Hivi karibuni, miji mingi nchini China ikiwemo Beijing, Shanghai na Guangzhou imezindua kazi ya kuwapatia kwa hiari raia wa kigeni chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19, ikiwa ni juhudi za kuwapa wageni haki sawa za kuchanjwa kama wachina.
Kijana Adhere Cavince kutoka Kenya ni mwanafunzi wa shahada ya tatu anayesoma katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Huazhong, mjini Wuhan na kazi ya kuchanjwa inaendelea katika chuo hicho. Hivi karibuni, katika makala aliyoandika kwenye gazeti la Daily Nation la Kenya, kijana huyo alisema, “wanafunzi wenzake wanasisimuka na uzoefu wa kuchanjwa, wana imani kubwa na chanjo ya China, na kuisifu serikali ya China kwa kuwapatia wanafunzi wa kigeni fursa ya kuchanjwa bure.”
Kuwapatia bure chanjo wanafunzi wa kigeni wanaosoma China ni kitendo halisi cha nchi hiyo kutekeleza sifa ya chanjo dhidi ya COVID-19 kuwa “bidhaa ya umma”. Kwa wanafunzi wa Afrika, hatua hiyo ina maana kubwa zaidi. Kwanza, idadi ya wanafunzi wa Afrika wanaosoma China ni kubwa. Takwimu zimeonesha kuwa, mwaka 2018, kati ya wanafunzi wa kigeni laki 5 waliosoma hapa China, asilimia 17 walitoka Afrika idadi ambayo ilishika nafasi ya pili kwa kulifuata bara la Asia.
Pili, si rahisi kuchanjwa Afrika. Hivi sasa wanafunzi wengi wa Afrika watakuwa au wamemaliza masomo yao nchini China na kuwa tayari kurudi nyumbani. Kutokana na athari ya “utaifa kuhusu chanjo”, nafasi ya kupata chanjo barani Afrika ni ndogo, haswa kwa wale ambao si watu wenye hatari ya kuambukizwa, uwezekano wa kuchanjwa ni karibu sifuri. Kwa hivyo baada ya kuchanjwa, wanafunzi wa Afrika wataweza kurudi nchini mwao, kwani sio tu wanajua si rahisi kwao kuambukizwa virusi, bali pia hawana hatari ya kuingiza virusi kwa jamii watakazoishi.
Ukweli ni kuwa baada ya mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19, jamii na idara mbalimbali za vyuo vikuu hapa China wametoa chakula, dawa, nguo za kujilinda na ushauri wa kiafya kwa wanafunzi wa kigeni, na kuwapatia raia wa kigeni wakiwemo wanafunzi chanjo dhidi ya ugonjwa huo ni mfano mwingine wa serikali ya China kuunga mkono juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo duniani.
Nje ya nchi, China inaongoza mchakato wa upatikanaji wa chanjo duniani, na kwa njia moja ama nyingine, inatoa chanjo kwa nchi na mashirika ya kimataifa zaidi ya 100, ili kutuwezesha sisi binadamu kujikwamua kwenye maambukizi makubwa ya COVID-19 hatua kwa hatua na kwa njia ya kibinadamu.
Kuhakikisha chanjo zinapatikana kwa usawa ni kulinda haki za binadamu, lakini kulimbikiza chanjo kunaweza kusababisha watu wengi duniani kuambukizwa virusi, na hata kupoteza maisha ambayo yangeweza kuokolewa. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO, hadi sasa dozi milioni 700 za chanjo dhidi ya COVID-19 zimetolewa kote duniani, lakini katika nchi zenye kipato cha juu, robo moja ya watu wamechanjwa, huku katika nchi zenye kipato cha chini, idadi hiyo ikiwa ni 1 kwa 500 tu.
Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Matshidiso Moeti wiki iliyopita mjini Nairobi alisema idadi ya watu waliochanjwa katika nchi za Afrika inachukua asilimia mbili tu ya watu waliochanjwa kote duniani, na usambazaji wa chanjo barani humo pia unakosa uwiano na kwamba nchi 10 zimepata asilimia 93 ya chanjo zote za Afrika.
Kwa nchi nyingi za Afrika, chanjo zilizotolewa na China ni sehemu ya kwanza ya chanjo kwao, zimepunguza kwa kiasi fulani“pengo la chanjo”kati ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea, na kuwezesha upatikanaji wa chanjo kwa watu wengi barani humo.
Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe aliielezea chanjo ya China kama ni “mwanga baada ya kiza kinene cha handaki”, rais Hage Geingob wa Namibia alisema “nchi zilizoendelea zinajiangalia zenyewe tu, na kuwasahau watu wa Afrika.” Naye makamu wa rais wa Guinea Ikweta Teodoro Nguema Obiang Mangue alisema, “ni China tu inatujali na kutusaidia.” Lakini kwa kutegemea juhudi ya China pekee haitoshi, “utaifa kuhusu chanjo” umedhoofisha vibaya hali ya kuaminiana kati ya nchi na nchi, na watu na watu.
Ni ndoto za Alinacha kwa binadamu kurudi kwenye maisha ya kawaida kama sehemu hata moja duniani itakuwa virusi vya Corona. Nchi mbalimbali zinatakiwa kushikilia wazo la “jumuiya yenye hatma ya pamoja”, kuvuka mipaka ya nchi katika usambazaji wa chanjo, kutoa msaada kwa nchi zenye mahitaji ili tumalize msukosuko huo wa kiafya kwa pamoja.