Dunia imekwisha ( MAAJABU YA NABII WA KIKE) kuna Manabii mpaka wa kike?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
NABII.jpg

NABIIFLORA2.JPG

Na Haruni Sanchawa
MAAJABU ya uponyaji ndani ya Kanisa la Huduma ya Maombezi lililopo Mbezi Beach chini ya Kiongozi wake, Flora Peter yameendelea kutokeaa baada ya hivi karibuni, Halima Awazi aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa kuombewa na kuanza kuona.

Akizungumza na Amani kanisani hapo hivi karibuni, Halima alisema, haamini kama sasa anaona kwani ni kama ndoto kwa sababu hakufikiria kama siku moja ataondokana na ulemavu wa macho.

“Mimi ni Muislamu lakini baada ya kupata taarifa za mtumishi huyu, niliomba ndugu zangu wanipeleke kwake ili aniombee, sasa ninaona na kutambua hiki ni kitu gani, jambo ambalo sikulitarajia. Kwangu haya ni maajabu ya dunia,” alisema Halima.

Naye Faraja Tweve aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Iringa alisema alifikishwa kanisani hapo akiwa hoi huku amebebwa na watu walioamini kuwa atakufa lakini baada ya kuombewa na nabii Flora alipona.

“Nilikuwa nasoma Tumaini (Chuo Kikuu) lakini nilikatisha masomo kutokana na kuugua ugonjwa nisioujua, namshukuru Mungu nimepona na kwa hali niliyonayo, naamini mwakani nitaanza mwaka wangu wa kwanza wa masomo baada ya kuokoka na kifo,” alisema Tweve.

Uponyaji wa magojwa yaliyoshindikana unaofanywa na nabii huyo, umepelekea idadi kubwa ya wageni kutoka Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kumiminika kwa wingi kanisani hapo kwa lengo la kupata huduma ya maombezi
 
ukisoma Biblia yako kuna kitabu kinaitwa ESTA. Esta alikuwa ni nabii.

Nadhani yupo pia DEBORAH ............

Deborah (Hebrew: &#1491;&#1456;&#1468;&#1489;&#1493;&#1465;&#1512;&#1464;&#1492;, <small>Modern</small> Dvora <small>Tiberian</small> D&#601;&#7687;ôr&#257; ; "Bee", Arabic: &#1583;&#1740;&#1576;&#1575; Diba&#8206;) was a prophetess of Yahweh the God of the Israelites, the fourth Judge of pre-monarchic Israel, counselor, warrior, and the wife of Lapidoth according to the Book of Judges chapters 4 and 5.
 
poleni sana msiojua mandika maana yalitabiri siku za mwisho watatokaea manabii wa uongo
 
Siku ya mwisho watu watamfuata na kumwambia, BWANA mimi nilitenda haya kwa jina lako. Naye atawajibu, ondokeni hapa, siwafahamu nyinyi. Kitu kimoja ambacho kitawapeleka watu wengi motoni ni Uponyaji na ahadi za kupata utajiri/ mafanikio kupitia maombi..shetani anakamata wengi kupitia umaskn na shda zao, na kukosa kwao maarifa ya kuwapima hao wanaojiita manabii kwa matendo yao na mafundisho yao...
 
Back
Top Bottom