Du! Yaani wa Tanzania hatuna muda tena wa kutumia vizuri ubongo na akili zetu, kwa nini?

milimo

Member
Nov 29, 2012
61
32
Watanzania walio wengi siku hizi wanataka usanii sanii tu(msinielewe
vibaya wale wasanii wa fani-hii ni lugha ya mtaani) ati maandiko
yakiwa marefu kidogo tu humu jf utasikia wachangiaji wanasepa
"ooh nitaruda baadaye, ooh sina muda, ooh acha ngonjera". Leo
nawatolea uvivu. Mnajenga mapokeo gani mabaya kwa wadogo zenu?,
acheni uvivu bwana jaribu kukitumia vizuri kichwa kisiwe kinabeba
nywele tu.

Hasa wewe unaependa kupiga porojo kijiweni bila hata kujua ulimwengu
unaendaje kwa kusoma maandiko. Ukiangalia tv wewe ni tamthilia tu,
tamthilia ni maigizo yaliyokolezwa uwongo, ndio maana utakuta kijana
anafanya mambo ya ajabu ajabu ati anaiga ulaya wakati hata mguu
wake haujagusa huko. Wazungu wangekua hivyo unafikiri wangendelea,
thubutu!!!!.

Lazima niwe mkali kwa sababu inauma sana, utasikia kijana wa ki tz hataki
kusunbua kichwa chake, mfano, kuna mada humu jf huwa zinajenga sana
lkn ikiwa ndefu tu utaona vijana wavivu wanaanza kusema, ‘eh unatuchosha,
andika kwa kifupi, hatutaki ngonjera n.k',watanzania wanataka vitu rahisi rahisi tu,
kisa hatuna muda, lkn ukiangalia ubize wenyewe huoni, mara utaona mchana
kutwa anashinda kwenye komputa kuangalia vitu vya ajabu ajabu, akitoka
kazini anaenda vijiweni kuongea mambo yale yale ya siku zote, simaanishi
kwamba usijichanganye la hasha ila ujue kwamba chanzo kikubwa cha maarifa
ni kwenye maandishi, na wala sio maandishi rahisi rahisi tu hapana lazima kichwa
au ubongo vifanye kazi ile inayokidhi haja ya uwepo wake, na unapoenda kijiweni
uwe na kitu kipya cha kuongea na wenzako.

Nani kakuambia maendeleo au mambo mazuri yanakuja kwa urahisi rahisi tu.
Ndio maana ufisadi umeshinda uadilifu hapa Tanzania kwa sababu wanaofanya ufisadi
wanachemsha bongo zao kujua mbinu za kuwaibia watz lkn waadilifu wanalaza
bongo na kulalamika tu. Hivi unajua maisha ni mafupi hapa duniani hivyo tunatakiwa
kwa muda wa uhai wetu tudhihirishe uwepo wetu.

Hiyo ilikua trela tu, na wengine tayari wamechoka kusoma ‘hivi ni kweli kwamba mtz
ukitaka kumficha kitu kiweke kwenye maandishi?' Ngoja nianze kuandika nilichokusudia
sasa.

Sichukii chama chochote cha siasa ila nawachukia watanzania (pamoja na mimi mwenyewe
najichukia sababu ni mtanzania pia). Hivi ulitarajia chama tawala wasifie juhudi za vyama
mbadala vishike dola, yaani kwa mawazo yako chama tawala wachekelee pale vyama
mbadala vipopata ungwaji mkono, kama mawazo yako ni hayo pole sana kwa sababu
utachanganyikiwa na kuanza kuchukia kila mtu. Hebu amka timiza wajibu wako.
Sio lazima iwe majukwaani, fanya unachokiweza km kufanya maombi, kuelimisha
wale uliokaribu nao, kutimiza majukumu yako ikiwa ni pamoja na kupiga na kuhamasisisha
watu kupiga kura.

Vijana hii ni nafisi yenu (simaanishi vijana wa umri ila wa kimtazamo, maana wazee
wengine wanafagilia mabadiliko na kuna vijana wanawaza kama wazee). Hapa tulipofikia
tunahitaji mabadiliko, nani kakuambia chakula kilichochacha kikiwekwa kwenye chungu
kizuri kitakua kitamu? Tumia akili yako vizuri mtz wewe.

Utasikia waoga wa mabadiliko wanasema hata chama kingine kikishika dola mambo
yatakua yale yale tu, nani kakuambia wanaongoza hivyo vyama ni malaika, si umesikia
maneno ya baadhi yao baada ya kupata umaarufu tu wameanza kusema wao ni
mwarobaini wa umaarufu wa hivyo vyama vyao, utasikia ati yeye na mwenyekiti ndio
wamekifikisha chama hapo kililpo, wanasahaua kujua ukweli kwamba kuna watz hawana
nafasi ya majukwaa ya kisiasa lkn muda wote wanaomba kwa Mungu ili mabadiliko ya
kweli yaje na Mungu anajibu kwa njia moja au nyingine, hivi hawajui kwamba kuna watz
wanavitangaza hivyo vyama nyumba kwa nyumba bila hata kuwa wanachama.
Umaarufu kidogo tu keleleee, hata wananza kutoa kejeli kwa wakubwa wao. Naomba
mnaongoza vyama mjua kwamba umaarufu wa chama unatokana na maombi ya watz
na Mungu huchagua kuwatumia wachache wasimame kuwa viongozi kwa niaba ya
wengine, hivi wote tungetaka tuwe viongozi kwenye chama hivi hii nchi ingekua na
amani? Ingekua busara sifa zitoke kwa wanokutazama na wala sio ujikweze mwenyewe.

Kinachoniuma sana ni pale ninaposikiliza hata wasomi wa tz wanaposema hata chama
kingine kikija mambo yatakua yale yale, kwa mtazamo wa mtu asiyetaka kutumia akili
yake vizuri ni kweli. Hebu nikuambie, kinachotafutwa na watz sio chama gani kizuri ila
namna gani madaraka ya kuiajiri serikali yawe mikononi mwao (na wajue hivyo) na pale
wasipotimiziwa matakwa yao kama waajiri waweke chama kingine. Na hata hicho kingine,
mfano, chadema au cuf au nccr n.k kikishika dola na baadaye kisipotenda yale kilichotuahidi,
tuwe na utashi na uwezo wa kukishikishe adabu kwa kukinyima kura .

Hapo kutakua na adabu kwa chama chochote tawala kwa kutenda yale yaliyo na manufaa
kwa mwajiri(wananchi). Kwani si mnajua wenye kampuni wanapomwajiri mkurugenzi wanataka
afanye kazi kwa maslahi yao ( kuzalisha faida kama ni kampuni ya biashara) na kama hajatimiza
bila sababu za msingi hufukuzwa kwenye ajira ( mfano huu, watz ni wenyewe kampuni na
wakurugenzi ni serikili iliyoko madarakani).

Hapa nieleze vizuri; janja ya mkurugenzi akishindwa kutekeleza matakwa ya mwajiri lazima
afanye mambo ya aja ajabu ili waliomwajri wasijue udhaifu wake haraka, ataanza kujipendekeza
kwa wakaguzi wa kampuni ili wasiandike ripoti mbaya hata kufikia kuwapa hongo (tunashuhudia
rushwa za uchaguzi).

Kuwagawa wamiliki kwa njia za hila ili apate kuungwa mkono na baadhi (tunashuhudia
propaganda za udini na ukabila), kujikusanyia mali nyingi isivyo halali –vikao vingi, kusafiri
kwingi kwa ajili ya masurufu (tunashudia ufisadi wa kutisha), kujenga uraki wa mashaka na
wale wenye uhusiano wa kiabiashara na kampuni ili achukue fedha isivyo halali na kizificha
kwao (tunashuhudia jinsi kampuni zinavyoibuka/na zingine kufufuliwa lkn uwazi wa chanzo
cha mitaji hakuna), kuhujumu kampuni kwa makusudi ili akifukuzwa wamiliki wapate shida
( tunashuhudia jinsi fedha zinavyofichwa nje ya nchi huku watz wakifa kwa kukosa huduma
za tiba, wakilala njaa, wakikosa ajira kwa sababu fedha zimetoka nje ya mzunguko wa
kutoa ajira).

Ngoja nikuambie, usiwe mwoga sana kwa sababu hakuna aliye juu ya Mungu wetu
aliye Mbinguni, hivyo usimtegemee wala kumwogopa sana binadamu, huyo binadamu
unayemtegemea au kumwogopa sana, leo yupo kesho hayupo lakini Muumba wetu wa
Mbinguni ni wa milele, Mungu akisema hutapata madhara au hutakufa mpaka utimize
malengo fulani, amini amini hufi hadi hapo yeye atataka upumzike milele (si umeona
huyu mnyambala nanii... Kama kweli alitegeshewa sumu hatari na hajafa, anadunda tu
na anaendelea kuwahudumia watz). Badilika, tetea watz wenzio kwa namna yeyote ile.

Tatizo lipo hivi; kuna watu wakikaa muda mrefu sehemu fulani wanajiona wao
ndio wenye haki miliki ya nahali pale. Angalia ccm ilivyo kwa sasa bila kuwa na
mtu wa kukupigia debe(baba,mama, mjomba, shangazi, binamu, jirani au rafiki wa
hao niliowataja) huna nafasi hata kama wewe ni mahiri kiasi gani(hasa hasa kama
ni mkweli). Na hicho ndicho kinachowachosha watu wengine. Wengi wako humo kwa
sababu ya maslahi na uwoga tu.

Woga unajidhihirisha unavyowasikia na kuwaona hata viongozi waliokuwa waandamizi
na hata ambao wako ndani ya mfumo wanavyolalamikia mambo yanavyokwenda, hawana
lolote hao ni waoga tu, wanadhani nje ya chama tawala cha sasa hakuna maisha, badilika
acha kulalama lalama kama kweli ni mzalendo.

Baba wa taifa (r.i.p) mwenyewe alisema ccm sio mama yake, maanake angekuwa hai leo
isingekuwa ndani ya ccm (hili liko wazi kabisa sababu hata viongozi wa chama wenye uwezo
na mamlakaya kufanya mamuzi wanalalamika). Kwa hali hiyo, muda sasa umefika wa
kufanya mabadiliko ili watoke nje wakatafakari na wakajipange upya.

Hapo juu nimesema hata vyama mbadala viongozi wake sio malaika, hivyo wanamapungufu
yao. Wengine wako kwenye vyama mbadala lakini mawazo yao, wasiri wao, mienendo yao,
majigambo yao wanachukua toka chama tawala. Si umewakia miongoni mwao wanavyosema
ati chadema kisingekua maarufu bila ya yeye(wao) na m/kiti. Wanasahau kwamba kinachofanya
chama kiwe maarufu inatokana na udhaifu wa chama kinachotawala na hivyo maombi mengi
ya waja wake Mungu yanaelekezwa kwenye mabadiliko. Hawa viongozi nawaheshimu sana
kwa sababu ni mahiri na weledi sana, lakini fikra zao ni za ki-ccm sijui kwa nini,sijui washauri
wao ni akina nani. Najua wamepotoka kidogo tu watabadilika na w ataonekana wapo pamoja
na wenzao kwenye mapambano ya mabadiliko.

Jamani hakuna aliye mkamilifu, si kila binadamu aliyezaliwa na mwanamke amewahi kufanya
makosa? Muhimu ni kwamba mtu akifanya kosa na akashauriwa kujirekebisha afanya hivyo.
Nieleweke hivi, tatizo sio kutaka ukiranja(urais), inawezekana kweli wana uwezo wa kuwa
viranja wa tz, kinachotakiwa kwa sasa ni namna gani mhitaji wa huo utukufu anashirikiana
na wenziwe kufika hapo bila kuathiri umoja na mshikamano wa chama, nje ya hapo tunaona
kama ni ubinafsi na usaliti, ni wazi kwamba ndani ya chama hicho kuna vijana wengi wenye
uwezo wa kuongoza na pia wanatamani siku moja waje kugombea ukiranja lkn busara inatumika
na wamekua watulivu.

Hivi kila mtu ndani ya chama anayejiona unaweza kuongoza atangaze kugombea ukiranja
umoja ndani ya chama utakuwepo? Muda wa sasa sio kuanza kulumbana nani agombee
ukiranja bali kuimarisha chama. Kila kiongozi akianza kutangaza kugombea chama kitapoteza
mwelekeo.

Namfagilia sana huyu mzee anayetoka kwa wafugaji,sijamsikia hata siku moja kujisifia.
Nani hajui alivyokibeba chadema kwenye uchaguzi wa 2010,angekua mtu wa misifa si
angepasuka kwa masifa, naomba Mungu wetu wa Mbinguni ampe maisha marefu na afya
njema kimwili na kiakili pia kwa sababu hata kama hatakuwa raisi lakini ana mambo mengi
na uwezo mkubwa wa kuitendea nchi hii. Samahani simfugilii huyu mzee kwa hila na wala
hata hanifahamu na sihitaji anifahamu, lkn kusema kweli huu upepo wa mabadiliko uliopo
umerutubishwa na mzee huyu.

