Dunia inawahitaji Marais hawa kwa sasa

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Aug 28, 2020
2,204
2,083
Angalia hizi picha yupo mwamba rais Putin wa Urusi, yupo mwamba Rais wa China Xi Jinping, na yupo na mwamba Rais Dkt John Magufuli.

Screenshot_20200920_212043.jpg

Hawa ni baadhi ya Marais Bora kabisa wa kipindi hiki ambao wameyatoa mataifa yao kimasomaso kwenye Uchumi na kujenga mifumo imara. Mifumo imara ya uongozi usio yumbayumba.

Kumbuka kutengeneza mfumo imara wa uongozi usio yumbayumba sio lelemama. Lazima ujifunze mchezo wa tumbu na kutumbua. Bila hivyo huwezi. Huo mchezo ana uweza mwamba Dkt John Magufuli tu na hawa wenzetu Warusi na Wachina.

Warusi wanaona kuwa ili maono ya Taifa lao yakamilike lazima pale juu awepo mtu mbishi Kama Putin na asiyeyumbishwa na mataifa Mengine.

Marais wa aina hii huwa hawazaliwi kila Mara mnaweza mkampata Mara Moja katika kipindi Cha miaka Mia.

China na Urusi wanajua fika wapo kwenye Vita kubwa ya kiuchumi na mataifa Mengine. Watu pekee ambao wameona Wana msimamo na wanaweza kuhimili Vita hiyo ni Marais wao. Angalia China inavyowakaba Marekani kwa sasa, angalia Urusi wanavyoikaba Marekani kwa sasa....

Kwa sasa Tanzania imekuwa tishio kwa nchi nyingi kutokana na misimamo ya mwamba Dkt. Magufuli. Kwasasa Tanzania ni nchi inayo julikana kila pembe ya dunia kwasababu ya Mwamba Dkt John Magufuli.
Watu tukienda ughaibuni tunatembea vifua mbele kama bata kwasababu ya Tanzania ya sasa isiyo na michezo michezo.

Mitano tena kwa Mwamba Dkt John Magufuli.

By Ellyskywilly.
 
Siku nyingine huwa nawaeleza halafu hamfuati, niliwaambia mnichague mimi mkasema sawa, nikawaambia mnichagulie na mbunge wa CCM hamkunichagulia, nataka niwaeleze ukweli wala siwafichi asingekuwa Kapuya hii barabara nisingeijenga". Dkt.Magufuli
 
Kweli kabisa mtoa mada, maana hao jamaa kimamlaka hawataki kuondoka madarakani, huyo wa urusi ndiyo anafanya mpango aendelee kuishi pale ikulu ya Kremlin, huyo mwingine wa china soon utasikia baba wa uchina mpaka afie pale ikulu.

Haya angalau kwa hao wawili wanakutana na kujadili mustakabali wa dunia tena wanapanda ndege na kuzunguka duniani kuangalia na kubadilishana uzoefu na utendaji in/out.
 
Mkuu utafuata mkia tu ngoja oktoba ipite
 
Kweli kabisa maraisi wanaojenga viwanja vya kimataifa kijijini kwao hawazaliwi mara kwa mara. Hata Tanzania tumeona , wamepita maraisi 4 hawajajenga viwanja vya kimataifa vijijini kwao ila Magufuli amejenga
 
Viwanja ni sehemu ya maendeleo.
 
Kweli kabisa maraisi wanaojenga viwanja vya kimataifa kijijini kwao hawazaliwi mara kwa mara. Hata Tanzania tumeona , wamepita maraisi 4 hawajajenga viwanja vya kimataifa vijijini kwao ila Magufuli amejenga
Yote hayo ni maendeleo
 
Back
Top Bottom