Dubai: Rais Samia ahudhuria Siku Maalum ya Tanzania (Tanzania Day) ya maonyesho makubwa ya Kimataifa ya Biashara na Uwekezaji ya Dubai Expo 2020

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Leo Jumamosi Februari 26, 2022 huko Dubai kwenye maonyesho makubwa ya Kimataifa ya Biashara na Uwekezaji ya Dubai Expo 2020 ni Siku Maalum ya Tanzania (Tanzania Day) kuonyesha fursa zake za uwekezaji, biashara, utalii n.k. ambapo Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa Mgeni rasmi leo Jumamosi akiongoza Taifa letu kwenye maonyesho hayo makubwa kabisa kuieleza Dunia fursa za uwekezaji na biashara zilizopo nchini.

Nchi zote 192 zilizopo kwenye maonyesho hayo pamoja na Wafanyabiashara na Wawekezaji wote wakubwa watakuwa Wageni wa Tanzania na kuelezwa kwa undani kila fursa ya Uwekezaji na kufanya biashara iliyopo Tanzania na kuwavuta waje kuwekeza nchini. Ni siku kubwa kwa nchi yetu na yenye maana kubwa sana kwa uchumi na maendeleo ya Taifa letu.

Bwanku M Bwanku
bwanku55@gmail.com

352d2b573a7444c1b1ccb55496fd6b01.jpg

FB_IMG_1645728710829.jpg
 
Kwenye maonesho makubwa ya kimataifa nchi zote zinazoshiriki hupangiwa siku yao, hilo hata hapa maonesho ya Sabasaba hufanyika hilo.
 
Tz imepoteza nafasi hii ambayo ushirikiwa wake ni BURE.

Nadhani kuna baadhi itawashangaza. Ni hizi ushiriki wake ni BURE. Itakugharimu tiketi chakula na malazi ambapo zipo hotel gharama zake ni kama gharama za hotel za kawaida dar.

Taasisi zilizopewa mamlaka ya kusimamia sekta hii wametuangusha sana sana. Na walipaswa kuwajibika. Nazifahamu lakini sipendi kuzitaja. The Dar Bulls.

Binafsi nimepata taarifa siku 15 zilizopita. Lkn baada ya kuanza kufatilia viza nikaambiwa nilipaswa kuaply siku 14 kabla. Hivyo Jana yake ndio ilikuwa deadline.

Maonyesho haya huchukua miezi 6. Na kila wiki huwa ni siku ya nchi fulani.
Maonyesho haya hufanyika kila baada ya miaka 5
 
No serious investor anapatikana kwenye matukio kama hayo.

Tutaishia kupata madalali tu.
Serious investors wana njia zao za kupata taarifa ya wapi ni salama kuwekeza na sio kwenye Maonesho ya biashara!!
Huko kwenye EXPOS nchi huenda kutafuta masoko ya bidhaa zao na hata hivyo siku hizi marketing kubwa duniani hufanywa kwa mitandao, hivyo watu wetu wasitupotezee fedha zetu kutudanganya kuwa wanakwenda kutafuta wawekezaji kwenye maonesho!!
Mnapo wasingizia wapinzani wenu wa kisiasa kuwa ni magaidi mjue mnawafukuza watu kuja kuwekeza nchini, wawekezaji hawawekezi kwenye nchi isiyo kuwa stable!
 
Tz imepoteza nafasi hii ambayo ushirikiwa wake ni BURE.

Nadhani kuna baadhi itawashangaza. Ni hizi ushiriki wake ni BURE. Itakugharimu tiketi chakula na malazi ambapo zipo hotel gharama zake ni kama gharama za hotel za kawaida dar.

Taasisi zilizopewa mamlaka ya kusimamia sekta hii wametuangusha sana sana. Na walipaswa kuwajibika. Nazifahamu lakini sipendi kuzitaja. The Dar Bulls.

Binafsi nimepata taarifa siku 15 zilizopita. Lkn baada ya kuanza kufatilia viza nikaambiwa nilipaswa kuaply siku 14 kabla. Hivyo Jana yake ndio ilikuwa deadline.

Maonyesho haya huchukua miezi 6. Na kila wiki huwa ni siku ya nchi fulani.
Maonyesho haya hufanyika kila baada ya miaka 5
Mlaka 5 duu kama kombe la dunia
 
Hii ningetemea zaidi wajae wafanyabiashara na Mawaziri..., Hizo pesa za Kumpeleka Rais bora wangeongezea namba za wafanyabiashara... Yaani hio ndege wajaze wauza vinyago n.k.
 
Tz imepoteza nafasi hii ambayo ushirikiwa wake ni BURE.

Nadhani kuna baadhi itawashangaza. Ni hizi ushiriki wake ni BURE. Itakugharimu tiketi chakula na malazi ambapo zipo hotel gharama zake ni kama gharama za hotel za kawaida dar.

Taasisi zilizopewa mamlaka ya kusimamia sekta hii wametuangusha sana sana. Na walipaswa kuwajibika. Nazifahamu lakini sipendi kuzitaja. The Dar Bulls.

Binafsi nimepata taarifa siku 15 zilizopita. Lkn baada ya kuanza kufatilia viza nikaambiwa nilipaswa kuaply siku 14 kabla. Hivyo Jana yake ndio ilikuwa deadline.

Maonyesho haya huchukua miezi 6. Na kila wiki huwa ni siku ya nchi fulani.
Maonyesho haya hufanyika kila baada ya miaka 5
Kuto taja bado umeonyesha udhaifu ule ule wa mtanzania halisi.. yaan huitaj kulaum mtu... Wew kutaja tu umeshindwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na muwaambie kwa ujinga wetu maembe na machungwa huwa yanarundikwa barabarani na kuwa kama mlima Hanang na kuoza bila wateja

Fursa gani wameenda kununua suti tu
 
No serious investor anapatikana kwenye matukio kama hayo.

Tutaishia kupata madalali tu.
Madalali ni kila kitu ktk ulimwengu wa teknilogia. Wanahamasisha na kusisimua uchumi.

Amazon, alibaba ni miongoni mwa madalali
 
No serious investor anapatikana kwenye matukio kama hayo.

Tutaishia kupata madalali tu.

seeious investors anapatikana wapi?...

hizi expo za kimataifa kwa taarifa yako, matajiri wenye mitaji ndio sehemu zao za kupata information na kutengeneza network worldwide.. Dubai expo ni moja ya expo kubwa sana duniani, nyingine ni Mining Indaba na Bauma ya Europe na America..
 
Kwa hiyo naomba kuuliza, hayo maonyesho yanatumia muda gani (kwetu Sabasaba huwa ni kama siku 10 hivi) kiasi kwamba kila nchi inakuwa na siku yake? Au hiyo Tz imependelewa tu katika maonyesha ya mwaka huu? Na pana uwezkano na sisi mwaka huu kwenye Sabasaba tutakuwa na Dubai day ili 'kurudisha' ukarimu?

Je, jana ilikuwa siku ya nchi gani na kesho itakuwa ipi ....Kenya Day au Uingereza day au Madagascar day, Brazil day nk?

Ni hayo tu
 
seeious investors anapatikana wapi?...

hizi expo za kimataifa kwa taarifa yako, matajiri wenye mitaji ndio sehemu zao za kupata information na kutengeneza network worldwide.. Dubai expo ni moja ya expo kubwa sana duniani, nyingine ni Mining Indaba na Bauma ya Europe na America..
Acha uongo investor hasubiri mpaka raisi aende Dubai expo ili aje kuwekeza. Hizo ni sehemu za kwenda kula bata tu
Ni sawa na useme investor anapatikana sabasaba
 
Back
Top Bottom