Ufafanuzi na Mchanganuo Kuhusu Biashara ya Vipodozi na Urembo

Naomba msaada natamani kufungua duka la vipodozi.

Naomba kujua je?
  • Hio pesa inatosha kwa kuanza na bidhaa tu maana frem na kabati la kioo tayari.
  • Mzigo naweza kupata wapi maana mm nipo mbeya.
  • Mazingila nayo kaa ni uswahilini na hakuna duka la vipodozi naomba ushauli wenu.
  • Kwa mtaaji wa 2.6 nilazima niende TRA au TFDA? Nasikia kwa mtaaji huu naweza kukata kile kitambulisho tu cha 20k kinacho toka kwa mtendaji.
Je, kunaukweli?

Ni bidhaa zipi za vipodozi nizizingatie sana.

Naomba msaada wenu.
 
Kama uko uswazi fungua sehemu ambayo imechangamka zaidi na kuna wadada wengi. Anza na bidhaa chache chache za urembo huku ukisoma aina ya wateja wako wanapendelea nini. Wa kiswazi wengi wanapenda mikorogo mikorogo... jifunze mikorogo inatengenezwaje, bidhaa za kuchanganya ili upate mkorogo lazima uzijue.

Usilete bidhaa za bei kubwa zitakudodea. Ajiri Muuzaji mrembo aliyejikoboaaa na kupendeza awavutie wadada. Usiweke bidhaa za aina moja... weka zooote kama mafuta ya nyonyo, nazi, vibanio, rasta, shanga za kiuno na miguuni na vingine
 
Unatazamia kupata mtaji na kufikiria biashara ya kufanya au tayari umepata mtaji ila bado unaifikiria biashara ya vipodozi?
Leo nakuandikia wewe kwa ajili ya kukupa mwangaza kidogo wa namna ya kuanza na gharama zake.

FAIDA YAKE IKOJE?
Biashara ya vipodozi (duka la reja reja) iko wazi moja kwa moja haina mambo ya siri wala mambo ya nyuma ya pazia. Unaandaa chumba na kuweka makabati pamoja na shelves, kisha unapanga vipodozi vyako aina mbalimbali (Losheni, body spray, mafuta, sabuni, shampoo na kadhalika) na kuuzia wateja wako watakaokuja kununua.

Wewe unanunua kutoka maduka ya jumla kwa bei ya jumla, kisha unauza kwa wateja wako kwa bei ya reja reja. Bei ya reja reja = bei ya jumla + faida. Mara nyingi faida = 10% hadi 50% ya bei ya jumla.

Kwa hiyo kwa mfano ukinunua losheni kubwa ya NIVEA kwa Tsh 10,000 wewe unatia faida ya 20% ambayo ni sawa na Tsh 2,000 kisha kuuza losheni hiyo kwa bei ya reja reja = bei ya jumla + faida = Tsh 10,000 + Tsh 2,000 = Tsh 12,000.

Kwa hiyo unakua umenunua kwa Tsh 10,000 na kuuza kwa Tsh 12,000 hivyo kupata faida ya Tsh 2,000; ukiuza makopo 50 kwa mwezi unapata faida ya Tsh 100,000.

Kwa hiyo kwa kifupi ni kwamba faida huwa kati ya 10% hadi 50% ya bei ya kununulia mzigo wako, kutegemea na bidhaa husika. Kuna mwezi unaweza kununua mzigo wa Tsh 3,000,000 na kupata faida ya Tsh 400,000; na kuna mwezi unaweza kununua mzigo wa Tsh 3,000,000 na kupata faida ya Tsh 600,000.

Ila kwa ujumla biashara ipo na faida yake ni nzuri. Cha msingi uwe na wateja wa kutosha na uwauzie bidhaa nyingi au za thamani kubwa. Chagua eneo zuri la kuweka duka lako, ukifeli location utapata tabu sana.

Location ndo kila kitu. Usijiweke kwenye ushindani usiouweza, usijiweke pasipo na wateja wanaoziweza na kupenda bidhaa zako, usijiweke eneo lisiloruhusiwa, usijiweke mbali kiasi cha wateja wako kufikiria mara mbili mbili kama waje kwako au waangalie sehemu nyingine tu.

