Samwemgomba
Member
- Mar 25, 2019
- 35
- 15
Ndugu wana jamvi, amani ya bwana iwe nanyi wote.
Naam dunia imeenda kasi sana, maendeleo ya sayansi na teknolojia ni makubwa sana katika kipindi hichi kuliko wakati wowote mwingine katika historia ya uwepo wetu sisi binaadamu hapa duniani.
Wakati mataifa ya dunia ya kwanza (MAREKANI, CHINA, JAPAN URUSI etc) yakiwa katika ushindani mkubwa wa uvumbuzi mpya wa masuala ya kisayansi na maendeleo ya kiteknolojia huku upande wa pili kwetu "AFRICA" bado tunauchapa usingizi mzito wa PONO.
Ni ukweli kuwa Wamarekani kupitia taasisi yake ya uchunguzi wa ANGA (NASA) wamefika hatua ya kuanzisha makazi katika sayari nyingine Zaidi ya sayari ya dunia tunayoishi kwa sasa! Lakini jambo la kushangaza kabisa Afrika na hususan Tanzania yetu sisi bado tunaendele kukumbatia "MILA" za kipumbavu kabisa ambazo "AT THIS LEVEL" tunaendelea kuendekeza mila za ukeketaji, ulonzi na uchawi usio na faida yeyote una upumbavu mwingine mwingi tu.
Nayazungumza haya kupitia mijadala mbali iliyowasilishwa na wadau wanaofanya kazi katika kupinga aina zote za Unyanyasaji wa Kijinsia(GBV). Mmoja wa wana warsha alieleza kisa kimoja cha kusikitisha ambapo katika moja za wilaya kusini mwa Tanzania zinazopakana na Zambia kilitokea KISA ambacho Yupo binti mmoja alimanusula azikwe hai na mama yake kwa sababu tu kuwa binti huyo ambaye mwaka 2017 alizaliwa kwa njia ya operation na kusababisha kifo cha mama yake mzazi ambae kabla ya kifo cha mama yake mzazi alikuwa na ndugu zake (Dada na kaka) saba ambao walizaliwa kwa njia ya kawaida kabla yake yeye ambae alizaliwa kwa njia ya Operation.
Sasa ndipo kikao cha familia na wana ukoo wa mume wa marehemu walipoazimia binti huyo mwenye siku moja ni balaa na mkosi kwenye ukoo kwa hiyo ni lazima akazikwe na mama yake akiwa hai ili kuepusha mkosi huo.
Baada ya shughuli za maandalizi ya msiba yalipokamilika ndipo binti huyo ambae kwa kipindi hicho alikuwa na siku 1 ikaamuliwa utobolewe mlango au dirisha nyuma ya nyumba ili atolewe huku na asitolewe katika mlango wa kawaida akazikwe akiwa hai.
Mmoja ya watu waliohudhuria mazishi malaika wa Imani akamshukia, alipiga yowe kubwa la uchungu na kulia kwa sauti kubwa sana wakati binti huyo alipokuwa anaviringishwa nguo (vitambaa) ili atumbukizwe kaburini yeye na mama yake!
Akaomba ummati wote na wanafamilia kwa ujumla wampe mtoto huyo akamlee yeye kuliko kumzika na shukrani za pekee na kwa ajabu ya aina yake mama huyo mzalendo akakubaliwa ombi lake la kupewa mtoto huyo ambapo mpaka leo anamlea ila ilibidi ahame Kijiji kwa ajili ya usalama wa mtoto huyo. Kisa ni krefu ila naomba nikiwakilishe kwa ufupi.
Pia yapo matendo mengine mengi ya ajabu sana na MILA za kipumbavu ambazo mpaka sasa bado tunaziendeleza kama Ukeketaji ambapo mmoja ya Mdau alitoa ushuhuda wa mama mmoja ambae anasema yeye kafanyiwa ukeketaji kwa Zaidi ya mara 4 kwenye UKE hivyo basi anasema lile umbile la asili alilozaliwa nalo kama mwanamke halipo katika uhalisia wake kwa Zaidi ya asilia 80%.
Kuna ishu nyingine pia za ajabu sana ambazo si ngeni kwenu wana jamvi ila habari za "TELEZA" huko Kigoma lakini kingine cha ajabu nilichokisikia kwa mara ya kwanza ni tiba za asili zinazotolewa kwa watoto wadogo wenye ugonjwa wa "LAWALAWA" ambapo mtu mzima anamuingizia mtoto mdogo KIDOLE matakaoni na kukizunguusha na kutumia kucha zake kukwangua kuta za (ANUS) Mpaka patoe damu nyingi wakiamini ndio tiba ya ugonjwa huo pamoja na minyoo.
Haya ni baadhi ya mambo machache kati ya mengi yaliyonisukuma ni share na nyinyi wadau kuhusu UAFRIKA na mila za kipumbavu dhidi ya maendeleo makubwa walionayo wenzetu huko kunakoitwa Dunia ya kwanza! achilia mbali ishu za mimba kwa watoto wa shule ubakaji, ndoa za utotoni, ubakaji na ulawiti kwa watoto wadogo! Inafika kipindi Waafrika tubadilike sana tunatia aibu sana kwa kuwa "AT THIS LEVEL OF ADVANCED TECHNOLOY AND SCIENCE" Bado tunafanya vitu as if bado tupo kwenye "OLD STONE AGE"! Sometimes naona ya maneno ya kejeli matusi ya mwanahistoria maarufu aitwae HEGEL dhidi ya waafrika alistahili sana kwetu. Kauli mbiu hebu sasa tuanze kufanyia kazi haya mambo katika family level na hata ngazi ya UKOO! Tupeane elimu!