Dumu la lita 20 mafuta ya kupikia sasa ni Tshs 90,000, bado yanaenda juu

Kwa style tunayoenda nayo Magufuli lazma akumbukwe bila kupenda.

1. Tozo
2. Bei ya vitu kupaa
3. Serikali haina kauli 1 tena.
4. Wakazi wa Dodoma
5. Wenyeji wa Chato

Yaani mwanaume mwanaume tu. Wengi tulimchukia sana Magufuli lakini hata kama hatokumbukwa lakini kimoyo moyo lazma umkumbuke.
Ile hali ya JK imesharudi rasmi ndani ya utawala.
  • Toka serikali iliposema inafatilia mambo ya tozo hakuna mrejesho mpaka leo.
  • Toka tume ya kuchunguza kuungua kwa soko la Kariakoo hatujapata mrejesho wa tume hiyo na siku za nyongeza 7 walizopewa sasa tupo zaidi ya 21 hakuna wa kuuliza watu wako bize kusafiri tu.

Kweli sikumpenda JPM ila namkumbuka tu sio kama napenda ila nalazimika kumkumbuka.
Na bado.
 
Nadhan wangetilia mkazo kwenye hili swala lakn wapo bize kukandamiza upinzani POLISI NAO MABWEGE SANA HADI NGUO ZINATOBOKA MATAKONI KWASABABU YA KUPAMBANA NA UPINZANI akiwauliza tatizo nn hata was hawajui sababu

CCM wanunulien POLISI sare mpya

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app

wanazungumzia mafuta ya kupikia kupanda bei sio upinzani peleka ajenda yako pengine ndio maana mnapigwa kama vile wezi wa viatu msikitini
 
Rudini mashambani mkalime michikichi na alizeti kwa wingi kama mnataka bei ya mafuta ya kula kushuka.
 
Mbona sisi tunanunua lita 5,000? Nikadhani wanauza 100,000 kwa dumu!
 
Mi nimejinunulia Machine ya kukamulia mafuta nyumban Saba Saba nikimekimbia vitu hivyo hivyo. Bei ya mafuta unakuta ipo juu halfu mafuta yenyewe hayana ubora yanasababisha Magonjwa.

Sasa hivi najikamulia mfuta ninayoyataka mwenyewe
Shida sio mashine shida ni malighafi. Wekezeni kwenye kilimo cha malighafi yanayozalisha bidhaa ya mafuta.
 
hivi unauhakika wengi walimchukia JPM? wakati akifanya ziara mikoani ilikuwa ukiangalia, au mikutano yake. msiba wake uliona watu pamoja na viongozi waliomzika. TZ hakuna rais aliependwa kama JPM
Sio kweli
 
Shida sio mashine shida ni malighafi. Wekezeni kwenye kilimo cha malighafi yanayozalisha bidhaa ya mafuta.
Ngoja nianze kuishi kwa Mbinu maana hakuna namna. Kwa sisi wa mikoani unanunua mbegu za alizeti gunia moja kwa elfu 45 unakamua kwa elfu 10 grahama zingine elfu 5 kisha unapata lita 22 unakuwa ume save kati ya elfu 40 au 50. Mjini mbinu.
 
Wapi huko gunia la ALIZETI linauzwa elfu 45?
 
Wanatangaza wanachukia ila moyoni wanampenda
Tutamkumbuka magufuli aidha kwa kupenda au kutopenda mzee alikuwa kiongozi bora
hivi unauhakika wengi walimchukia JPM? wakati akifanya ziara mikoani ilikuwa ukiangalia, au mikutano yake. msiba wake uliona watu pamoja na viongozi waliomzika. TZ hakuna rais aliependwa kama JPM
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom