Duh, Tususie mechi za timu ya Taifa na Ligi kuu ya VODACOM?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,278
6,636
Wakuu inaonyesha Wabongo wana hasira sasa
hebu soma hii meseji ambayo na mimi nimetumiwa
na mtu ambaye naye katumiwa pia....

Je, wewe ni mpenzi wa soka? wakati umefika
sasa kwa wapenzikususia mechi za timu ya
Taifa na LIGI KUU mpaka TFF itakapoonyesha
nia ya dhati ya kuinua soka letu. kuingia
kwenye mechi ni kuzidikudidimiza soka letu.
TUSUSIE HATA KUSIKILIZA. Isambaze kadri uwezavyo.
Time: 12/9/2012 1:15:38 PM
 
Mi nishasusia toka Maximo alipofanyiwa MIZENGWE, nilikuwa Yanga.
Timu ya Taifa nimechagua GHANA klabu kwa nje nilikuwa LIVERPOOL
lakini kwa sasa niko MANCITY kwa mkopo, angalau napata raha ya soka.
 
Hata mimi nimeamua kususia, yaani wale wanaume wetu uwanjani
wako legelege kama nini vile..... Nilitamani kulia jinsi wale wanaume wa
wenzetu walivyokuwa wanahangaika uwanjani. Sijui hawali wale.......
Yaani wamenikera.... nahisi hawa wa kwetu wanashindia soda na biskuti
mbona mesi ni mfupi kama wao lakini ana nguvu?
 
Jamani taifa letu limeoza kila sehemu.

Tunashanga nini hapo cha ajabu?

Tuhamasishane kuondoa viongozi wazembe kwenye siasa, wanasiasa wanavyoboronga ndivyo kila kitu kinavyochacha.

Jiulize wizara husika inafanya nini? kinachofanywa na wizara ya michezo hakina tofauti na wizara ya elimu, afya, maliasili nk.

Kuoza kwa sisiem na ufisadi ndiyo sababu ya kuchacha kila kitu, wanasiasa hawajishughulishi na kuumia kwetu mioyoni wao

wanafikiria namna ya kuiba wanyama wakiwa hai, madini, mikataba feki nk. TFF ni chambo tu mambo yapo kwa watawala.

Kutuletea makocha wa kigeni bila kuwa na mikakati ya kuandaa vipaji vya watoto kwa kuwatunza, kuwawezesha nk hatutafika.

Bila kuwa na wizara yenye mtazamo wa ushindi, hamasa na mbinu za kiushindani TFF peke yake ni bure.
 
Mi nishasusia toka Maximo alipofanyiwa MIZENGWE, nilikuwa Yanga.
Timu ya Taifa nimechagua GHANA klabu kwa nje nilikuwa LIVERPOOL
lakini kwa sasa niko MANCITY kwa mkopo, angalau napata raha ya soka.
huko mancity leo lazima uumie bila kujali upo kwa mkopo!!united 2 city 1!
 
Hata mimi nimeamua kususia, yaani wale wanaume wetu uwanjani
wako legelege kama nini vile..... Nilitamani kulia jinsi wale wanaume wa
wenzetu walivyokuwa wanahangaika uwanjani. Sijui hawali wale.......
Yaani wamenikera.... nahisi hawa wa kwetu wanashindia soda na biskuti
mbona mesi ni mfupi kama wao lakini ana nguvu?
nguvu zipi za messi unazoziongelea!!!
 
Mi nishasusia toka Maximo alipofanyiwa MIZENGWE, nilikuwa Yanga.
Timu ya Taifa nimechagua GHANA klabu kwa nje nilikuwa LIVERPOOL
lakini kwa sasa niko MANCITY kwa mkopo, angalau napata raha ya soka.
mkuu Mzee wa kurekebisha,pole utaendelea kukaa huko kwa mkopo au utakuja man u kwa usajiri wa kudumu!!
 
Last edited by a moderator:
kila siku naona unamkimbia mbuni, unamuogopea nini?
mkuu hako kaumbo kangu kadogo akinikanyaga nitabaki kweli!!
anyway in life you need to be running always!!hasa sisi tusio na historia ya ufisadi katika ukoo!!
 
mkuu hako kaumbo kangu kadogo akinikanyaga nitabaki kweli!!
anyway in life you need to be running always!!hasa sisi tusio na historia ya ufisadi katika ukoo!!

Leo kiongozi imekula kwa man city kama nilivokutabiria jana hongera mkuu.
 
Leo kiongozi imekula kwa man city kama nilivokutabiria jana hongera mkuu.
ni kweli kiongozi united naona kama watakula sikikukuu wakichekelea!!ila dakika za mwisho city walikua juu!!thank God Van yuko united!!!
 
ni kweli kiongozi united naona kama watakula sikikukuu wakichekelea!!ila dakika za mwisho city walikua juu!!thank God Van yuko united!!!

Asernal tunakula kwa macho si unaona upachikaji mabao umekuwa shida kwetu! mmepata jembe mkuu.
 
mkuu hivi hata lile kabati la kuwekea makombe bado mnalo au mlishaliuza!!!just kidding

Mkuu sisi huku Asernal ni mapenzi tu, hatuna chochote cha kujivunia kiongozi. kabati bado lipo japo vumbi imejaa halijapokea chochote kwa mda mrefu sana.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom