Dunia ina watu milioni 70 wasioweza kusikia, 80% wanatokea nchi zinazoendelea

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Umoja wa Mataifa(UN) unaitumia siku ya Septemba 23 kila mwaka kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Lugha ya alama ambayo ni muhimu kwa wasioweza kusikia

Kuna watu milioni 70 wasioweza kusikia duniani ambapo 80% wanatokea katika nchi zinazoendelea. Mbali na kuwepo kwa lugha moja ya alama inayotambulika kimataifa, nchi mbalimbali zina lugha zao ambapo hadi sasa kuna lugha 300 za alama

UN unaitumia siku ya leo kuamsha uelewa wa lugha za alama na umuhimu wa lugha hizo katika mahali pa kutolea huduma ili kuwapa haki wasiokuwa na uwezo wa kusikia
 
Back
Top Bottom