Kabisa..Ethiopia bana... ila upande wa Kenya wamekwenda poa, barabara shwari, kero ni vuzuizi vya mapolisi ila wamefurahi...napenda sana hitchhiking, yaani hunipa raha sana.
Anyway tuendelee kukomaa, tutafika, sisi ni mashujaa!!
Ieleweke lakinni kwamba upande wa Ethiopia, bara bara bado inajengwa. Tumepiga hatua kama Africa lakini bado tuna changamoto kibao sana!
Usiseme Africa, Sema Kenya bado sana,
Nashangaa 2019 bado hamjafungua hiyo Boarder, Huo ndio uvivu wenyewe.
Vipi Tandale bado supu ya Pweza inauzwa tu??
Africa au Kenya?...
Ieleweke lakinni kwamba upande wa Ethiopia, bara bara bado inajengwa. Tumepiga hatua kama Africa lakini bado tuna changamoto kibao sana!
Kama nchi gani izo?Africa au Kenya?...
Zipo nchi upande wa barabara wanafanya vizur at wamefanya vizur na hawapigi kelele
Angalia hyo video vizuri halafu ucheki barabara kutoka moyale hadi nairobi...kilichowakwaza ni mziki na hko kusimamishwa na polisi tu...Africa au Kenya?...
Zipo nchi upande wa barabara wanafanya vizur at wamefanya vizur na hawapigi kelele
Kafrican,
Afrika gani unayosema? Labda nchi wanachama wa IGAD .
Lakini nchi za SADC Unaweza kuendesha gari kupitia barabara za lami toka Namanga au Bukoba Tanzania mpaka Cape Town. Pia unaweza kusafiri kwa reli toka Dar es Salaam mpaka Cape Town kwa njia ya reli moja kwa moja siyo tu Afrika ya Kusini bali hata Benguela Angola ktk pwani ya bahari ya Atlantic.
Afrika ya matatizo ya nchi wanachama wa IGAD inayojumuisha nchi za Kenya, Ethiopia, Eritrea, Somalia, the Sudan, South Sudan na Uganda ndiyo kuna matatizo makubwa ya miundombinu / miundomsingi ya barabara na reli.
Africa au Kenya?...
Zipo nchi upande wa barabara wanafanya vizur at wamefanya vizur na hawapigi kelele
Utakua hujatazama video, unajibu kwa kusoma comments, wacha uvivu itazame, lini umeskia hatujafungua mpaka na Ethiopia, pia humo kwenye video inaonyesha barabara upande wa Ethiopia ni majanga, mwandishi amelalamika tangu alipotoka Addis, ila baada ya kuvuka mpaka akawa anatiririka bila matatizo, sema kulikua na vizuizi vingi vya polisi upande wa Kenya, ambalo ni jambo la kueleweka maana raia wengi wa Ethiopia huitoroka nchi.
Vipi Tandale bado supu ya Pweza inauzwa tu??
Wakenya wenzako wakishangaa Barabara za tz kuelekea tanga, ukizingatia tz inamikoa mingi kuliko Kenya na imepakana na nchi nyingi kuliko Kenya na mikubwa kuliko Kenya ila barabara ni safi mkeka wa kupendeza
Ieleweke lakinni kwamba upande wa Ethiopia, bara bara bado inajengwa. Tumepiga hatua kama Africa lakini bado tuna changamoto kibao sana!
Tanzania Tunapakanana Nchi Nane, yaani Kenya, UG, DRC, RW, BU, Malawi , Zambia na Mozambique,
Na zote hizi tumeziunganisha kwa Barabara Safi,
Yaani Utatoka DSM kwenda, Lusaka, Blantyre au Lilongwe, Utatoka Dar Kwenda Pemba hadi Nampula au Kwenda Kigali hadi Bujumbura Kote huko Lami swafi,
Na kwa upande wa Kenya ndio usiseme, Uamue tu kupitia Namanga au Holoholo/Lungalunga, au Tarakea,
Vipi kuhusu Kenya -Sudan-Somalia-Ethiopia???
Barabara zote hizo na kainchi ketu kadogo tunawazidi kwenye urefu wa paved roads kwa maelfu ya kilometers, hivi huwa mnakwama wapi kwa kweli, ni uvivu uliopitiliza.
Anyway, sisi jukumu letu linaishia kwenye kutengeneza barabara hadi mpakani, huko kwengine ni kazi ya Ethiopia kujua wanaanzaje.
Sasa hivi tumeanza kutumia ardhi ya Tanzania kufikia hayo mataifa ya huko kupitia Voi-Taveta-Singida-Kobero