (orbit) kama jinsi Qur'an inavyosema- ninasema hivyo kwakuwa usiku na mchana vinatokea hapa duniani, na tafiti za kisayansi kupitia nyenzo kama satellites, Telescope, na vyombo vya anga za juu vime-prove kwamba dunia ina-- revolve/rotates..

Shukrani kwa Allah aliyetupatia Akili na kutuwezesha sisi binadamu kujua mambo hayo na hivyo kujua sehemu ya uumbaji na utukufu wake na hivyo imani juu ya kuwepo kwake na uwezo wake juu ya kila kitu kuongezeka mioyoni mwetu.

Alhamdulillah.
 
Kaka, kabla sijakuwekea hizo ithibati za kisayansi ningependa kujua katika elimu ya kimazingira (secular education ) ulifika wapi, shule ya msingi, shule ya sekondari o/A level, au kiwango cha chuo ??, samahani kwa kukuuliza hilo swali kama litakuchukiza, lengo ni kwamba kwa kujua kiwango cha elimu yako nitajua nianze wapi kukufahamisha kwamba Dunia inajizungusha na pia inazunguka jua kupitia "falaki" (orbit) kama jinsi Qur'an inavyosema- ninasema hivyo kwakuwa usiku na mchana vinatokea hapa duniani, na tafiti za kisayansi kupitia nyenzo kama satellites, Telescope, na vyombo vya anga za juu vime-prove kwamba dunia ina-- revolve/rotates..
Sijaona haja ya kutaja kiwango changu cha elimu,sababu "secular education" haimsaidii mtu kuelewa mambo au kutoelewa mambo,sababu kuna mambo magumu tunayaelewa kuliko haya.

Kwanza kabla ya kuongelea Sayansi ulitakiwa ujue madhaifu na mipaka ya Sayansi,lakini hili unaonekana limekupita,sasa ulitakiwa kabla ya kujadiliana na mimi ujue misingi ya Sayansi ni nini ? Kwahiyo usitafute kichaka,jibu maswali yangu.

Nimekupa kazi unionyeshe ni aya gani inayo onyesha Dunia inajizungusha katika muhimili wake,unaleta aya kando kabisa kisha unahitimisha kwa kauli dhaifu sana.

Kitu kingine ninacho kushauri ni kuwa uwe unasoma tafsiri ya Qur'aan katika vitabu vyenye kutegemewa.

Kwanza nakuuliza swali dogo,huwa unasoma Tafsiri gani ya Qur'aan ?
 
Wewe ulitaka nikupe ithibati ya kisayansi, sasa ni vyema kabla sijashuka sayansi nijue kiwango chako cha elimu na hasa elimu ya sayansi, siwezi kukuelezea "Kepler laws of planetary motion" wakati hata Physics ya form 4, huijui. Kaka sina nia ya kukashifu au kuonyesha kwamba mimi ninajua zaidi, lakini nilitaka kukujuza kwa kadiri Allah alivyoniruzuku japo hichi kidogo.

Unauliza ni tafsiri ipi ya Qur'an ninaisoma??!!, na mimi nakuuliza Mtume mtukufu (saw) alisema tusoma tafsri ipi na ya nani??-- nijibu hapo nami nitakujibu.
 
Unauliza ni tafsiri ipi ya Qur'an ninaisoma??!!, na mimi nakuuliza Mtume mtukufu (saw) alisema tusoma tafsri ipi na ya nani??-- nijibu hapo nami nitakujibu.
Shule muhimu sana,bado nasisitiza ya kuwa huna haja ya wewe kujua nina kiwango gani cha elimu,sababu haitabadilisha kitu.

Mtume hajasema tusome Tafsiri gani ila uhalisia unataka tujue mtume aliwafasiria vipi maswahaba zake hizo aya,sababu aya zilipokuwa zinashuka alikuwa anawaambia maswahaba na maswahaba walikuwa wanamuuliza maana ya aya husika kisha wanaifanyia kazi. Hayo yote yamenukuliwa katika vitabu vya tafsiri,kwahiyo lazima tujue sababu ya kushuka hiyo aya a mtume aliielezea vipi na maswahaba waliielewa vipi na kuifanyia kazi vipi aya husika.

Kwahiyo ni lazima uniambie maana hiyo ya aya hiyo umeipata wapi ? Nasubiri jibu.
 
Kaka naona unapata tabu sana,kwa kulazimisha mambo sio kweli,kwanza aya tunayo ijadili haionyeshi ya kuwa Dunia inazunguka,hapa hata nikupe miaka mia.

Nikikuuliza huo usiku na mchana unatokeaje,nalo litakuwa swali gumu kwako.

Allah aliye juu anasema :

5. Ameumba mbingu na ardhi kwa Haki. Hufunika usiku juu ya mchana, na hufunika mchana juu ya usiku. Na amefanya jua na mwezi vitumike. Kila kimojapo kinakwenda kwa kipindi kilicho wekewa. Jueni mtanabahi! Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe! ( az Zumar : 5 )

Sasa kazi ninayo kupa sasa hivi ni utuwekee hizo ithibati za kisayansi zinazo onyesha Dunia inazunguka.
kuna uwezekano mkubwa sana wa kuwa hata dunia inazunguka hasa kwa mujibu wa Qurani.

Allah asema...

وَتَرَى الْجِبَالَ تَحْسَبُهَا جَامِدَةً وَهِيَ تَمُرُّ مَرَّ السَّحَابِ ۚ صُنْعَ اللَّهِ الَّذِي أَتْقَنَ كُلَّ شَيْءٍ ۚ إِنَّهُ خَبِيرٌ بِمَا تَفْعَلُونَ

[ AN-NAML - 88 ]
Na unaiona milima unaidhania imetulia; nayo inakwenda kama mwendo wa mawingu. Huo ndio ufundi wa Mwenyezi Mungu aliye tengeneza vilivyo kila kitu. Hakika Yeye anazo khabari za yote myatendayo.

kwanza kitendo cha Allah kusema "unadhani imetulia(static)"..?

hapo maana yake ni kinyume chake kwamba haijatulia(motion)
kitu chochote ambacho hakijatulia lazima kiwe kipo katika hali ya mwendo ama kcheza cheza.

lakini Allah akamalizia kwa kusema "NAYO INAKWENDA"

kumbe kinyume cha kutulia alichosema Allah pale basi maanayake ni kwenda.
mpaka hapo tumeona ya kwamba milima inakwenda haijatulia.

mkuu Mokaze na Zurri niwaulizeni

"MILIMA IPO WAPI KAMA SIO IMEAMBATANA NA ARDHI AMBAYO NDIO DUNIA YENYEWE HIYO ?

ni sawa na mtu awepo kwenye gari kisha gari inatembea alafu yeye aseme HAYUPO KWENYE MWENDO WAKATI PALE ALIPO KILE KITU KINATEMBEA.

Mkuu zurri angalia tafsiri ya shekhe Abdallah saleh alfarsiy رحمه الله katika tafsiri yake kaandika hivi..

"na hili vile vile ni katika hayo yaliyosemwa katika Qurani miaka 1400 leo na ndiyo kwanza sasa maulamaa wa huko wanatambua haya ya kuwa DUNIA INAZUNGUKA"

mwisho wa kunukuu.

mkuu zuri hapo utaona hata sheikhunaa Abdallah saleh anamafhumu hayo ya kuwa dunia inazunguka kwa mujibu wahiyo aya.sio mimi na mokaze ndo tumeleta ufahamu huo laa.

unasemaje juu ya tafsiri ya sheikh Abdallah saleh alfarsiy katika aya hiyo..?

lakini pia Allah akasemate tena..

خَلَقَ السَّمَاوَاتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ۖ وَأَلْقَىٰ فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَن تَمِيدَ بِكُمْ وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَابَّةٍ ۚ وَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَنبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍ كَرِيمٍ

[ LUQMAN - 10 ]
Ameziumba mbingu bila ya nguzo mnazo ziona; na ameweka katika ardhi milima ili ardhi isikuyumbisheni; na ametawanya humo kila namna ya wanyama; na tumeteremsha maji kutoka mbinguni, na tukaotesha katika ardhi mimea mizuri ya kila namna.

umeona Allah ufundi wake anasema kuwa ile MILIMA KAIWEKA ILI ARDHI ISIJE KUTUYUMBISHA..

sasa hapa tukiunganisha tutaona kwamba kumbe ardhi nayo inakwenda pamoja namilima na hyo ndo tunaita dunia.

Na Allah alituambia kwamba huko angani vitu vinaogelea kwa maana vinaelea tu.

nakama ardhi namilima inakwenda (inazunguka) inabidi iwe imara ili isiyumbe yumbe kwa maana ya kuwa ikiwa nyepesi basi inaweza kuwa UNSTABLE katika mwendo wake.

kumbe ile milima Allah kaiweka ili iongeze uzito naardhi isipate kuyumba yumba katika mwendo wake.

na hilo tunaona hata katika magari gari ikiwa na mwendo mkubwa na ikawa nyepesi basi haitulizani, ila ikiwa nzito gari na mw3ndo mrefu inakwenda bila shida waakuyumba yumba.

momentum = mass x velocity

mass haibadiliki kitu kikiwa kwenye mwendo bali velocity ndio inabadilika.

mass ikiwa kubwa kuliko kuliko air resistance basi mass haiwezi kuwa affected na hiyo air reststance kamwe.

kunamwaajeshi alipata kumuokoa mtu waati treni imepoteza muelekeo na spidi ilikuwa kali kiasi kwamba ukiruka kawaida utarushwa huko.

alichokifanya akamkamata mtu akaruka nae na eakafika chini salama tu bila kuyumba na kuumia kwa ile speed ya treni.

kwa hyo kitendo cha jamaa kumbeba mtu mwingin3 aliongeza uzito na hivyo hata waliporuka mass yao ilikuwa kubwa kuliko ile AIR na ikawafanya kufika chini salama.

Na Alla kaweka milima ili isituyumbishe na hapo tunaweza kuona kuwa milima Allah kaiwea ili mass ya dunia iongezeke.

tukisema dunia tunakusudia na ardhi ikiwemo ati.

mkuu Mokaze nadhani hapa unalo la kuongeza kutilia nyama viele, o hivi karibuu..
 
nakama ardhi namilima inakwenda (inazunguka) inabidi iwe imara ili isiyumbe yumbe kwa maana ya kuwa ikiwa nyepesi basi inaweza kuwa UNSTABLE katika mwendo wake.
Kaka naanzia hapa,kwani kutembea kwa mawingu ndio kunaonyesha mbingu inatembea ?

Pili,ili kitu kisiyumbe lazima kiwe kinatembea ?
 
na hilo tunaona hata katika magari gari ikiwa na mwendo mkubwa na ikawa nyepesi basi haitulizani, ila ikiwa nzito gari na mw3ndo mrefu inakwenda bila shida waakuyumba yumba.
Haya mambo mepesi sana,nawauliza maswali kwanza kabla ya kuleta maana ya hizo aya.

Unaweza kuniambia uelekeoa wa Dunia ikiwa inazunguka ni upi ?

Je dunia inaelea au haielei ?
 
Haya mambo mepesi sana,nawauliza maswali kwanza kabla ya kuleta maana ya hizo aya.

Unaweza kuniambia uelekeoa wa Dunia ikiwa inazunguka ni upi ?

Je dunia inaelea au haielei ?
sijui inaelekea wapi.

kutokujua kwangu mimi na wewe haikanushi kuwa haizunguki.

na wala sijui yangu haikanushi Aya inayosema kuwa Milima inskwenda.

unas3maje juu ya tafsiri ya shekhe abdallah saleh kuhusu iyo haya...?
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom