Dullah Planet kuwa makini, Sepenga anakuharibia show

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
7,909
13,476
Napendaga kuangalia friday night live show inayorushwa na East Africa TV na East Africa Radio na host wa show ni Dullah Planet. Sasa kuna jamaa yake wanakuwaga wote kwenye show. Huyu jamaa nadhani anaitwa Sepenga. Jamaa ni mshamba sana.

Kwanza sijui kama ni maarufu. Na kama ni maarufu sijui kaupata wapi. Pamoja na kuwa kwenye show na dullah kwa muda sasa jamaa bado tu hajaizoea camera. Anapenda kuonekana yeye kuliko hata wageni wanaokuja pale kwa ajili kuleta video zao mpya. Anaingilia sana maelezo ambayo mgeni anakuwa anayatoa. Kwa kifupi anamkatishakatisha wakati akiongea kwa maswali ya kibwege kabisa.

Kwa kifupi mle ndani jamaa anavyofanyafanya ni mambo ya kiduanzi. Dulla huyo mduanzi Sepenga usipokuwa makini atakuharibia kipindi. Kama vp mpige chini. Maana hana anachoongeza kwako. Zaidi sana anakuharibia.

Mpige chini.
 
Sio ataharibu shoo, sema ameharibu sho. Jamaa mpiga malele utafikiri wanaokunywa pombe ya kienyeji ambayo ukifika bandani mama muuza anakuja kukufunga suruali.
Yaani jamaa hana mpangilio wa kuongea, ana bwatuka bwatuka tu.
Halafu wenzangu mnamwonaje? Mbona kama
 
Nye nye nye" in sepenga voice.
Screenshot_20210709-210354.jpg
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom