Dunia imesimama na Rais Samia Suluhu Hassan hoja ya Teenage Mothers

Joao de Matos

JF-Expert Member
Jun 16, 2022
334
264
Mimba bila utaratibu ni laana.
Usimsingizie MUNGU mambo ya uongo.
MUNGU aliposema watu wakazaliane hakusema wazaliane hovyo hovyo bila ya kufuata taratibu za ndoa.

Biblia inasema wazi kabisa kuwa mtoto anayezaliwa nje ya ndoa ni "mtoto wa haramu".

Ifike mahala tuwe na heshima kwenye Maandiko ya MUNGU na kamwe tusilete "siasa" kwenye Maandiko ya MUNGU.
Mkuu hayo maneno yake , Mimi nimemwambia yeye atakuwa Ni mwakilishi wa Lucifer, kwa yeye anamahanisha kuwa watu wazaliane hovyo tuu bila kufuata taratibu.
 

Joao de Matos

JF-Expert Member
Jun 16, 2022
334
264
Siafiki kabisa watoto wanafunzi waliopata ujauzito kurejea shule rasmi.

Tafiti iliyofanyika hivi karibuni, kwa maelezo ya mshiriki ITV wa mada kuhusu hili suala, kati ya 2015-2019 wanafunzi waliopata ujauzito waliongezeka kwa 90%. Hakutoa sababu zaidi ya kulaumu kuwa katazo ndilo linachochea.

Ukweli ni kwamba tupo kwenye karne ya TEHAMA watoto wanaona ngono mitandaoni na hivyo kushawishika kujaribu. Kuruhusu warudi shuleni hakuna shaka kutachochea na kusababisha mlipuko wa watoto wazazi shuleni.
Serikali wengewe hawafanyi jitihada zozote zile za kuzuia watoto kupata ujauzito.
 

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
2,332
1,839
Mkuu ngoja nikuulize swali hili.
Kama binti akimpenda kijana yeye mwenyewe na kumtafuta yule kijana na kufanikiwa kuingia kwenye mahusiano, lakini binti alimdanganya kijana kuhusu umri na pia alimdanganya kuwa yeye SI mwanafunzi, lakini binti akapata ujauzito,
Vipi kuhusu mahakamani uwamuzi wao utakuwaje na Kama mahakamani wakasibitisha kuwa binti alimdanganya kuhusu umri wake,
Kesi Kama hii inakuwaje.
Muwe mnaomba vyeti vya kuzaliwa
 

Joao de Matos

JF-Expert Member
Jun 16, 2022
334
264
Muwe mnaomba vyeti vya kuzaliwa
Usikimbie njoo huku,
Ninavyojua Serikali ya Bongo land hawajafanya juhudi zozote zile za kuzuia mimba mashuleni.
Sasa Kama mnajua kuwa kwa mwaka zaidi ya mabinti 6500 wanapata ujauzito shuleni, je hao wanaume 6500 mnawafunga wote? Jibu na Hilo usikimbie.
Kama kweli mnafuatilia.
 

CHIEF WINGIA

JF-Expert Member
Jul 12, 2013
1,937
3,223
Hapana huu ni ukandamizaji kwa wanaume haiwezekani baba mtoto apingwe nyundo 30 halafu mwanamke abaki mtaani kufurahia maisha
 

Claude Henry

Senior Member
May 25, 2017
189
196
Mimba bila utaratibu ni laana.
Usimsingizie MUNGU mambo ya uongo.
MUNGU aliposema watu wakazaliane hakusema wazaliane hovyo hovyo bila ya kufuata taratibu za ndoa.

Biblia inasema wazi kabisa kuwa mtoto anayezaliwa nje ya ndoa ni "mtoto wa haramu".

