Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 17,415
- 21,110
Kuelekea pambano la 50 tangu aanze kucheza ngumi za kulipwa akitokea kule kwenye ngumi za ridhaa, namuombea sana mwanangu Floyd Mayweather aibuke kidedea kwenye pambano lake dhidi ya Conor McGregor litakalo fanyika T mobile arena Las Vegas.
Pambano hili litakuwa la mwisho kwa Floyd na ameshakula kiapo juu ya suala hili, ingawaje si mara ya kwanza kusema hivi kwa kuwa hata pambano lake dhidi ya Andre Berto alisema hivi hivi lakini hakusimamia msimamo wake.
Nahofia asije akapoteza aisee maana McGregor ni bondia mdogo sana, Floyd akipigwa itakuwa bonge la aibu kiasi kwamba mashabiki wake tunaweza tukafa kwa mshtuko, pia itamuharibia sifa yake iiyodumu kwa miongo miwili sasa.
Pia nahofia asije akapata usumbufu kama alioupata kwenye pambano lake dhidi ya Miguel Cotto lilimsababishia kutokwa damu kwa siku kadhaa.
Huyu Conor hata akipigwa hana cha kupoteza kwa kuwa ameshapigwa sana hapo awali.
Nahofia Floyd atajilinda sana ili asipigwe katika pambano hili, ila ubaya nahofia wasije wakamaliza sare au akampiga kwa points chache sana.
Conor anaonekana akijiamini sana katika pambano hili ingawaje ni bondia mbovu sana, lakini kwa upande wa Floyd amekuwa mara kwa mara akisema anaona kama pambano hili ataenda kupoteza kwa mara ya kwanza.
Kauli hii ya kupoteza inatupa simanzi sana mashabiki wake wa damu hasa mimi, nitaumia sana kama mdogo wangu Floyd atapoteza pambano hili.
Dua zangu za dhati ziende kwa undefeated world champion Floyd Joy Mayweather Jr a. k. a The Pretty Boy aweze kushinda kwa kishindo katika pambano lake litakalo chezwa usiku wa kuamkia jumapili