Uchaguzi 2020 Dua ya Askofu Mwamakula: Atakayehusika na kudhulumu uchaguzi afedheheshwe yeye hadi kizazi chake cha nne!

Kweli maombi yana nguvu, wale wote waliokuwa na nia ovu na nchi yetu wamegaragazwa na kushindwa vibaya ktk uchaguzi huu
 
Kama watumishi wa NEC, TISS, Wakurugenzi, Watawala, Wasimamizi wa vituo na mtu yeyote anayehusika na uchaguzi wanataka waendelee kuishi kwa baraka katika maisha yao, basi wajichunge sana namna watakavyoendesha na kusimamia uchaguzi huu.

Wawe makini kwa sababu kuna dua nzito sana imeombwa na Askofu Mwamakula, Dua ya mtu yeyote yule atakayehusika kuiba haki katika uchaguzi huu ya kufedheheshwa hapahapa duniani yeye mwenyewe hadi kizazi chake cha nne.

Sasa nyie Watawala, watumishi wa NEC, TISS, Wakurugenzi, Wakuu wa vyombo vya usalama fahamuni kuwa baada ya uchaguzi kuna maisha yenu binafsi, kunamaisha ya familia zenu. Hao watawala mnaowapigania watapita lakini Jueni kuwa kuna Dua ya Laana iko juu yenu mkivuruga uchaguzi huu.

Nyie mna watoto, au wajukuu, mtapata vitukuu n. k itawasaidia nini mtie uzao wenu laana eti kwa sababu ya ajira ya leo au posho ya leo?

Rais Magufuli, Jaji Kaijage, Jaji Mihayo, Diwani Athumani, Simon Sirro, Mkuu wa Majeshi Mabeyo na wooote ambao wanapokea amri zao hadi huko kwa wasimamizi wa vituo vya kura. Mko tayari nyinyi hii Dua ya kuwapatilizeni nyie hadi uzao wenu wa nne iwatafune?

Basi watendeeni haki Watanzania la sivyo msije mkafanywa dhalili katika dunia hii, mkawa na vizazi vilivyolaaniwa sababu tu ya kutowatendea haki watanzania!

Kuna maisha baada ya uchaguzi huu, kumbukeni hilo
Dua la bata
 
Back
Top Bottom