Duni: Kuandikisha Wapiga Kura Idd ni Kuvunja Katiba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Duni: Kuandikisha Wapiga Kura Idd ni Kuvunja Katiba!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Sep 22, 2009.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Sep 22, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Salim Said

  CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema kitendo cha Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kuendelea kuwalazimisha Wazanzibari kwenda vituoni ili kuandikishwa hadi katika sikukuu za kitaifa, ni kuvunja katiba na sheria ya nchi na kwamba kutokana na hali hiyo, uchaguzi utakuwa batili.

  CUF imelezimika kutoa kauli hiyo baada ya ZEC kuamua jana kufungua vituo vya kuboresha daftari la kudumu la wapigakura katika visiwa vya Unguja na Pemba hapo huku ikijua kwamba juzi na jana ilikuwa ni sikukuu ya kitaifa ya dini ya kiislaam.

  Akizungumza na Mwananchi jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Juma Duni Haji alisema kitendo cha ZEC kufungua vituo hadi siku za sikukuu za dini, ni ishara ya kutapatapa

  Duni ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha wa chama hicho, alisema kitendo hicho cha kuwataka wananchi kwenda vituoni kujiandikisha siku ya Idd ni dhambi hata kwa mwenyezi Mungu.

  Alisema katiba ya nchi inatoa uhuru wa kuabudu na kwamba sheria ya maadhimisho nchini inatoa uhuru wa kusheherekea sikukuu za kidini ambazo pia ni sehemu ya ibada.

  "Kwa kweli kuwafanyisha watu kazi sikukuu si haki na dhambi hata kwa Mwenyezi Mungu. Lakini ZEC wanafanya hivyo makusudi na ni ishara ya kutapatapa kwao ili kutimiza malengo yao waliyojiwekea.

  "Hata kikatiba na kisheria tayari umeshaingilia uhuru wa kuabudu wa watanzania jambo ambalo halikubaliki," alisema Duni.

  Duni alisema kitendo hicho si halali na wala si haki kwa sababu asilimia kubwa ya Wazanzibari ni waislaam na wanahitaji muda huo wa mapumziko ili kutembeleana na kupumzika na familia zao.
  katika kutimiza malengo yao.

  "Kidini si halali na kikatiba kwani imevunjwa na sheria imekiukwa na hivyo utaratibu huo si halali kwa wananchi na wananchi wamenyimwa haki ya kuabudu," alisema Duni.

  Hivi karibuni Katibu Mkuu wa CUF maalim Seif Sharif Hamad aliandikia barua ZEC akiitaka kusogeza mbele daftari hilo hadi hapo mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na sikukuu zake.

  Duni alisema Katiba ya Zanzibar imevunjwa na sheria ya uchaguzi ya Zanzibar ni batili na kwamba hata uchaguzi utakaofanyika visiwani 2010 utakuwa batili!

  "Katiba imevunjwa na sheria ya uchaguzi ni batili na kwa mantiki hiyo hata uchaguzi wowote utakaofanyika kwa kutumia sheria hiyo utakuwa batili tu,"alidai Duni.

  Aliitaka ZEC kusitisha mara moja uandaaji wa daftari hilo na kuitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kuhakikisha kwamba, inatoa vitambulisho vya Mzanzibari Mkazi (Zan ID) kwa wazanzibari wote wenye sifa.

  Mkurugenzi wa Zec Salum Kassim akizungumzia tume yake kuamua kufungua vituo vya kuandikisha wakati wa sikukuu za Idd el Fitri, alisema vituo hivyo vimefunguliwa licha ya juzi kuwa ni sikukuu ya Idd El Fitir. "Vituo viko wazi hivi sasa, lakini mimi siwezi kukujibu lolote kwa sababu leo ni siku ya mapumziko ya kitaifa, nipigie kesho nitakueleza," alisema Kassim.


  Source: http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=14778

  My take:
  1. Hivi Duni na Maalim Seif ni viongozi wa kidini na siasa at the same time?
  2. Na hao wananchi walilazimishwaje kwenda kwenye vituo vya kujiandikisha?
  3. Kama wananchi wangekaa nyumbani au kuwatembelea marafiki kuna mtu angekuja kuwatoa nyumbani kwenda kujiandikisha?
  4. Mbona chaguzi mbalimbali zimewahi kufanyika Jumapili au Jumamosi ambazo ni siku za mapumziko na hawajawahi kutoa tamko la kuvunjwa kwa Katiba au sheria nyingine yoyote? Au kwa sababu wao sio Wakristo?
  5. Mbona kama vile wanachukua pre-emptive action inayolenga uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kama anavyofanyaga Lipumba kuwahi kutangaza matokeo kabla ya Tume ya Uchanguzi kutangaza ili kutafuta public sympathy?
   