Simpigii kampeni ili chadema wamteue kugombea 2015 Mungu akimpa afya njema kwa
sababu naamini kama chama wamejipanga vyema namna ya kumpata mgombea kwa njia
ya uwazi na umakini. Huyu mzee tumwombee afya njema na Mungu amwongezee hekima
na unyenyekevu (low profile).

Kwa sababu ya propaganda tu na ubinafsi baadhi ya watu waliofilika kimtazamo na
maadili wanawatia hofu ndugu zangu waislamu ati kwa sababu ni padri hawezi kuwatendea
haki, sio kweli, nimejaribu sana kumfuatilia maongeze yake pamoja na hoja zake sio mtu
wa kuendekeza udini, anajali sana ustawi wa watz bila kuegemea imani yake. Naomba ndugu
zangu waislamu na wakristo tumpime mtu kwa matendo yake na wala sio kwa hisia tu na
kusikiliza propaganda.

Ni ukweli ulio wazi kwamba chadema wasipotumia vizuri huu mwamko watavuna dhambi.
Watavuna dhambi kwa sababu watz angalau wameweka matumaini kwao (baada ya nccr
1995 na cuf 2005). Wakishindwa kuonyesha bayana kwamba wana nia ya kuleta mageuzi,
ni imani yangu kwamba itachukua muda mrefu wananchi kuamini tena kwamba chama
mbadala kitatawala nchi hii. Hakuna kisingizio cha kuibiwa kura, si mnajua hilo? Kujua tatizo
ndio msingi wa kutatua tatizo,hatutasikia tena tatizo la ‘ooh usalama wa taifa wamechakachua,
ooh polisi wanawabeba n.k'.

Hawa usalama wa taifa kwani wanafurahia ufidi unaoendelea, si tunaishi nao mtaani hawa,
wanapigika kama sisi na wanalalamika kama sisi, ndugu zao wanakosa dawa wakienda
hospili kama sisi, binamu zao wanakula mlo mmoja kama sisi. Nawashauri hao usalama
wa watz na polisi kwamba wasimamie mabadiliko hayo kwa uaminifu mkubwa ili nchi yet
isingie kwenye machafuko, hivi kwa jinsi watz tunavyoishi kwa udugu nyie walinda usalama
mtapata wapi ujasiri wa kuwakandamiza watz wenzenu, si tunakua na nyinyi misikitini na
makanisani, hivi utamwambia nini Muumba wako akikuliza kuhusu kuwatumikia mafisadi badala
ya kutumikia nchi.

Mimi sijui wanajifunza nini kuhusu usalama wa taifa ila nadhaniwanafundishwa
kuwatamikia watz kwa jinsi hiyo ni lazima wawalinde kwa gharama yoyote wanao
simamia ustawi wa watz, for that matter viongozi wanaosimamia rasilimali za nchi
kwa uadilifu, kiongozi amepewa kipaumbele cha ulinzi kwa sababu inaminika kwamba
anasimamia ulinzi wa mali na maisha ya watz wengine kwa ustawi wa nchi na wala
sio yule anayehujumu ustawi wa nchi.

Hapa nasisitiza , karibu wanausalama wote ni waadilifu na weledi isipokua wachache
tu wenye maslahi binafsi na waroho. Huku ndio kulogwa sasa, ati inakuwaje wachache
wanaosaidia uovu wawashinde wengi wenye uchungu na ndugu zao watz, itabidi
nimtafute profesor wangu mmoja tutengeneze theory ya kusapoti hicho kitu na tutafute
evidence za kusapoti (si unajua wazungu wametupumbaza, ati hamna kitu kipya mwafrika
anaweza gundua, yaani yeye ni kukopi tu ya waliyogundua wazungu au akitaka
kufanya kitu lazima kuwe na reference ya kitu kilichofanyika yaani hamna kitu kipya
tena hapa duniani. Lkn mbona mazingira ni tofauti sana na ya kwao). Hebu imarisheni njia ya kushirikiana
hao wanausalama wenye nia njema na nchi hii hata kwa siri, si wapo jamani wenye
uchungu wa kweli na nchi hii, tena ni wengine tu, si hata shule waliyoenda kwa kiwango
chochote wamelipiwa na kodi za wananchi hohehahe, nina amini wadilifu wapo tena wengi
sana. Hata police wazalendo wapo wengi tu, si tunaishi nao mtaani, tunakunywa nao, ni
ndugu zetu, kwani wenyewe hawaoni jamanikwamba njia nzuri ni kumpa madaraka
mwananchi ya kuajari serikali na kuitimua (hire and fire –sijui vizuri kithungu usinicheke).

