Dunia hutoa ishara zake ambazo Mungu anataka tutambue kisha tuzikabili (Mkasa wa SARS Cov2)

JAY MTAALAM

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
1,594
1,384
Mungu atukuzwe..

Ndugu wana jamii forums pia na wale watembeleao mtandao huu na Serikali yetu pia. Napenda kutumia jukwaa hili kugusia kiasi fulani kuhusu maisha na mazingira tunayoishi.
Dunia ni nyumba ya wanadamu na mjenzi wake hupenda kutoa changamoto ili kila mmoja amkumbuke!.

Covid 19 analeta hatari katika afya ya mwanadamu..kwa muda mrefu walimwengu wameunda mfumo wa matabaka kisa mali na madaraka.

Kuna baadhi ya watu walishawahi kutoa maoni/mipango jinsi ya kuunda maisha yampendezayo Mungu lakini watu wengi bado ni wabishi sana.

Wakati huu ni muda wa kutafakari huu tunaouita uchumi je ni uchumi sahihi? Waweza kutuokoa sisi au Dunia? Pengine maisha halisi tunayostahili kuishi tumeyakosea.

Viongozi wengi wanatoa matamko ya Kifalme kama zamani..wanasema uchumi utayumba badala ya kutumia kila kilichopo kuokoa uhai.

Pengine wakati huu ndio viongozi wanapaswa kumkumbuka Mungu na kusisitiza watu kumuomba Mungu atupe maarifa ya kukabili huu ugonjwa. Chanzo chake ni nini haswa kiasi athari kwa binadamu imekuwa hivi kuliko viumbe vingine..

Covid haina huyu tajiri au masikini, inahitaji tu watu wajitambue kuwa maisha tunayoishi sio halisi kama inavyotakiwa si vyema kusongamana, kula kila mnyama, kujilimbikizia mali, kutishana, kujitapa n.k

Hadi sasa na juhudi zote bado sijaona nchi zinazokiri imani kubadili maisha zaidi ya kutafuta dawa na kuendelea na mambo yale yale!

Huu ni wakati wa kutafakari sana. Maoni ya watu wengi bado hayajumuishi kupeana mbinu za kuutokomeza huu ugonjwa bali kukosoa au kudanganya takwimu.

Si China, Marekani wala Rusia wote hawajawa pamoja kushirikiana kama Mungu anavyotaka,wote wapo wanalinda uchumi na kutafuta mbinu ya kufaulu zaidi ya mwingine katika ugonjwa badala ya kuifikiria Dunia japo ipatikane dawa ya kupuliza Dunia nzima..
Makombora ya kuangamiza maelfu wanayo...Tafakari

NB: Soma huku ukizingatia kanuni za kujikinga na Covid 19.

Fanya Ibada Mungu akusaidie..
 
Corona ni kali kweli lakini sio mwisho wa dunia..
Kwahio mutation ya virus msianze kuifanya kama Mungu ndio katoa adhabu..
Kuna majanga makubwa yaliipiga dunia kwenye historia na bado dunia inaendelea.
 
Corona ni kali kweli lakini sio mwisho wa dunia..
Kwahio mutation ya virus msianze kuifanya kama Mungu ndio katoa adhabu..
Kuna majanga makubwa yaliipiga dunia kwenye historia na bado dunia inaendelea.
Corona ni funzo..hapana sehemu nimependekeza ni mwisho wa dunia kama wengine wazaniavyo..

Soma tena utafakari yawezekana unahisi wewe hutopata Corona kiasi hutaki ata kumkumbuka Mungu.

NB: Hoja hii si ya Mungu yupo au hayupo!
 
Russia hawana Mungu
China hawana Mungu

Imani ulionayo usidhani ndio kila mtu anayo.
Corona ni funzo la kutafakari..
Si kweli China na Rusia hawana Mungu bali wamepotoshwa..Ila kuna wanaoamini uwepo wake.
 
Unaweza kuleta ushahidi wamepotoshwa na nani?
Wewe wasema..amini Corona itapokulaza ndipo utafahamu
kutokusadiki kwa baadhi ya watu..si kila kitu tunalazimika kuweka ushahidi ni swala la kutafuta mwenyewe ushahidi.
NB: Hoja hii itakufaa kama unasoma Maandiko ya Dini,Siasa za ulimwengu pia kuichunguza tabia yako binafsi kama inaendana na roho yako kabla ya tamaa kuanza kukutawala au madaraka yako au ulipoundiwa madaraja ya uchumi..
 
Back
Top Bottom