Quemu
JF-Expert Member
- Jun 27, 2007
- 984
- 133
Hii siku huwaga inanitoa nishai sana. Kwa sababu huwa inakuja just before payday. kwa wale wenye akaunti zinazotuna terehe 15 na siku ya mwisho wa mwezi wanaelewa nina maana gani.
Inanitoa nishai kwa sababu huwa inakuja wakati mifuko imetoboka vibaya mno. Na mamsapu huwa atulii mpaka apate maua ya roza, dina, kadi na kazawadi kadogo. Yani huwa hata haelewi nikimwambia kuwa mwenzio sina ngawira hata chembe.
Kwa mahesabu ya haraka haraka, yani inabidi niwe na kama kiasi hiki ili niweze kuipitisha siku ya valentina nimelala kitandani, badala ya kwenye kochi.
1) Maua ya roza - $80
2) Dina - $50
3) Kadi - $5
4) Zawadi - $100
Total = $235. Yes, mamsapu wangu huwa anaweka kiwango cha kuspendi nae. Haya ndio matatizo ya kutulia na sistaduu...gademu!
Sasa hebu nishaurini, kwa mfuko uliotoboka, ni vipi nitaweza kufanikisha hii siku ipite murua?......Na siku hizi hata hot-check huwezi andika tena. Zamani ulikuwa unaweza kwenda agalau Wal-Mart na kuandika check wakati unajua hauna hela kwenye akaunti. Mambo yalikuwa yanajipa mbele kwa mbele. Lakini siku hizi hata Wal-Mart wana sisitimu ambayo ina access akaunti yako kucheki kama kuna ngawira kabla hujaanza mbele na bidhaa. Na haya mambo ya Payday Advances yamekuwa magumu kweli kweli siku hizi. Mpaka wampigie simu bosi wako ndio wakupe ki $200 chao. Na bosi ni mbeya kishenzi...haitachukua masaa 2 kabla dipatimenti mzima haijajua yaliyojiri kwenye ulimwengu wa mfuko wako. Na kwa bahati mbaya au mzuri, tumejazana wabongo kinoma kwenye warehouse ninayopiga mzigo (si unajua tena mambo ya kupiga boksi). Sasa hebu niambie hizi habari zikifika masikioni mwa wabongo, sijui nitajificha wapi...maana ndani ya masaa 2 zitakuwa zimebandikwa kwa Michuzi.. Duh jamani!!!
Anewei, sasa nifanyeje? Hivi kwani ni lazima yawe maua ya rozi? Hivi ni vipi nikimpatia maua ya saa nne? Unajua kwanza wakidada huwa hawafikirii vizuri. Maua ya saa nne pengine ni romantiki zaidi ya maua ya roza. Maua ya rosa yanachanua pale mwanzo mwanzo tu, kesho yake yanaanza kufifia. Lakini maua ya saa nne huwa yanachanua kila siku saa nne....kila siku saa nne huwa yana kuwa "mwarumwaru."...hebu niambie kuna kitu romantiki kama kile chenye uhakika wa kutabasamu kila siku...tena muda ule ule. yani huna hata haja ya kuwa na wasiwasi wa kujua ni saa ngapi yata chanua.
Gademu!!!