  Last edited: Sep 22, 2009
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana nae Bwana Duni. Kwani kuandikisha au hata kuendelea na kazi yoyote ile siku za Ijumaapili au siku za Sikukuu ni kuvunja katiba ya Tanzania.

  Kwani katiba imezitambua siku za mapumziko kuwa na ijumaaMosi na ijumaaPili na siku za Sikukuu zinazotambulika Kiserikali.

  Tume kuweni makini kwani mambo madogo kama hayo yanaweza liingiza Taifa katika hasara kubwa pindi pale mahakama itakapo batilisha uchaguzi na kusema kuna kanuni zilikiukwa akti wa uandikishaji
   
 3. j

  jagirango New Member

  #3
  Sep 22, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo siyo kuandikisha siku ya sikuku tatizo ni maudhui ya kufanya kitendo hicho siku ya sikukuu ndio kinaweza kuhalalisha uhalali wa tukio lenyewe,Je,ni wananchi wanaolalamika kuwa wanalazimishwa kujiandisha siku ya sikuku au viongozi wanaofanya maoni kuwa hoja za wananchi?, Umuhimu wa kujiandikisha na sherehe ukoje katika kutimiza uhai wa mbeleni wa wakazi wanaotamani kuishi maisha ya utu na haki kwa kutamaliki kwa demokrasia.
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Sep 22, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kuna mtu alilazimishwa kwenda kujiandikisha? Si wale ambao sikukuu haiwahusu wangeenda kujiandikisha na wengine wangeenda kujiandikisha siku isiyo ya sikukuu? Ibara ya ngapi ya Katiba ya Zanzibar, 1984 imezitambua siku za mapumziko kuwa Jumamosi na Jumapili na siku za Sikukuu?
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  .

  Buchanan.

  Hiyo ni kwa mujibu wa katiba ambayo ndio sheria mama za nchi. Hebu pitia kalenda ya Serikali utaona siku zilizobainishwa na Serikali kama ni siku za mapumziko.

  Kutokana na katiba ya
  Tanzania ,sheria za nchi, Kifungu cha 15 Ibara ya 6 ya mwaka 1984 inasema hivi
  Sasa vifungu hivyi ni mwiba mkali sana kwa sakata zima.
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  .

  Buchanan.

  Hiyo ni kwa mujibu wa katiba ambayo ndio sheria mama za nchi. Hebu pitia kalenda ya Serikali utaona siku zilizobainishwa na Serikali kama ni siku za mapumziko.

  Kutokana na katiba ya
  Tanzania ,sheria za nchi, Kifungu cha 15 Ibara ya 6 ya mwaka 1984 inasema hivi


  Sasa vifungu hivyi ni mwiba mkali sana kwa sakata zima.
   
 7. O

  Omumura JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sioni cha zaidi ya kutafuta sympathy kwa wananchi,zaidi ya hapo hakuna aliyewalazimisha hao jamaa wakajiandikishe katika siku hiyo.Mambo mengine ni lazima tutumie akili ya kuzaliwa na sio kutafuta visingizio mapema kabla ya uchaguzi.Pamoja na watanzania kuwa na mwamko wa kupigana na mafisadi hivi sasa, bado vilevile hawatakuwa tayari kutumika kisiasa kama walivyozoea kufanywa na watu type ya akina Duni Haji na wengineo waliopo either ccm au vyama vingine, habari ndo hiyo!!!
   
 8. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mara nyingi shughuli hizi zinafanywa kwenye siku za mapumziko ili kuruhusu kila mwananchi aweze kufikiwa/kuhudumiwa. Wale ambao wana majukumu ya kikazi huo ndiyo wakati wao. Sidhani kama kuna dini inayokataza mtu kujiandikisha siku ya mapumziko. Huku ni kutapatapa kwa hawa waheshimiwa.

  Amandla......
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Sep 22, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nashindwa kujadili na wewe maana nimeuliza juu ya Katiba ya Zanzibar, 1984 wewe umejibu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1984 ambayo haipo kwa maana kwamba Katiba hiyo haikutungwa mwaka 1984!
   
 10. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Kila siku CUF wanalalamikia tume ya uchaguzi Zanzibar, hivi wao si ni sehemu ya tume hiyo? mbona wana makamishina kwenye tume hiyo? wanajilaumu wenyewe ama ni maigizo kwa wazanzibar?

  Kila siku viongozi wa CUF wanalia juu ya ZEC sasa mbona hawawaambii makamishina wao wakajiuzulu?
   
 11. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  .

  BARUBARU aHSANTUM KWA KULIONA HILO. Kwani watu wengi hawajui kuwa hizi kasoro ndogo ndogo ndizo zigharimu sana taifa mara baada ya uchaguzi kwisha. Kwani kunakuwa na mapingamizi kibaaaaaaaaaaao.


