Dunia inaiangaza Tanzania na Mwenyekiti mpya wa SADC katika kadhia ya ndege kushikiliwa Afrika Kusini. Weledi ni muhimu kwenye kadhia hii

mwananyaso

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
2,829
3,118
Hili suala si jambo geni hapa duniani ni mambo ya kawaida kabisa kutokea ,

Ni imani yangu litatatuliwa katika njia sahihi kabisa na litapita,na yatakuja mengine.
kwani matatizo na furaha ni sehemu ya maisha ya kila siku kwetu wanadamu.

Cha msingi katika suala hili ni serikali kwa ujumla ikiongozwa na Amiri Jeshi Mkuu Rais Magufuli kuonyesha weledi katika kulimaliza suala hili.

Dunia inafuatilia kwa umakini kuona suala hili linamalizwaje ikizingatiwa yeye kwa sasa ndio chairman wa sadc.

Kumalizika kwa weledi kwa kadhia hii kutazidi kumuimarisha Rais Magufuli na serikali yake, pia kuonyesha kimataifa diplomasia yetu iko makini zaidi hapa duniani.

Kwani huu unaweza kua ni mtego makini kwa wasioitakia mema serikali hii na nchi kwa ujumla.

Ni wakati wa viongozi wetu kuwa makini na washikamane ,nasi wananchi wazalendo tuko pamoja nao,hakika tutashinda,ni vita ngumu inayohitaji umoja wetu.wachache wenzetu wanaobeza na kufurahia tukio hili, tuwasamehe na kuwaombea ili wazinduke na wapate ufahamu.

Mungu ibariki Tanzania na Afrika kwa ujumla wake.
 
Si mtumie mbinu zenu bora kabisa, kama zile , mlizozitumia kwa wapinzani wanahabari na wanaharakati nchini mwakomeshe kabisa mabeberu.
 
Wacha deni 'riripwe' tu mura 'richa' ya kwamba 'waripa' kodi ndo wanaoumia. 'Turirikoroga' wenyewe 2015, wacha 'turinywe'.
Kuna jamaa humu nilimnukuu akisema, "kucheka mcheke wenyewe ila kwenye kulia mtake tulie wote" dawa ya deni ni kulipa
 
Back
Top Bottom