Dudu Baya kuna siku atawageuzia kibao Wasafi

sonofobia

JF-Expert Member
Jun 21, 2015
368
2,511
Kuna msemo wa kiswahili unasema ukifuga chatu uwe na unga wa kumlisha, kwa maana ukiishiwa unga atakugeuza wewe ndio msosi wake.

Hii ni sawa na team ya Wasafi wanavyomuendekeza Dudu Baya aka Konki masta.

Kwa sasa Dudubaya amekuwa msema hovyo kupitia page yake ya Instagram na kwa sababu anasema yanayowapendeza Wasafi basi wameamua kumuendekeza na kumpa platform ya ku-shine.

Lakini niwataadharishe tu Wasafi ipo siku Dudu Baya atawageuzia kibao sababu ukimtazama kwa makini anapozungumza na vitu anavyozungumza unaona kabisa huyu mtu ana shida kichwani. Yani kwa kifupi Dudu baya kwa sasa afya ya akili yake Ina mushkeli.

Anaweza kuwa anaongea mengi yenye ukweli lakini kusema ukweli pekee akutoshi kuonesha uzima wa akili yake, maumivu na kutotendewa haki kwenye muziki wamefanyiwa wengi sana tena waliofanya makubwa kwenye muziki lakini watu wameanguka wakasimama na maisha yanaendelea, kina P Funk Majani wamefanya kila kitu kwenye muziki lakini walilizwa na wadau ila wakachagua busara zaidi maisha yanaendelea.

Dudu baya ni mtu anayeonekana ana hasira, amechanganyikiwa na ana msongo wa mawazo asiyejua kesho yake inakuwaje.

Nawashauri Wasafi kaeni mbali na Dudu Baya, au msaidieni aende rehab akatibiwe.
 
Wasafi mda wote wanapigwa wimbo wake,miaka 20 kwingine nyimbo zake hazijapigwa ,ana haki ya kuwasifu wasafi,hawezi kuwageuzia kibao ndo wanaomfanya asikike sasa hivi,halafu isitoshe pamoja na konyagi zake mengi anayoongea kuna ukweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmh bila shaka wewe mtoa uzi ni team clouds, konk Masta anongea ukweli mtuangu kama umeanza muda mrefu kumfuatilia utajua jamaa ni mwanaharakati kama ilivyokua kwa kina 2pac

Siyo siri jamaa kuna vitu akiongea mm mwenyewe ananigusa,

Dudu masta nakuomba endeleza harakati mzee wangu wasanii wamenyonywa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi hii siku hizi kumekuwa na watwana na watumwa.

Kila mtu mwenye ufuasi kidogo na vipesa katengeneza kundi lake la misukule, inachofanya ni kumsifu na kumwabudu tu.

- Domo ana ya kwake

- Magufuli ana ya kwake

- Mbowe ana ya kwake

- Bashite ana ya kwake.

- Kiba naye ana ya kwake

Na hao wamiliki wa misukule ni jambo la kila mmoja kuitumia awezavyo kumwongezea UTAJIRI.

SIKU ZOTE Kwa Misukule Hao Watwana Wao Ni PERFECTIONISTS. Ni WATU TIMILIFU hawakosei. NI MIUNGU WATU.
 
Dudu mbaya ni mkweli Kama unachukia vitu anavyoongea na wewe fungua page yako andika unachopenda
 
  • Thanks
Reactions: THT
mimi namkubari mzee chid Benz jamaa ana busara kinoma yule
 
  • Thanks
Reactions: THT
Anaswaga yake mwenyewe anasemaga"we live your life" anamaanishaga Nini?mi simuelewagi mamba Aisee 😁😁
 
Back
Top Bottom