  Buchanan.

  nafikiri wewe una chuki na Znz na waZnz na hupendi watu wajifunze.

  Na mimi naomba nikufahamishe kuwa Znz kuna uchaguzi wa aina mbili
  1. Ule wa wawakilishi na Wa rais wa zanzibar( huu upo chini ya ZEC na sheria za Znz)
  2. Ule wa wabunge na rais wa muungano( Upo chini ya NEC na sheria za Tanzania)

  sasa utaona daftari hilo linazihusu chaguzi zote mbili yaani za wabunge, wawakilishi, rais wa Znz na wa muungano hivyo inakuwa kama kuku na yai
   
 12. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Si kamba unashindwa kujadili na mimi BALI HUWEZI KABISA kujadili na mimi kama mambo madogo madogo HUJUI.

  Nimesema KATIBA YA TZ (nikaweka koma) ambapo nimemaanisha Katiba ya Mwaka 1977,
  Kisha nikaendelea Sheria za Nchi, na nikakupa (kifungu cha 15 ibara ya 6) ambacho kilifanyiwa na kuingizwa ndani ya katiba ya TZ mwaka 1984.
  Kitaalamu tunasema hivi ( katiba ya TZ, KIF 15, Ib 6 cha 1984).

  Sasa kutokana na uwelewa wako mdogo nazidi kukurahisishia Fungua katiba ya ZNZ pg 39 para 3 mpaka 6, utaona hilo unalotaka.


  Nazidi kukushukuru Br Hafif kumbainishia wazi Buchanan. nakushauri tu ujue its better to have them IN pissin' OUT lather than having them OUT pissin' IN
   
 13. K

  Kinyikani Member

  #13
  Sep 23, 2009
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 65
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  watanganyika kazi yao ni mbege na wezi tu
   
 14. C

  Calipso JF-Expert Member

  #14
  Sep 23, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tunachozungumza ni kuwa katiba imevunjwa au haijavunjwa,na kwanini wafungue vituo siku ya Eid ya kitaifa ambapo kuna sheria kabsa kuwa hairuhusiwi? kwa maana hiyo kwanza wamekiuka sheria na la pili walikuwa wana nia yao,maana wanajua siku ile watu wengi wanatembea kwa hiyo watapata kuandikisha watu wao ambao ni mamluki. Mwaka huu tunasema Noooooooooooooooooooo. hata wakitupiga mabomu kwa helikopta kama juzi lkn watatoka tuuuuuuuuuuu.
   
 15. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #15
  Sep 23, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145


  Hiki kifungu ni cha jumla mno. Wekeni kinachosema kuwa ni marufuku kwa mwananchi kufanya kazi siku ya mapumziko! Hapa mnakamata chelewa wakati mnazama!

  Tuosheni ni wapi wamesema kuwa ni mwiko kufanya kazi siku ya mapumziko? Mbona unguja maduka yanafunguliwa siku za mapumziko? Mbona bara vioski vinafunguliwa siku za mapumziko. Mbona kote vituo vya mafuta vinafunguliwa siku ya mapumziko? Mbona wakulima wanalima siku za mapumziko? Mbona wavuvi wanavua siku za mapumziko? Serikali haina mamlaka ya kumlazimisha mtu apumzike siku fulani. Msitudanganye.

  Amandla.....
   
 16. C

  Calipso JF-Expert Member

  #16
  Sep 23, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tofautisha shughuli za Serikali na za Binafsi.
   
 17. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #17
  Sep 23, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo Katiba inasema MARUFUKU kufanya SHUGHULI za kiserikali siku ya mapumziko? Tuonyesheni basi wapi inaposema hivyo! Mbona polisi wanafanyakazi siku za mapumziko. Mbona wanajeshi wanakuwa kazini siku za mapumziko. Mbona hospitali za serikali hazifungwi siku za mapumziko? Mbona bandari zinafanya kazi siku za mapumziko. Mbona zimamoto wako kazini siku za mapumziko? Mbona wakunga wanazalisha siku za mapumziko? Mbona vivuko vinafanya kazi siku za mapumziko? Unataka niendelee?

  Acheni uongo. Na unafik.

  Amandla......
   
 18. C

  Calipso JF-Expert Member

  #18
  Sep 23, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Inaonekana badoooo wewe.
   
 19. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #19
  Sep 23, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Umeishiwa?

  Amandla.....
   
 20. C

  Calipso JF-Expert Member

  #20
  Sep 23, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Katiba imepindishwa na na sheria imekiukwa,basi acha iendelee tumezowea kwa hilo ktk ccm ili kuhakikisha yao yanakwenda,siwezi kubishana na wewe wakati kitu kipo wazi kabisa... wa waendelee kupiga mabomu ile ndo sheria inavosema na katiba inavotaka. Mkuu haya yanauma wewe tuyaaache tu. kila la kheri..
   
Loading...