Kama kweli siwaende Muhimbili na Ocean Road. Waache kudanganya watu.
View attachment 40692
View attachment 40693
Na Haruni Sanchawa
MAAJABU ya uponyaji ndani ya Kanisa la Huduma ya Maombezi lililopo Mbezi Beach chini ya Kiongozi wake, Flora Peter yameendelea kutokeaa baada ya hivi karibuni, Halima Awazi aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa kuombewa na kuanza kuona.
Akizungumza na Amani kanisani hapo hivi karibuni, Halima alisema, haamini kama sasa anaona kwani ni kama ndoto kwa sababu hakufikiria kama siku moja ataondokana na ulemavu wa macho.
"Mimi ni Muislamu lakini baada ya kupata taarifa za mtumishi huyu, niliomba ndugu zangu wanipeleke kwake ili aniombee, sasa ninaona na kutambua hiki ni kitu gani, jambo ambalo sikulitarajia. Kwangu haya ni maajabu ya dunia," alisema Halima.
Naye Faraja Tweve aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Iringa alisema alifikishwa kanisani hapo akiwa hoi huku amebebwa na watu walioamini kuwa atakufa lakini baada ya kuombewa na nabii Flora alipona.
"Nilikuwa nasoma Tumaini (Chuo Kikuu) lakini nilikatisha masomo kutokana na kuugua ugonjwa nisioujua, namshukuru Mungu nimepona na kwa hali niliyonayo, naamini mwakani nitaanza mwaka wangu wa kwanza wa masomo baada ya kuokoka na kifo," alisema Tweve.
Uponyaji wa magojwa yaliyoshindikana unaofanywa na nabii huyo, umepelekea idadi kubwa ya wageni kutoka Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kumiminika kwa wingi kanisani hapo kwa lengo la kupata huduma ya maombezi
Mkuu usi log off hahahahah wewe kazi yako Ku Log off tupe News Bwana Washawashakuna mijinga kibao imejaa ni wewe tu na akili yako ili uweze kuishi kimjinimjini. Nalog off
Kama kweli siwaende Muhimbili na Ocean Road. Waache kudanganya watu.
Yule 'babu' wa loliondo atafunguliwa mashtaka muda si mrefu. Sasa wanazuka wengine wanatumia nguvu za kiza, kisha baadae tunashuhudia vilio. Kibwetere wa kike huyo eeenh? Uongo mtupu. Moto mkali unawangoja siku ya hukumu.Imani yako itakuponya.
Imani yako itakuponya.