Duka la vipodozi.jpg

MTAJI KIASI GANI UNATAKIWA?
Mtaji unategemea na gharama za eneo lako, ukubwa wa duka na vipodozi utakavyoanza navyo. Tsh 4,000,000 hadi Tsh 8,000,000 inatosha kuanzia.
MTAJI = Gharama za kukodi na kuandaa duka + gharama za vibali, vyeti na leseni (halmashauri + TBS + TRA + Brela) + gharama za kununua vipodozi + mawasiliano na usafiri + gharama za kujitangaza + Bili za maji na umeme + michango ya serikali za mitaa/kijiji+ Akiba + Mengineyo.

Kwa mahesabu ya chini (Eneo la mjini) Inabidi uwe na angalau Tsh Millioni Nne (Tsh 4,000,000). Ikiwa chini ya hapo itabidi utumie akili nyingi sana na mbinu mbadala nyingi nyingi, ila ikiwa zaidi ya hapo maisha yako yatakuwa rahisi zaidi na duka lako litakuwa zuri sana.

So cha muhimu ukiwa na mtaji anza kuupangilia vizuri kabisa utautumiaje kuanza biashara yako. Panga mapema kabla hujanunua kitu chochote wala kulipia chochote. Ukihitaji ushauri na kupanga pamoja unaweza kucheki na mimi nitakusaidia: 0788179686 | afyazaidi@gmail.com

JINSI YA KUANZA BIASHARA
Kusanya taarifa za kutosha na ujiridhishe vya kutosha kabla ya kuanza biashara hii maana kuna baadhi ya mambo ambayo umewahi kuyasikia yanaweza yasiwe kweli au yasiendane na mazingira yako wewe. Ukishakuwa na taarifa za kutosha na kujiridhisha kwamba upo fit basi sasa unaweza kumalizia kujipanga, kujiandaa na kuanza.
  • Weka mtaji wako tayari
  • Tafuta sehemu ya kuweka duka lako
  • Wasiliana na TBS upate uhakika kwamba hapo duka lako litakubaliwa
  • Lipia kwa mwenye jengo na pata mkataba
  • Kama hauna TIN nenda ofisi za TRA ukiwa na mkataba, kitambulisho cha Taifa na barua kutoka serikali za mitaa kwa ajili ya kupatiwa TIN (TIN ni bure, ila unaweza kushauriwa kulipia kabisa makadirio ya kodi yako ya robo mwaka)
  • Nenda ofisi za TBS kwa ajili ya kupata kibali cha duka la vipodozi (Utalipia ada ya kibali)
  • Nenda ofisi za halmashauri ukiwa na Copy ya kataba, kitambulisho chako, TIN na kibali kutoka TBS kwa ajili ya kupatiwa leseni ya biashara (Utalipia ada ya leseni)
Ukiwa na TIN ya TRA, Kibali cha duka la vipodozi kutoka TRA na leseni ya biashara kutoka Halmashauri hapo sasa utakuwa tayari kufungua duka lako na kuanza biashara.

UMEIPENDA KWELI?
Kama umeipenda kweli biashara hii basi kila la kheri. Ni nzuri na ukiifanya kwa moyo na akili utafanikiwa.
Ukihitaji maarifa zaidi, business plan, list ya bidhaa, kupangilia matumizi ya mtaji, kuelewa changamoto, support na mambo mengine mengi nipigie au nitumie meseji/email nitakupa maujanja.

UKIHITAJI USHAURI NA MUONGOZO MZURI
Anza kutuma meseji yenye neno BIASHARA YA VIPODOZI kwenda namba 0788179686 kisha utapokea dondoo na mambo mengine mengi ya muhimu kuyafahamu.
Karibu sana AFYA ZAIDI (AZ) CONSULTANTS!
0788179686 | afyazaidi@gmail.com | Afyazaidi | Nyumbani



AFYA ZAIDI CONSULTANTS LOGO.jpg
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom