DUNIA Ijiandae kushuhudia Mabomu ya Nuclear yakitumika huko Ukraine na Urusi

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
9,564
15,919
Wadau wa siasa za kimataifa natumaini hamjambo.

Ule wakati wa kushuhudia matumizi ya mabomu hatari zaidi sanaa hapa duniani umefika. Nakumbuka kutupwa kwa bomu hili kule Nchini Japan katika miji ya Hiroshima na Nagasaki na marekani ndio ilikua mwanzo wa mwisho wa Vita vikuu vya pili vya Dunia.

Sasa tukae mkao wa kula historia imejirudia mshindi wa Vita hivi ataamuliwa na mabomu makali ya Nuclear.

USHAURI:
Kama una ndugu yako au mtoto au yeyote anaishi ulaya mashariki au anafanya kazi huko mwambie aondoke haraka sana wakati ujao utakua mgumu sana. Athari za mionzi ya Nuclear ni mbaya sana Ulaya yote pamoja na urusi kutakua na shida kubwa. Chukueni tahadhari kabla ya hatari.
 
Mtumiaji wa hyo nuclear weapons ni nan sasa?
emoji635.png
au
emoji1255.png
Endapo hilo litatokea (Kitu ambacho sidhani), Huo ndio utakuwa ni mwanzo wa Afika kupokea wakimbizi wa Kizungu, Wahamiaji haramu wa Kizungu na zaidi ya yote Uhamishwaji wa lazima wa Teknolojia kutoka bara Ulaya kuja Afrika. Ni FURSA.
 
Urusi hawezi kuji expose kijinga kiasi hicho kwa kuangamiza watu watu wake kwani anajua fika kwamba mabomu hayo pia yatatua kwenye ardhi yake na kuleta maafa.

Pia ukae ukijua kwamba mabeberu yameshafanya analysis ya kutosha na kujua kwamba anga la urusi linaingilika kirahisi watu wanaingia na kutoka kama choo Cha stand so uwezekano wa nuclear kutus klemlin na Moscow ni mkubwa.

So Putin akae kwa kutulia na ajue kwamba vita ndio Kwanza inaanza.
 
Sawa nimetoa tahadhari kulingana na ninavoona mwelekeo . Nuclear ndio itamaliza huu mgogoro kama bado tupo hapa utashuhudia ninachosema.
 
Urusi hawezi kuji expose kijinga kiasi hicho kwa kuangamiza watu watu wake kwani anajua fika kwamba mabomu hayo pia yatatua kwenye ardhi yake na kuleta maafa...
Vita ikishafikia point fulani haiangalii tena watu. Ni wazi kwa sasa mpango wa na NATO nikuongeza silaha nzito zaidi kuisaidia Ukraine kitu ambacho urusi hataki/ hakunali unadhani kifuatacho ni nini? Angalia mbele zaidi mzee
 
Wadau wa siasa za kimataifa natumaini hamjambo.
Ule wakati wa kushuhudia matumizi ya mabomu hatari zaidi sanaa hapa duniani umefika. Nakumbuka kutupwa kwa bomu hili kule Nchini Japan katika miji ya Hiroshima na Nagasaki na marekani ndio ilikua mwanzo wa mwisho wa Vita vikuu vya pili vya Dunia...
Ni kweli unachoongea mdau kwa hali iliyofikia huenda putini anataka kutumia nuclear weapons muda wowote sasa tunasubiri itakuaje ila endapo atatumia atajutia maamuzi yake kwa reaction itakayotokea dhidi ya nato
 
Wadau wa siasa za kimataifa natumaini hamjambo.
Ule wakati wa kushuhudia matumizi ya mabomu hatari zaidi sanaa hapa duniani umefika. Nakumbuka kutupwa kwa bomu hili kule Nchini Japan katika miji ya Hiroshima na Nagasaki na marekani ndio ilikua mwanzo wa mwisho wa Vita vikuu vya pili vya Dunia....
Hivi wadau putin anawaza nn kuhusu nuclear weapons,hivi sayari hii iangamie kabla ya muda wake mungu alioupanga kweli ,aisee huyu dikteta putini atapotezwa kama hitler alivyopotea
 
Urusi hawezi kuji expose kijinga kiasi hicho kwa kuangamiza watu watu wake kwani anajua fika kwamba mabomu hayo pia yatatua kwenye ardhi yake na kuleta maafa.

Pia ukae ukijua kwamba mabeberu yameshafanya analysis ya kutosha na kujua kwamba anga la urusi linaingilika kirahisi watu wanaingia na kutoka kama choo Cha stand so uwezekano wa nuclear kutus klemlin na Moscow ni mkubwa.

So Putin akae kwa kutulia na ajue kwamba vita ndio Kwanza inaanza.
Ingekuwa anga la Urusi haliingiliki wala UK asingejitapa kuwa yupo tayar kupeleka Nuclear Poland endapo Russia akaendelea kutishia Nuclear.

Toka Russia aanze vitisho vya Nuclear, tayari Ulaya ishajipa muda wa kukabiliana nayo.
 
Hayo mabom ni ya kazi gani Kama hayatumiki? Wao wapigane nayo huko ulaya yote iwe Kama Libya,Mogadishu,au Kama ilivyo Ukraine now,wawe masikini mafukara.kipindi hicho Africa tutakuwa supa power wao tutawaamulia na kuwawekea vikwazo😁😁😁😁
 
Endapo hilo litatokea (Kitu ambacho sidhani), Huo ndio utakuwa ni mwanzo wa Afika kupokea wakimbizi wa Kizungu, Wahamiaji haramu wa Kizungu na zaidi ya yote Uhamishwaji wa lazima wa Teknolojia kutoka bara Ulaya kuja Afrika. Ni FURSA.
ww utaponaje??
 
Ni kweli unachoongea mdau kwa hali iliyofikia huenda putini anataka kutumia nuclear weapons muda wowote sasa tunasubiri itakuaje ila endapo atatumia atajutia maamuzi yake kwa reaction itakayotokea dhidi ya nato
Nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa hakuna silaha za maangamizi kuelekea Moscow ktk ardhi ya Ukraine. UK alishasema atapeleka Nuclear Poland, kitendo cha Russia kupiga bomu Ukraine. Ni kitendo cha dakika kadhaa tu Moscow inategeuzwa kuwa vumbi, muda wa wao kujipanga na wajue wapige nani sidhani kama wanaweza wakafanya kwa usahihi.

Putin anajua fika uwezo wa NATO kijeshi, ndio maana hataki Ukraine ijiunge na NATO. Na hivi vita mwanzoni kabisa tuliona Ukraine akipambana mno mwenyewe ila kwa sasa anapewa sana msaada, hii ni sababu mwanzo WESTERNS walikuwa wanasoma uwezo wa Russia kijeshi. Na mpaka sasa wanakubali kumsaidia Ukraine kwa kumpa silaha nzito, inamaanisha wameshamsoma.

Kupitia hii Vita tumeona vile mifumo ya russia ya ulinzi ilivyo weak, Putin hawezi kuthubutu kufanya huu uchafu wa kutjmia Nuclear.
 
Back
Top Bottom