Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Pichani chini Waziri Mkuu amefanya ziara ya kushtukiza kwenye Hospitali Kuu ya Mkoa wa KLM, Mawenzi, na huko amekutana na matatizo ambayo yameniachia maswali mengi sana, pmj na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali yetu chni ya Raisi Magufuli
lkn kunaonekana kwamba tuna matatizo makubwa sana kama nchi na tunahitaji blueprint ya namna ya kutatua haya matatizo kwa mara moja ili yasiendelee kujitokeza huko mbele, jambo ambalo nimeligundua sehemu kubwa sana ya haya matatizo kwenye hili eneo la Afya ni uzembe tu wa wahusika na kutokujali kwa mfano Wagonjwa hawana Dawa Mkuu wa Hosp. anaulizwa anasema wameagiza Dawa MSD tangu miezi 2 iliyopita lkn bado hazijafika, sasa hapa kuna tatizo hizi Dawa si zinatoka km 500 tu ktk Moshi yaani DSM iweje zichukuwe miezi 2?
Hii ni sehemu tu ya matatizo makubwa aliyoyakuta W.Mkuu huko Mawenzi Hospitali na haya matatizo yapo kila Hospitali ya Mkoa nchi nzima, sasa tufanye nini? Yaani tutatue vipi haya matatizo?
,,RESPECT"
Hii ni sehemu tu ya matatizo makubwa aliyoyakuta W.Mkuu huko Mawenzi Hospitali na haya matatizo yapo kila Hospitali ya Mkoa nchi nzima, sasa tufanye nini? Yaani tutatue vipi haya matatizo?