Duh, hadi watoto wanaanza kutetea haki zao, wausambaratisha msafara wa DC Kahama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Duh, hadi watoto wanaanza kutetea haki zao, wausambaratisha msafara wa DC Kahama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Mar 24, 2012.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Wanafunzi huko Kahama wasambaratisha msafara wa DC wakidai haki zao!
  Na Shija Felician wa Mwananchi - Friday, 23 March 2012

  MSAFARA wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kahama, ukiongozwa na Mkuu wa wilaya, Meja mstaafu Bahati Matala na Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU), umelazimika kutimua mbio kutafuta hifadhi kwenye mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu, baada ya wanafunzi wa Sekondari ya Bulyanhulu kuwashambulia kwa mawe.

  Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Onesmo Lyanga, alisema tukio lililotokea juzi asubuhi eneo la Kata ya Bulyanhulu wilayani Kahama, baada ya wanafunzi hao kuzuia barabara itokayo Kahama kwenda Kakola wakishinikiza walimu wao kurudishwa shuleni.

  Lyanga alisema kabla ya maandamano hayo, Kamati ya Maendeleo ya Kata hiyo (WDC) ilifika shuleni hapo na kufanya kikao kilichopitisha uamuzi wa kuwafukuza walimu wa sekondari hiyo, hali iliyopingwa na wanafunzi walioanzisha maandamano na kufunga barabara, huku wakifanya baadhi ya shughuli ndani ya mgodi kusimama.

  Katika vurugu hizo, Lyanga alisema polisi wawili walijeruhiwa kwa mawe hali ambayo iliwafanya kuongeza askari wengine kutoka kituo cha wilaya, waliokwenda kudhibiti vurugu usiku na kwamba, hawakutaka kutumia nguvu kubwa kutokana na waandamanaji wengi wao ni watoto.

  Hata hivyo, Meja Matala kabla ya msafara wake kushambuliwa alisema lengo lilikuwa kufanya mazungumzo na wanafunzi hao kusikiliza malalamiko yao, kisha kumaliza tatizo hilo ambalo chanzo chake ni kutofuata taratibu za mapendekezo ya kuwakataa walimu.

  Meja Matala alisema mazungumzo hayo yalishindikana juzi baada ya vurugu hizo, badala yake, yalifanyika jana asubuhi na kuonya Kamati ya Maendeleo ya Kata, kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kufukuza walimu kwa sababu haina mamlaka hayo.

  Alisema WDC haina mamlaka ya kufukuza kazi walimu, bali inaweza kutoa mapendekezo na kwamba, imekuwa chanzo cha mgogoro huo uliosababisha vurugu kubwa.

  Matala alisema jana hali ilikuwa shwari baada ya kufanya mazungumzo na kuwapa taratibu za kupeleka madai yao kisheria, wanafunzi hao walielewa na kusitisha maandamano yao, ingawa polisi walikuwa tayari wamefika kuongeza nguvu kwa wenzao waliozidiwa na kutimkia mgodini.
   
 2. h

  hans79 JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Shagara bagara,maajabu ya tz kila mwananchi kujitafutia mwenyewe utaratibu wa kumaliza limkabirilo.Tulipo pa baya hapana muda wala saa wakati wo wote nchi kuingia kwenye machafuko kubwa kama Libya na kwingineko,hatuna viongozi bali tu na watawala ambao wamevaa miwani za mbao.Lakin ipo siku ya kutoka hapa tulipo na kuwa nchi yenye heshima duniani.
   
 3. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Eti Kamati ya Maendeleo ya Kata yaweza kujichukulia sheria mkononi na kuwafukuza waalimu, CCM bwana! Kwa mbali nawashuku wajumbe wa kamati hii, si ajabu ni hao hao wazazi aina ya wale wa Arumeru wanaopigiwa mayowe na vijana wao. Kwa mtindo huu ukombozi hauko mbali, heko kwa wote wanaofanya jitihada ya kuwaamsha wananchi kutambua haki zao.
   
 4. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,015
  Likes Received: 2,669
  Trophy Points: 280
  Hii nchi haina taratibu za kufuata sheria,kila mtu anajiamulia anavyotaka, na yote hii imesababishwa na serikali legelege ya sisiemu.
   
 5. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  WDC imekurupika!!
   
 6. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mkuu wa wilaya kahama hajui kazi yake yeye ni kukulupuka tu
   
 7. Sorrow to Joy

  Sorrow to Joy JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 293
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huyo diwani ambaye ni mwenyekiti wa WDC ana elimu gani? Wamegombea capitation na walimu. Pumbaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaavuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
   
Loading...