Uchaguzi 2020 Dua ya Askofu Mwamakula: Atakayehusika na kudhulumu uchaguzi afedheheshwe yeye hadi kizazi chake cha nne!

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,487
51,064
Kama watumishi wa NEC, TISS, Wakurugenzi, Watawala, Wasimamizi wa vituo na mtu yeyote anayehusika na uchaguzi wanataka waendelee kuishi kwa baraka katika maisha yao, basi wajichunge sana namna watakavyoendesha na kusimamia uchaguzi huu.

Wawe makini kwa sababu kuna dua nzito sana imeombwa na Askofu Mwamakula, Dua ya mtu yeyote yule atakayehusika kuiba haki katika uchaguzi huu ya kufedheheshwa hapahapa duniani yeye mwenyewe hadi kizazi chake cha nne.

Sasa nyie Watawala, watumishi wa NEC, TISS, Wakurugenzi, Wakuu wa vyombo vya usalama fahamuni kuwa baada ya uchaguzi kuna maisha yenu binafsi, kunamaisha ya familia zenu. Hao watawala mnaowapigania watapita lakini Jueni kuwa kuna Dua ya Laana iko juu yenu mkivuruga uchaguzi huu.

Nyie mna watoto, au wajukuu, mtapata vitukuu n. k itawasaidia nini mtie uzao wenu laana eti kwa sababu ya ajira ya leo au posho ya leo?

Rais Magufuli, Jaji Kaijage, Jaji Mihayo, Diwani Athumani, Simon Sirro, Mkuu wa Majeshi Mabeyo na wooote ambao wanapokea amri zao hadi huko kwa wasimamizi wa vituo vya kura. Mko tayari nyinyi hii Dua ya kuwapatilizeni nyie hadi uzao wenu wa nne iwatafune?

Basi watendeeni haki Watanzania la sivyo msije mkafanywa dhalili katika dunia hii, mkawa na vizazi vilivyolaaniwa sababu tu ya kutowatendea haki watanzania!

Kuna maisha baada ya uchaguzi huu, kumbukeni hilo
 
Biblia husema,kabla hujatoa boriti kwenye jicho la mwenzako, basi toa kibanzi kilicho jichoni mwako, Biblia husema tii mamlaka iliyopo maana ina kibali na Mungu,kila mamlaka ina makusudi yake mbele ya Mungu, hivyo yeye kama askofu hana mamlaka ya kushindana na Mungu, yeye ni binadamu tu
 
Biblia husema,kabla hujatoa boriti kwenye jicho la mwenzako,basi toa kibanzi kilicho jichoni mwako,Biblia husema tii mamlaka iliyopo maana ina kibali na Mungu,kila mamlaka ina makusudi yake mbele ya Mungu ,hivyo yeye kama askofu hana mamlaka ya kushindana na Mungu,yeye ni binadamu tu
Ndio matokeo ya kureply kabla hujasoma thread,hivi umeelewa mada inasema nini?,kwani askofu hajatii mamlaka?,kwani askofu amekana kwamba mamlaka hazina vibali?,
 
Hawa maaskofu wengine! Ina maana hao TISS, NEC na wakurugenzi wanauwezo kuzuia MAPENZI ya Mungu? Mungu anamjua na atatupa RAIS tunayemhitaji. Ikiwa watanzania tumejaa ujinga kiasi cha kutomjua RAIS anayetustahili, basi kwa jinsi anavyoipenda Tanzania atawatumia hata TISS, NEC na Wakurugenzi kutupatia yule ALIYEMTEUA YEYE. Mungu asipopenda kutupatia RAIS kibaraka, hata tumpende vipi, ATATUEPUSHA NAYE. Kwa sababu anaipenda Tanzania kuliko huyu Askofu anavyompenda anayempenda. Askofu huyu ajue - Kuna MAISHA baada ya Uchaguzi. Asije akajikuta anafedheheshwa yeye. Na atafedheheswa yeye tu bila kizazi chake kuguswa. Maana Mungu tunayemjua ni mtenda haki. Hawezi kufedhehesha kizazi chake kisichohusika na UJINGA wake.
 
Biblia husema,kabla hujatoa boriti kwenye jicho la mwenzako,basi toa kibanzi kilicho jichoni mwako,Biblia husema tii mamlaka iliyopo maana ina kibali na Mungu,kila mamlaka ina makusudi yake mbele ya Mungu ,hivyo yeye kama askofu hana mamlaka ya kushindana na Mungu,yeye ni binadamu tu
Wanaposema Kila mamlaka inatoka kwa Mungu,huwa hawamaanishi Kila mamlaka Ni nzuri.Mamlaka nyingine huwekwa ili iwe funzo kwa wanadamu waliomkosea Mungu ili waweze kutubu.
 
Vizuri..
Pia naskia Kuna ALBADIRI tayari imesomwa🙄

Hapo ni kila mmoja kuchunga HATMA yake na uzao wake. Ukitekeleza maagizo ya kihuni ya watawala, inakula kwako na uzao wako
 
Back
Top Bottom