Dunia hii inagawanywa katika makundi mawili

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
1639008178761.png

Dunia hii inagawanywa katika makundi mawili, na jina la “utawala wa kiimla” zinatwikwa nchi zinazothubutu kusema “lahasha”.

Kwa mujibu wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa uliosainiwa mwaka 1945, kuwa na mfumo fulani wa utawala ni suala la mamlaka ya kila nchi, ambalo linaamuliwa na watu wake. Inajulikana kuwa Jumatano na Alhamisi wiki hii, kuna nchi inaandaa ati“mkutano wa kilele wa ××” katika mji mkuu wake, lakini karibu nusu ya nchi za dunia hazijaalikwa kwa kisingizio kuwa nchi hizo hazijafikia kigezo chake

Kitendo kama hicho si kigeni kwetu. Kauli ya “ama uko pamoja nasi, ama uko dhidi yetu” bado inakumbukwa vizuri, na ilitolewa mwaka 2001 dhidi ya nchi yoyote iliyothubutu kusema “hapana”. Lakini dunia ya sasa imebadilika, na kuendelea kufuata hiyo kunaweza kuishia kugonga mwamba.

Katika miongo kadhaa iliyopita unafiki wao umefichuliwa, na nchi nyingi barani Afrika, Asia na Mashariki ya Kati zimeharibiwa kabisa kwa visingizio vya ajenda kuu zinazojadiliwa kwenye mkutano huo. Lengo pekee walilonalo ni kutaka kuziambia nchi hizo kuwa kama zikitaka kuishi kwenye mazingira yasiyo na vikwazo na vita, kwanza ni lazima zifuate kanuni wanazoweka.

Inawezekana kuwa kuna nchi ambazo hazielewi mifumo na sera za nchi nyingine, lakini zinaweza kuheshimu mafanikio yao na pia kutaka kupata maendeleo makubwa kama yao.

Ikumbukwe kuwa chochote inachofanya serikali ni kuwahudumia wananchi wake, ili wawe na furaha, waridhike na waishi maisha bora. Si kila nchi inatakiwa kufuata mfumo wa aina moja wa kimagharibi. Vilevile ikumbukwe kuwa kuna mifumo mbalimbali kutokana na hali tofauti, ambako nchi zinapaswa kufunzana na kuungana mikono, ili dunia iwe na rangi mbalimbali.
 
View attachment 2037742

Kinachogawanya jamii ni the have and don't have. Yani mfano the have ni kama mimi and don't have ni kina Idugunde the witch na Wakudadavuwa
 
Back
Top Bottom