Dunia imeamua kujitoa ufahamu: Inadai Yerusalemu siyo mji mkuu wa Israel

Kwanza si alishaambiwa limejengwa Jerusalem jipya la "kiroho" hili la kimwili ni la kazi gani? Kuna watu wanatumikishwa sana, hakuna lolote hija ni utalii tu na nchi zinaingiza mapato ktk hija. Mkristu kujifungamanisha na Israel, ambao walio wengi bado wanapingana na Ukristu na kumkana huyo Yesu, ni kujitoa ufahamu.

Jerusalem hata kabla ya kujengwa haikuwa ya wayahudi, kwa hadithi ile ya nchi ya ahadi walivyoipata, waliwakuta wenyeji, lakini pia walishahama kwa mamia ya miaka, hivi bado tu wawe na umiliki wa maeneo tu?

Tunafundishwa, kwamba wabantu kwa asili ni wenye asili ya misitu ya Kongo, je wazaramo wana Haki leo kurudi na kujikatia eneo kwa Kongo eti babu zao waliishi hapo?

Hili swala linawasumbua watu Sana, wanaolishikilia kwa manufaa yao ya kisiasa na kiuchumi wanasingizia dini kupata mashiko na huruma kwa wengine.
Israel yupo sababu ananguvu ni sawa na Ni waarabu asili yao ni Saudia Huko Arabian peninsula hawana haki kudai Jerusalem so ni upumbavu kuikatalia Israel mji wake mkuu
 
Wakati nabii Ibrahim akijenga msikiti wa maka na mwanae nabii Ismail nabii Ishaka alijenga masjid Aqsaa nabii Ishaka alikuwa mtoto wa Sara mke wa nabii Ibrahimu
Ibrahim siyo mwehu ajenge majengo na mtoto wa mchepuko wkt ahadi kibao zipo kwa mtoto wa ndoa. Kumbuka aliwatimu, na hakuna mahali aliwarejesha nyumbani.

Mchepuko siyo dili mkuu
 
Tofautisha kuondoka mahali kwa hiari na kuondolewa mahali kwa nguvu. Ukiondoka kwa hiari huhitaji kurudi, ukiondolewa kwa nguvu unahitaji kurudi! Wayahudi waliondolewa kwa nguvu na walivyorudi? wakaamua kutumia nguvu kurejesha ardhi na miji yao!
Umesoma historia?
Waliondolewa kwa nguvu na nani?
Hata wangoni waliondoka Afrika ya kusini kwasababu ya vita ya Shaka Zulu alipokuwa anapanua utawala wake.
Je wanaweza kurudi leo wakadai eneo walilokuwa wakiishi?
 
aya si unazijua..tafuta uone kama uongo ni jihad au laa
taqiyya-kitman.jpg
 
Hapo umesema vizuri na umekiri kuwa waisrael ndio wamiliki wa mwanzo wa mji wa Yerusalemu. Tatizo ni kwamba walitekwa na kusambazwa duniani kote! Wangoni kama wakirudi afrika ya kusini Leo na wakakumbuka mahali walipokuwa wanaishi na wakawa na nguvu, wana haki ya kuwatoa waliokalia maeneo yao! Tatizo tu ubavu huo hawana na wameridhika kuwa Tanzania!
Hivi umesoma historia kweli?
Unajua kabla ya hao mnaowaita Waisrael kurudi pale kuwa kulikuwa na sehemu nne tofauti ambazo zilifikiriwa ikiwemo Kenya ya leo?
Basi leo hii wahindi wekundu wadai America yao maana ndio wenye nchi hiyo
 
Ibrahim siyo mwehu ajenge majengo na mtoto wa mchepuko wkt ahadi kibao zipo kwa mtoto wa ndoa. Kumbuka aliwatimu, na hakuna mahali aliwarejesha nyumbani.

Mchepuko siyo dili mkuu
hata isaka alitimuliwa na ibrahim .......halafu uzao wa isaka ndio ulioteseka sana kwa nini?
 
Tena hawa wa akina Trump ndo kwanza wameamia miaka ya hivi Karibuni hata kuliko waarabu wa Kipalestina, ambao Israel ni yao kwa miaka nenda rudi.