Ifike mahala tuwe na heshima kwenye Maandiko ya MUNGU na kamwe tusilete "siasa" kwenye Maandiko ya MUNGU.
Huyo mtoto Haramu haitaji kula, kutunzwa, kwenda shule, kulelewa. Vile vile huyo mtoto Haramu ni kiumbe cha nani kama si cha Mungu. Dunia inasonga mbele, binadamu kwa asili si watakatifu, kila mmoja wetu anafanya makosa mengi yasiyoonekana na wengine- ingawa Mungu anatuona. Tusijidai eti ni wasafi mbele za watu na wengine ni haramu. Mungu pekee ndiye anayehukumu- Acha kutumia vitabu vya Mungu kuthibitisha udhaifu wako- Huna upendo kwa jirani yako (mtoto wa kike aliyepata mimba katika umri mdogo)
 

Son of Gamba

JF-Expert Member
Oct 26, 2012
4,318
5,907
Huyo mtoto Haramu haitaji kula, kutunzwa, kwenda shule, kulelewa. Vile vile huyo mtoto Haramu ni kiumbe cha nani kama si cha Mungu. Dunia inasonga mbele, binadamu kwa asili si watakatifu, kila mmoja wetu anafanya makosa mengi yasiyoonekana na wengine- ingawa Mungu anatuona. Tusijidai eti ni wasafi mbele za watu na wengine ni haramu. Mungu pekee ndiye anayehukumu- Acha kutumia vitabu vya Mungu kuthibitisha udhaifu wako- Huna upendo kwa jirani yako (mtoto wa kike aliyepata mimba katika umri mdogo)
Ni wapi nimesema mtoto akiwa haramu haruhusiwi kula, kuvaa, kusoma na kupata mahitaji yake yote ya msingi??

Ni wapi nimesema mimi ni msafi sana na wengine ni wachafu?

Ni wapi katika hoja yangu nimehukumu mtu?

Tena ni wapi nimesema mtoto haramu au aliyezaa nje ya ndoa achukiwe na jamii?

Hivi unaelewa maana ya neno "haramu"???

Nafikiri hoja yangu ilikuwa kukukumbusha kuwa kuzaa au binti kupata ujauzito ni jambo linaloruhusiwa isipokuwa tu pale utaratibu husika unapofuatwa.

MUNGU aliweka uataratibu wa ndoa ili wanaotaka kuzaa wazae wakiwa ndani ya ndoa.

Kufanya tendo la ngono nje ya ndoa ni uasherati au uzinzi na mtoto anayezaliwa kwa uzinzi au uasherati, mbele za MUNGU mtoto huyo ni "haramu" sababu ametokana na tendo chafu. Uzinzi na uasherati vinahesabiwa mbele za MUNGU kama matendo machafu.

Mtoto anayezaliwa kwa njia hizi chafu, yeye kama yeye hana hatia kwasababu sio kosa lake kuzaliwa haramu. Lakini wanaobeba hatia ni hao waliomzaa.

Ili kuepusha hayo, ndiyo maana jamii iliyostaarabika, yenye kuishi kwa kufuata misingi bora iliyowekwa na MUNGU, imekuwa ikiwasisitiza sana Mabinti na vijana kujiepusha kabisa na vitendo vya uzinzi na uasherati vinavyoweza kuwasababishia kupata ujauzito kabla ya ndoa.

Na Tanzania sababu tunaamini katika MUNGU na ndiyo maana hata katika wimbo wetu wa Taifa tunamtambua MUNGU kwa kumtaja, tukimwomba aibariki nchi yetu na atubariki sisi pia, Je, si vyema tukiwa kama Taifa lenye kumtambua MUNGU tukiishi kwa kufuata kanuni, taratibu, na miongozo ya MUNGU??

Kwanini tusiweke nguvu kubwa kuwazuia watoto wasifanye zinaa, badala yake tunaweka nguvu kubwa kuwagharamia masomo waliopata mimba nje ya utaratibu??

Je, kwa kufanya hivyo huoni kama tunahamasisha zinaa kwa watoto wetu?
Maana kuwasomesha waliopata mimba na kuzaa ni sawa na kutuma ujumbe kwa wengine kuwa hata wao wakizaa nje ya utaratibu hakuna shida.
Like seriously? What kind of a future generation are we raising?
 

Similar Discussions

15 Reactions
Reply
Top Bottom