Dunia iko kasi, zamani mnachati kwa meseji na mpenzi wako usiku kucha unasikia hisia mpaka rohoni

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,693
36,081
Daaaahhh kuna vitu ukivikumbuka unaweza kulia. Dunia iko kasi sana.

Enzi zetu mnachati na mpenzi wako kwa sms mpaka unahisi Mungu dunia aliiumba kwaajili yenu tu.

Sasa hivi mkichati kidogo tu mnaombana vikojoleo, mkitumiana chatting inakata kwa siku hiyo mnasubiri siku nyingine.

Mkichati siku 3-5 tu tayari mmoja anaanza kuwa busy.

Ule upendo wa kumpenda mtu mpaka unasahau kula umeshapotea ulimwenguni. Sijui miaka 10 mbele hali itakuwa vipi.
IMG_20210531_200444_819.jpg
 
Pesa imetawala mapenzi kwa sasa wanawake wanapenda pesa kuliko unavowaza. No true love without money
 
Wanawake wa siku hizi kazi kuomba hela tuu, hizo hisia zinatoka wapi na wakati unajua dakika 10 zijazo unapigwa mzinga
 
Ukiacha kuwa ulikua mwanafunzi enzi hzo kuna shuhuli nyengne ulikua unafanya?

Kadri unavyokuwa mkubwa majukumu nayo yanaongezeka na unaanzan kuweka priorities zako sawa

Huwez kuwa unachat whole night then asbh saa 12 uamke kwenda kazini ni lazma itakuchosha, huwez kuchat whole day na bado uko kazini so majukumu yanapunguza baadhi ya vitu
 
Kama nakufeel tutachart au kuongea had nisinzie maana maneno hayaishi. ukiona kila siku ubize jua hujaingia kwenye aorta vena cava ya mtu
 
Siku hizi hata akikuvulia nguo zote, hisia za kusaka kwa manati. Ukiwaza alishakutumia sms zaidi ya 60 za "TUMA NA YA KUTOLEA" na miscall 300 kabla hamjaonana nae.
 
Back
Top Bottom