Kuna kitu kinawasumbua watu hapa, Israel na Palestine yote ni mataifa, na yote yana makundi tofauti tofauti ya watu, kwa race tofauti kote, dini tofauti kote. Kuna waarabu Israel na vivyohivyo kawa Palestinians, kuna wayahudi Palestine na pia Israel, kuna waislam Israel kama walivyo Palestinians, pia kuna Ukristu Israel kama walivyo pia Palestine. Idadi yao kiasilimia hauuondoi Ukweli wake.
Kuna tofauti ya miaka nenda rudi na miaka yote. Israel siku zote ni nyumbani kwa wayahudi na mji wao mkubwa siku zote umekuwa ni Jerusalem. Miji mingine ni Galilaya, Yerico, etc. Iko hivyo siku zote
 
hii kitu inanipaga raha sana nikiiona tu nashuka moja kwa moja kwenye comments....waafrika sie sijui jerusalemu yetu ni ipi..manake mapovu hapa yanawatoka watu balaa..wayahudi hawawatambui wala kuwathimini waafrika kivile (read: wao dini yao ni judaism sio ukristo)..waarabu hawaathamini wabantu kivile (read: uislam sio ishu..ukabila/race ndo mambo yote)..tuendelee tu kutoka povu kwa ajili ya watu wa mashariki ya kati ilihali wao hawapotezi hata chembe ya usingizi kwa miafrika....shikamooni watu weupe (waarabu na wayahudi kwa tafsiri yangu hapa)....
Mkuu suala siyo dini, suala ni utamaduni wa mtu na historia yake lzm vilindwe na viheshimiwe. Nawashangaa mnaojadili kwa kuegemea dini zenu, mnapotea
 
Hapo sasa Mkuu unakuta bendera ya Israel kwenye nyumba ya ibada wakati wao hawautambui Ukristo just only 2% ndo Wakristo.
Si unaona wanataka rudisha Waafrika Afrika hawawataki kule
Suala siyo ukristo, uislam au uyahudi. Suala ni mila na desturi, historia na utamaduni wao. Lazima ulindwe. Utaishije utumwani wakati una kwenu?
 
Wakati nabii Ibrahim akijenga msikiti wa maka na mwanae nabii Ismail nabii Ishaka alijenga masjid Aqsaa nabii Ishaka alikuwa mtoto wa Sara mke wa nabii Ibrahimu
Hivi unamchukulia Abram fala kiasi hicho? Hawezi fanya ujinga huo
 
Waisrael wenyewe just 2% ndiyo wakristo hata waislam ni wengi kuliko wakristo wako 17%.
Nashangaa kwanini wewe unayeamini kuwa ni taifa teule usifuate wanachokiamini wao maaana 75% ni Judaism
Hatufuati wanachoamini wayahudi wala ila tunakubaliana nao kwa mambo ambayo wako sahihi kama vile Yerusalemu kuwa ni mji wao tangu mababu na mababu! Waarabu ni uzao wa Ishmael ambaye ni mtoto wa haram maana alizaliwa na mjakazi nje ya ndoa! Mtoto wa jinsi hiyo hana haki ya kurithi chochote! Tatizo liko pale! Waisrael ambao ni uzao wa Yakobo mwana wa Isaka ndio wenye haki ya kurithi. Sasa wana halali Israel walipokuwa utumwani, mtoto wa mjakazi na uzao wake (waarabu) wakajichukulia maeneo na miji! Mwenye eneo na miji yake aliporudi mwaka 1948 alilazimika kutumia nguvu/vita kuurejesha nusu ya mji wa Jerusalem yaani Yerusalemu magharibi. Lakini mji hasa wa Daudi (mji wa kale) ni Yerusalemu mashariki na hiyo ikabaki mikononi mwa waarabu hadi mwaka 1967 Israel walipofanikiwa kuirudisha Jerusalem mashariki kwenye himaya yao kwenye vita ile ya siku 7! Waarabu hawaamini mpaka Leo kilichotokea! Kipigo kile kilikuwa kipigo kitakatifu!
 
Back
Top Bottom