Elections 2010 Duh!!! Kweli nchi tunayo, fuatilia habari hii

mamanalia

JF-Expert Member
Nov 7, 2009
666
146
Kweli hawa watu wa tume ni wajinga sana yani hamna kitu kabisa. Nafikiri masikio yao yalishabomoka.

Hii habari toka mtanzania daima

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jana ilimtangaza mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete kuwa mshindi kwa kupata asilimia 61.17, ikiwa ni tofauti ya asilimia 21 ya ushindi alioupata mwaka 2005, ambao ulikuwa asilimia 82.

Akitangaza matokeo hayo kwenye ukumbi wa Karimjee mjini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Lewis Makame alisema jumla ya wapiga kura waliojiandikisha walikuwa mil. 20,137,303 wakati waliopiga kura ni mil. 8,398,394, sawa na asilimia 42.8. Jaji Makame alisema jumla ya kura 227,829 ziliharibika.

Jaji Makame alianza kwa kumtangaza mgombea wa Chama cha APPT – Maendeleo, Peter Kuga Mzirai, kwa kupata kura 96,933, sawa na asilimia 1.12, akifuatiwa na mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete, aliyepata kura 5,276,827, sawa na asilimia 61.17, akifuatiwa na mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibrod Peter Slaa aliyepata kura 2,271,941, sawa na asilimia 26.34, wakati mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba akipata kura 6,95,667, sawa na asilimia 8.

Jaji Makame, aliwataja wagombea wengine kuwa ni Hashimu Rungwe wa Chama cha NCCR Mageuzi, aliyepata kura 26,388 sawa na asilimia 0.31, akifuatiwa na mgombea wa Chama Tanzania Labour (TLP), Mgahywa Mutamwega aliyepata kura 17,482 sawa na asilimia 0.02 na kufuatiwa na mgombea wa UPDP, Fahm Dovutwa, aliyeambulia kura 13,176 sawa na asilimia 0.15.

“Kwa mujibu wa vifungu vya 35E,35F (8) na 81B vya sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi sura 343, ninamtangaza rasmi mgombea wa CCM, Jakaya Kikweye kuwa mshindi wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano ijayo,” alisema Jaji Makame.

Ushindi huo unaonyesha kutofautiana na utabiri wa baadhi ya kampuni za utafiti kutoa matokeo ambayo yalionyesha Rais Kikwete angeshinda kwa kiwango cha juu.

Miongoni mwa taasisi hizo ni REDET ambayo ilisema Rais Kikwete angeibuka na ushindi wa asilimia 74, huku Mwenyekiti wa Kampeni wa CCM kitaifa, Abdulrahaman Kinana yeye alitamba kuwa lazima Kikwete aibuke na ushindi wa asilimia 87.

Katika hali ambayo, haikutarajiwa, wageni waliohudhuria tukio hilo walipigwa na butwaa baada ya kushindwa kumuona mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, licha ya kushika nafasi ya pili na aliyetakiwa kutoa salamu za shukrani kwa niaba ya wagombea wenzake wa upinzani.

Hata hivyo kutokana na kukosekana kwake, nafasi yake ilichukuliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba kuwakilisha kambi hiyo.

Katika salamu hizo, Profesa Lipumba alionyesha mshtuko baada ya kuitupia lawama nzito NEC kuwa ni jambo la kushangaza kuona idadi kubwa ya wapiga kura waliojiandikisha walikuwa mil. 20,137,303 lakini waliojitokeza kupiga kura ni mil. nane ambao ni sawa na asilimia 42.8.

Alisema hilo ni tatizo kubwa ikiwa ni tofauti na mwenendo wa kampeni ambako watu walijitokeza kwa wingi katika mikutano yao, lakini siku ya kupiga kura idadi hiyo imepungua mno.

“Kutokana na hali hii, inamaanisha kwamba waliojitokeza kupiga kura na kumchagua rais ni asilimia 27, tunahitaji demokrasia, hapa tume katika hili imetuangusha, kwa kuwa hata watu wengi waliojiandikisha hawakuona majina yao… hivyo kukosa haki ya msngi na ya kidemokrasia ya kupiga kura,” alisema Profesa Lipumba.

Alisema tume kuaminiwa katika nchi ni jambo muhimu lakini kumekuwa na wasiwasi wa siku nyingi kutoka kwa wadau kuwa tume iliyopo si huru, jambo ambalo linapaswa kufanyiwa kazi.

Alimshauri Rais Kikwete kujenga malengo ya demokrasia, kupambana na ufisadi na kujenga utawala imara na ulio bora.

Katika hali ambayo watu hawakutarajia, Profesa Lipumba alimkabidhi Rais Kikwete Ilani ya chama chake kwa nia ya kutekeleza mambo yaliyomo, kwa lengo kujenga nchi.

Naye Rais Kikwete akitoa neno la shukurani, alivitaka vyombo vya habari kutibu majeraha ya uchaguzi yaliyojitokeza wakati wote wa kampeni, ili kujenga umoja na mshikamano uliopo.

Alisema wakati wa kampeni kulikuwa na maneno na vitendo ambavyo vilisababisha nyufa, ukiwemo udini na ukabila.

Akivishukuru vyombo vya habari, alivitaka kuhakikisha vinafanya kazi zao kwa umakini na kurudisha umoja.

Alisema kama chama wameupokea ujumbe wa upinzani na kuwa watakaa chini na kutafakari changamoto kubwa waliyoipata katika uchaguzi huo, kwa kuwa hakuna mshindi katika uchaguzi huo.

Akiwa anazungumza huku akitoa misemo mbalimbali, Kikwete alisema ndani ya CCM kuna misemo kwamba “mtu hawezi kugombea fito wakati wa kujenga nyumba, kwa maana nyumba itakuwa haiendelei kujengwa”.

Katika hatua nyingine, Jaji Lewis Makame alisema hadi sasa majimbo saba yaliyofanyika uchaguzi huo hayajatangazwa matokeo yake na kata 23 nazo pia hazijatangazwa, bila kutoa sababu za kutotangaza huko.
 
Ahadi za Mh. Kikwete zipo zaidi ya 90, sasa sijui kama ataweza kumaliza zake then aanze kutekeleza yaliyomo kwenye ilani ya CUF, ambayo imeelezea kuwa itatoa elimu bure mpaka chuo kikuu. kazi ipooooo!!!!!!!!!!
 
Ahadi za Mh. Kikwete zipo zaidi ya 90, sasa sijui kama ataweza kumaliza zake then aanze kutekeleza yaliyomo kwenye ilani ya CUF, ambayo imeelezea kuwa itatoa elimu bure mpaka chuo kikuu. kazi ipooooo!!!!!!!!!!

hivi huwa mnajifanyisha au akili zenu zimeishia hapo? naona hili pia kwa slaa, kudanganya mchana kweupee.
 
Miongoni mwa hayo majimbo saba ni majimbo ya wilaya ya kinondoni. Ina maana yatokeo ya hayo majimbo yakitoka yataweka kapuni au sio au wata adjust results kimya kimya. Kweli tume ya uchaguzi tunayo. inaachiria walilazimishwa kuwa kwa namna yoyote ile lazima rais aapishwe leo.

Ni aibu majimbo yapo kwenye mkoa yalipo makao makuu ya tume na bado matokeo yanashindikana kupatikana
 
Back
Top Bottom