Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Msanii mkongwe katika muziki wa Bongo fleva Dully Skyes amefunguka na kusema ugomvi wa wasanii Alikiba na Diamond kwa sasa ni mkubwa kwani umeshatoka mpaka kwa watu wa nje.
Dully Skyes akiongea kwenye kipindi cha Planet bongo alisema kwa sasa wasanii hao kupatana ni jambo gumu sana ila yeye anasubiri mpaka watakapotokea wasanii wengine wenye majina makubwa kama wao ndipo itakapokuwa rahisi kuwaweka chini na kumaliza tofauti zao.
“Kuwapatanisha inawezekana lakini si kwa ‘Age’ hii waliyofikia ni ‘Age’ ya sifa kila mtu anataka sifa na kila mtu anataka kuwa mkubwa kwa hiyo mimi nitasubiri baadaye kidogo itakapofikia muda kama miaka mitano hivi mbele au mitatu Mungu akipenda, vuguvugu hili litakapokwisha mimi na uwezo wa kuwakutanisha na kuwaambia ugomvi umekwisha lakini kwa ugomvi wao kupatana leo au kesho kwa sasa si kweli” alisema Dully Skyes.
Dully Skyes alizidi kutoa ufafanuzi kwa nini wasanii hao kwa sasa kupatana si jambo rahisi na kusema ugomvi wao umetoka nje mpka kwa watu wao wa karibu na mpka kwa mashabiki hivyo inahitaji muda.
“Unajua ugomvi wao si wa wao peke yao saizi ugomvi wao ni wa watu wengi kumbuka kuna team pale huyu ana team yake na huyu ana team yake, kwa hiyo kuanza kusimamisha watu kwanza wa nje wawe marafiki halafu kuja kuwakutanisha wenyewe, au uwakutanishe wao wawe marafiki halafu watu wa nje wawe marafiki ni kazi kubwa sana ngoja vuguvugu lao kwanza lipungue.
Waje Alikiba na Diamond wengine halafu mimi nitaweza kuwatuliza wao” alimalizia Dully Skyes
Source: EATV