Duh! Rais Samia amkataa mama mnyonge aliyetaka kumlilia kama Magufuli. Nenda kakae…

Nilisikilza hiyo statement ya bahati mbaya sana, nikajiuliza maswali mengi. Naunga mkono hoja kuwa mama aandikiwe speech, akifika pale azisome bila kuongeza mawazo yake binafsi kama hayo ya bahati mbaya na mipasho mingine. Anatu let down wanawake.
Ukianza na ile speech ya urefu wa kamba, SPIKA KUJIUZULU, na hii bahati mbaya serikali haitoi hukumu BALI NI MAHAKAMA, swali ni kuwa hawa viongozi wanaelewa kweli umuhimu wa hii mihimili? Unawawezaje kujadili statement ya leo ya bahati mbaya bila kuhusisha na kinachoendelea mahakamni (mtuhuru in engish) kwa kesi ya ufisadi?

Hakuna Rais hapo!
 
Kafanya sahihi na hiyo ndiyo good governance, delegation of power, division of labour, organization structure na specialization. Atawajibu wangapi?

Ule ulikuwa ni upumbavu wa Mwendazake tu na kutaka masifa matatizo ya wananchi hayatatuliwi namna ile. Hata akina Nabii Musa walioishi miaka 4,000 kabla ya Kristu walishauriwa wasitatue matatizo kwa namna ile.

Soma Kutoka 18: 19-22
Musa. Alipokuwa kiongozi wa Israeli, ghafla alikuwa mtu mwenye shughuli nyingi. Watu wa Mungu walihesabiwa mamilioni na maisha ya Musa yalikuwa magumu kwani alihukumu na kuwahudumia watu tangu asubuhi hadi usiku.

Kuangalia yote haya, mkwewe wa Musa Jethro aliingilia kati na kumuonya Musa kwamba atajifunga mwenyewe ikiwa haitafanya mabadiliko.

"Wewe ni mchungaji, Musa, na unahitaji kujifunga na Mungu. Wape wengine kazi za ugomvi na ushauri nasaha. Kisha uwe peke yako na Mungu, utafute uwepo wake, pata akili yake, na upokee neno lake. Hii inapaswa kuwa kipaumbele”
Mama kaupiga mwingi hivo yeye anaamini tu kuwa yeye hayo ya wengine hayamhusu .
 
Umenena vyema! Ila kuna kundi kila madahaifu ya Rais wanapiga mapambio! Yaani Rais anaonesha hadharani hawezi kujali masrahi ya mwananchi wa chini Wasaidizi wake si ndo itakuwa balaa!
Ndio lumumba buku 7 hao yani hata siku kiongozi akijinyea watasema ni mfumo wake wa tumbo unafanya kazi vizuri tu ni hali ya kawaida mtu kujisaidia😅
 
Huyo mwenye shida ni mnyonge asiejua hata huo utaratibu wa kusubiri. Yeye anachojua ni kupaza sauti tu kuomba msaada.

Angemsikikiza ili ajue atakapo kwenda kuona alichoandika alinganishe na maneno mubashara kutoka kwa muhusika.

Usipende kurahisisha mambo hujui mtu anamaumivu ya kuonewa kiasigani.
Hii nchi itakapofikia watu wanaviziana na kuuana ndipo ambapo serikali itastuka😜 na kugundua kuwa kumbe inatakiwa iwajibike kwa matatizo ya wananchi
 
Hawa jamaa ni wajinga sana! Rais analipwa na kulishwa na kodi za watanzania! Sasa yupo hapo kwa ajili ya tumbo lake au watanzania! Rais akikosea lazima asemwe yeye ni nani?
Mbona JPM mlikuwa mnamuona mdogo wake mungu, na waliomkosoa walikiona cha mtema kuni, wengine wakapotezwa wengine wamebaki kuwa walemavu mpaka leo...au JPM alikuwa halipwi mshahara na wananchi? Maana mzee alikuwa anaona wengine wote kama ng'ombe tu isipokuwa yeye!

