Dunia ikijadili athari za Corona na Uchumi, Sisi ni kuvunja Katiba na kuongeza muda

Mkongwe Mzoefu

JF-Expert Member
Aug 10, 2018
842
2,467
Dunia ikiwa inatumia mabunge yake kufikiri na kujadili janga hili la gonjwa la Corona, athari zake kiuchumi na tafiti za matibabu yake, hapa kwetu Bunge hili la kuchonga kama kinyago limejikita kujadili kumuongezea Magufuli muda kinyume na katiba.

Kazi za wabunge ni kupeleka sauti ya wananchi bungeni kwa niaba yao, je hawa wabunge wametumwa hilo na wananchi?

Kuna kila dalili kuwa bunge la 12 ni anguko la kishindo la taifa hili.
 
Screenshot_20210204-025238.png
 
Ni aibu sana kujulikana ni mtanzania huku nje. Miaka ya nyuma ukisema Tanzania unasiki habari za bonde la ngorongoro, serengeti, kilimanjaro, zanzibar na kuwa hatuna vita wala njaa. Sasa unasikia kuua albino, kuikana covid na sasa kukataa chanjo. Sasa tunahoji hata nia za wahisani eti kwa sababu hawajagundua chanjo ya malaria na cancer (hii sio kitu hata ya chanjo), lakini hapo hapo hatuna uwezo wa kununua chanjo za surua, polio, pepopunda, dondakoo na hata ARVs. Zote hizo zinalipiwa na wahisani!!! Tumeamua kuwa masikini jeuri!!

Tunakataa chanjo na huku tukijua kabisa kuwa imeharibu uchumi wa dunia na nchi yetu. Hata tu kujikinga na maambukizi tunaogopa kutamka hadharani!!

Tumekosa maarifa, na siku za kuangamia zatujia usoni.
 
Back
Top Bottom