Duka la MSD Muhimbili lazidiwa idadi kubwa ya msongamano wa watu kununua Sanitizer: Ikumbukwe liko moja kuhudumia Dar na Pwani

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Msongamano uliopo sio wa kitoto, watu wanazidi kumiminika kuja kununua sabuni maalum ya maji ya kuulia virusi (sanitizers) katika duka la MSD Muhimbili!

Ambalo ndilo duka la MSD moja pekee katika serikali ya awamu ya tano linalouza sanitizer Dar na Pwani!

Wakati hayo yakitokea hapa Tanzania! Nchi ya Kenya imesema inaandaa sanitizer ili kugawa bure nchi nzima!
 
masoudkipanya_B95nJqvjY8-.jpeg
 
Tatizo kwenye maduka binafsi ya dawa, wamepandisha bei aisee.. Imagine mask iliyokuwa inauzwa Tshs. 500/=, sasa hivi mask hiyo hiyo inauzwa Tshs. 3,500/=.. Wenye mamlaka wangelijua mapema hili kwamba kwenye demand kubwa hizi zingepanda bei, wangekuwa wameshajipanga..
 
Katika maradhi ya milipuko kama hii corona nchi zote duniani hutengeneza bajeti pamoja na mkakati wa kupambana na hali hiyo hii ikiwa ni pamoja na matibabu na kuzuia maambukizi. Matumizi au gharama za moja kwa moja kwa serikali ni chanjo ikiwa ipo, madawa, sanitizers, masks, vyakula ikiwa kuna kuzuia watu kwenda kujitafutia, maji, umeme, vyote hivi huwa BURE hadi pale mfumuko wa gonjwa unapoisha. Sasa kwetu sijui itakuwaje! Maana hawa watu ni mali ya Jamhuri kama inavyodaiwa wakati tukiwa wazima. Jamhuri iko vizuri kuwahudumia wakati huu wa corona na mkipona mrejee makazini kuziba pengo. Asanteni kwa kunisikiliza.
 
MSD wameondosha duka lao muhimbili kwa maelezo kwamba muhimbili wamesema wanajitosheleza wenyewe na duka lao la dawa.
 
Back
Top Bottom