Mama is doing good, mwacheni aijenge nchi, msemeni anapokosea ili mambo yaende saw a sawa
 
Wananchi milioni 50 wanaishi huko vichochoroni, Rais akiwasikiliza wote hatafanya kazi nyingine.Jawabu la Miungu watu wa vichochoroni ni KATIBA MPYA.
Raisi hawezi sikiliza watu zaidi ya 3 kwenye hotuba. Hio inajulikana kabisa sema tu raisi wetu wa sasa amedhihiri kuwa hana time na wanyonge 😂
 
Hilo dawati/madawati hayataasaaidia mtu yoyote ikiwa wenye nafasi ya kufanya hivyo wamegoma kutoa msaada.
Kwa watanzania Hawa, bila pesa hakuna msaada hata ufanyeje.
Kuna mtu kanyanyaswa na halmashauri, kaenda kwa mkurugenzi holaaa, kaenda kwa mkuu wa wilaya holaaa, kaenda kwa mkuu wa mkoa holaaa kote huko hakuna anayempa majibu.
Huu ndio uhalisia wa sehemu nyingi nchini.
Yani hapo kwa tafsiri tu huyo mama haki ndio ishapotea aandike maumivu tu😅!

Sababu kuu ni kwamba hao wanaotakiwa kumsaidia wote wanamuona msumbufu sababu hela ya kuhonga hana na sio mtu wa maana. Ubaya haya yanafanyikaga kwa coordination sababu viongozi wa level zote wana mawasiliano na taarifa juu ya huyo mtu isipokuwa raisi mwenyewe.

Kwahio raisi kuli forward kwa watu wa chini yake still haitasaidia. Ni sawa na utume barua ya maombi halafu secretary aitupe kwenye dustbin. Usitegemee boss atakaa aione labda kwa neema za Mungu!
 
Hii Safi, inaondoa unafiki nafiki... mama afuate taratibu atasikilizwa, sio kusubiri barabarani na mabango, mahindi au jogoo.
Hizo taratibu za kibongo tena kwa awamu hii ya kula kwa urefu wa kamba yako mwenye mda na wewe kama huna pesa ya hongo ni nani? Huyo mtu amechoshwa na kuzungushwa.
 
Kafanya sahihi na hiyo ndiyo good governance, delegation of power, division of labour, organization structure na specialization. Atawajibu wangapi?

Ule ulikuwa ni upumbavu wa Mwendazake tu na kutaka masifa matatizo ya wananchi hayatatuliwi namna ile. Hata akina Nabii Musa walioishi miaka 4,000 kabla ya Kristu walishauriwa wasitatue matatizo kwa namna ile.

Soma Kutoka 18: 19-22
Musa. Alipokuwa kiongozi wa Israeli, ghafla alikuwa mtu mwenye shughuli nyingi. Watu wa Mungu walihesabiwa mamilioni na maisha ya Musa yalikuwa magumu kwani alihukumu na kuwahudumia watu tangu asubuhi hadi usiku.

Kuangalia yote haya, mkwewe wa Musa Jethro aliingilia kati na kumuonya Musa kwamba atajifunga mwenyewe ikiwa haitafanya mabadiliko.

"Wewe ni mchungaji, Musa, na unahitaji kujifunga na Mungu. Wape wengine kazi za ugomvi na ushauri nasaha. Kisha uwe peke yako na Mungu, utafute uwepo wake, pata akili yake, na upokee neno lake. Hii inapaswa kuwa kipaumbele”
Kama hizo delegation of power, specialization of labor zingekuwa zinafanya kazi kwa weledi hao watu wasingekuwa wanafika kuanika mabango kwenye hafla na hotuba za raisi
 
Yani hapo kwa tafsiri tu huyo mama haki ndio ishapotea aandike maumivu tu!

Sababu kuu ni kwamba hao wanaotakiwa kumsaidia wote wanamuona msumbufu sababu hela ya kuhonga hana na sio mtu wa maana. Ubaya haya yanafanyikaga kwa coordination sababu viongozi wa level zote wana mawasiliano na taarifa juu ya huyo mtu isipokuwa raisi mwenyewe.

Kwahio raisi kuli forward kwa watu wa chini yake still haitasaidia. Ni sawa na utume barua ya maombi halafu secretary aitupe kwenye dustbin. Usitegemee boss atakaa aione labda kwa neema za Mungu!
Wako wangapi wenye shida kama hizo sasa.. Au Rais awe anatenga muda katika ratiba zake wa kufika kila wilaya kusikiliza matatizo yaliyoshindikana na watendaji wake? Liko practical kweli hilo?
 
Nilisikilza hiyo statement ya bahati mbaya sana, nikajiuliza maswali mengi. Naunga mkono hoja kuwa mama aandikiwe speech, akifika pale azisome bila kuongeza mawazo yake binafsi kama hayo ya bahati mbaya na mipasho mingine. Anatu let down wanawake.
Ukianza na ile speech ya urefu wa kamba, SPIKA KUJIUZULU, na hii bahati mbaya serikali haitoi hukumu BALI NI MAHAKAMA, swali ni kuwa hawa viongozi wanaelewa kweli umuhimu wa hii mihimili? Unawawezaje kujadili statement ya leo ya bahati mbaya bila kuhusisha na kinachoendelea mahakamni (mtuhuru in engish) kwa kesi ya ufisadi?
Au mi nimeelewa vibaya... Ujue kuna baadhi ya watu kuongea kiswahili kwao.. Ili waeleweke.. Wanabadili maneno ya kiingereza kwenda kiswahili... Na hadhira anayoongea nayo, anaitafsiri kama ni wale "laymen" kabisa... Kwa hiyo anaiangalia hadhira, anaiona inamtegemea yeye kama "mtatuzi" wa mwisho wa shida zote za wananchi, wakati kuna masuala ya haki yanayotolewa maamuzi mahakamani. Nadhani hiyo statement isimhukumu Rais.. Ni kule kutafsiri neno "unfortunately" ambako kumesababisha hiyo sintofahamu...
 
Ule ujinga wa maigizo hatutaki,safi Sana Rais..

Haiwezekani kila mwenye tatizo amtafute Rais.
ukifikiria kwa kutumia nguvu kidogo tu utaelewa. Hakuna mwenye akili ambae atakaa na shida yake amsubiri raisi apite ndo amueleze.
Ukiona mama kamfata raisi kuelezea shida yake uwe na hakika hajapata msaada katika ngazi alizopita huko chini ndo mana anaona msaada wake utatoka kwa raisi.
Hukumbuki wakati wa Yesu? sio kama hapakua na waganga wa kutibu watu ila kwanini wagonjwa walikua wanamuandama Yesu? ni kwasabab hawakupata uponyaji kwa hao waganga.
Ukiona huyo mama kafanya ujinga omba yakukute ndo utapata akili
 
  • Thanks
Reactions: nao
Mtoto Mwenye Hekima na busara ,aliyelelewa vema na mwenye maadili,hawezi kumkatisha Mzazi au mkubwa wake wakati anaposema.
 
Maigizo nani kayaleta?

Ingeuwa wakati wa Magufuli mngesema hivyo.

Samia angepungukiwa nini kama angemsikiliza na kumpa mtu wa kumusaidia wa karibu zaidi?

Acheni kujifanya wapambe masiokuwa na msaada kwa Wananchi. Au kwa vile ni Urais wa Mchongo ndo maana wananchi wakae pembeni.
Alishaandika hoja yake na Rais kasema ataenda kuitazama na kuifanyia kazi, Sasa ulitaka amjibuje? Siyo Kila kitu kinapaswa kutolewa majibu ya papo kwa hapo vinginevyo itakuwa ni ukurupukaji. By the way Rais kamjibu kwa upole yeye akaendelea kung'ang'ania ndo maana kaamua kwa Mara ya pili kukaza sauti "KAA CHINI". Sijaona kosa la Rais
 
Raisi hawezi sikiliza watu zaidi ya 3 kwenye hotuba. Hio inajulikana kabisa sema tu raisi wetu wa sasa amedhihiri kuwa hana time na wanyonge 😂
Kukubali kuitwa mnyonge ni kuidhalilisha nafsi yako. Mungu aliumba binadamu mkamilifu mwenye nguvu za mwili na ubongo. Yeyote akizitumia akili zake na nguvu zake vizuri ana uwezo wa kupiga hatua kiuchumi na kijamii. Usikubali kuitwa Mnyonge, utapata LAANA kama aliyoondoka nayo Mwendazake
 
Back
Top Bottom