Dunia inawakumbuka waliofanya

Dunia yakoo

Senior Member
Nov 23, 2019
139
214
Watu wengi walipokuwa wanakutana na Albert Einstein jambo la kwanza walikuwa wanamuambia...

“Einstein, Mungu amekujalia akili nyingi sana, wewe ni Genius”.

Siku moja alipoambiwa hivyo akasema...


“Ngoja niwaambie siri ya akili zangu nyingi na mafanikio yangu imetoka wapi.

“It’s not that I’m so smart, it’s just that I stay with problems longer.”

(Sio kwamba nina akili kuliko ninyi wote, ni kwamba niko tayari kuvumilia kutafuta SULUHISHO la tatizo kwa muda mrefu bila KUKATA TAMAA).

Changamoto kubwa ya watu wengi sio kwamba wanakutana na MATATIZO MAKUBWA kuliko wengine...

...au HAWANA UWEZO wa kuyatatua, HAPANA.

Changamoto kubwa ya watu wengi ni KUKATA TAMAAA MAPEMA SANA.

Kama ambavyo vitu vingi viko “automatic” kwa sasa kuna watu wanataka wakianza tu wapate kila matokeo wanayotaka.

Wakiona haiko hivyo wanaharakisha kukata tamaa:

Wanaacha hilo wazo wanaenda lingine,

Wanasitisha mahusiano wanaanzisha mengine,

Wanaacha kazi wanatafuta nyingine n.k

Matokeo yake kila siku wanakuwa wanaanza UPYA kwenye kila kitu...

...na wanajikuta hakuna WANACHOKAMILISHA kwenye maisha yao.

Hii ndio maana Thomas Edson aliwahi kusema...

“Watu wengi waliofeli kwenye maisha ni wale amabo HAWAKUGUNDUA wako karibu sana na MAFANIKIO YAO”

- Wewe usiwe mmoja wao.

Kuna wengine wanajifariji wanasema...

“Nimejitahidi sana KILA MTU ANAJUA, hata nikiishia hapa WATANIELEWA”.

Kumbuka DUNIA haiwakumbuki waliojaribu kisha wakakata tamaa,

Haiwakumbuki WALIOISHIA NJIANI,

Haiwakumbuki waliosema NIMEJITAHIDI,

Inawakumbuka WALIOFANYA.

Maisha hayabadiliki kwa KUHALALISHA juhudi zako,

Yanabadilika kwa KUTOKUKATA TAMAA HADI UMEPATA UNACHOTAKA.
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom