ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,543
Goli 4-0 ni kipigo kikubwa kwa timu iliyo kwenye hatari ya kushuka zaidi. Nimeifuatilia kwa karibu klabu hii hivi karibuni tangu alivyotua ndugu yetu pale, na nilichokigundua kuna tatizo katika idara za ulinzi na hata viungo, pia kocha naye inambidi awe mbunifu wa kubadili mifumo ya uchezaji kwa maana ya formation. Yawezekana mapungufu hayo yameigharimu timu kwa kipindi kirefu mpaka timu kufikia hapo ilipo.
Samatta anasimama kati mbele peke yake, mipira haimfikii viungo wamekuwa na umahiri mdogo wa kumiliki mpira, hawako sharp kuigawa kwa wenzao na kusonga mbele badala yake mtu anataka kukimbia mita 10 na mpira peke yake mwisho wake adui wanaupata kirahisi na wakianza kushambulia goli wanakutana na beki isiyoweza kujipanga vizuri au iliyochoshwa na mipira mingi inayorudi mara kwa mara.
Tuwaombee timu yetu hii ili angalau wasalie EPL msimu ujao maana kibaya zaidi game zilizosalia ni ngumu mno.
Mungu ibariki Aston Villa.
Sent using Jamii Forums mobile app