Kitu kingine kinachokera, ati baba ndani ya nyumba analalamika lalamika kwamba
kwanini watoto wake wanakosa chakula wakati mwenyezi Mungu amempa afya,
akili,madaraka na mamlaka kuongoza familia. Watoto wakilalamika kwamba tunalala
njaa anawashangaa ati kwa nini wanalalamika (nadhani yeye hasikii njaa kwa sababu
akiwa huko baa anapata supu). Kama baba ana shamba si awambie watoto kwamba
shamba liko na andae pembejeo wakalime, sasa unashangaa nini, unataka watoto
wafurahie kushinda njaa.

Siku hizi viongozi ndio wa kwanza kulalamika kuhusu mambo yanavyokwenda hovyo,
hata wale tuliowapa mamlaka na madaraka ya kufanya maamuzi nao wanalalamika.
Imekua nchi ya walalamikaji tu, wewe kiongozi unalalamika unafikiri wananchi watashindwa
kulalamika, kiongozi maana yake tumekuamini uwe mbele yetu utuonyeshe mwelekeo.
Ati wananchi wakilalamika viongozi wanashangaa na kuwabeza, kwa nini kama
kiongozi usiwaelekeze njia maana kazi ya kiongozi ni kuonyesha njia. Kama umeshindwa
kuonyesha njia si upishe wengine watuelekeze njia.

Kila mtu akifanya kila anavyotaka si itakua vurugu. Matokea ya kila mtu kufanya
atakavyo ndio tunaona biashara zinafanyika barabarani bila utaratibu, kwa nini
baada ya uchaguzi mnawatimua wamachinga sehemu wanazofanyia biashara
(barabarani) si mnasema kila mtu afanye kinachomfaa, mnafikiri watu wengi wanajua
sheria?

Maana ya kiongozi ni kuwasikiliza anaowangoza na kuonyesha zilipo fusa kwa ajili ya
ustawi wa maisha ya walio mwamini kuwaongoza. Tatizo zaidi ni kwamba ukiwa kiongozi
tz unajua kila kitu, hawataki ushauri, wanafanya vile wanavyotaka hadi tumefikia hatua
ya wataalamu kukata tamaa, ndio maana wataalamu nao wameamua kuingia kwenye
siasa kwa kasi.

Hivi nani katuloga watz? Tumekua watu wa kutegeana tegeana tu, viongozi wengi
kwenye sehemu za kazi wanaogopa kufanya maamuzi magumu, wanafalsafa wanasema
afadhali kufanya maamuzi mabaya kuliko kutofanya kabisa, bila kufanya maamuzi
utajifunzaje? Inawezekana inatokana na kukatishwa tamaa na namna ya maamuzi
yanavyopokelewa na walio juu yao, lakini mbona hata hao walio juu kabisa wanakua
waoga wa kufana maamuzi. Nadhani tatizo ni kwamba viongozi wanataka kumfurahisha
kila mtu na hivyo kubaki njia panda (vua gamba).

La mwisho kwa leo lkn muhimu sana; naomba watz kwa ujumla wetu na kila mmoja na
dini yake tumwombe mwenyezi Mungu ifikapo 2015 atupe kiongozi(raisi) makini anayejua
kwamba nchi ya tz ina kila aina ya utajiri kwa ustawi wa watz. Ni nguvu kidogo tu
zinahitajika kuamsha uchumi uliolala na kuwaongozi watz kutambua kuwa nguvu zao,
akili zao na maarifa yao ndio msingi wa maisha mazuri.

Hatuhitaji tena kuendlea kuwa omba omba (inakera), hatuhitaji kiongozi anaye lalamika
lalamika (maana anawakatisha tamaa anaowaongoza), tunahitaji kiongozi ambaye ni
mnyenyekevu lakini jasiri wa maamuzi, sio kiongozi anayekimbilia ikulu kwa nguvu yake
mwenyewe na wapambe wake, tunahitaji maombi ili Mungu atupe hekima ya kutambua
hila zinazotumika za kutugawa kwa makusudi kwa kutumia propaganda za udini, ukabila
na ukanda. Tunahitaji kiongozi anayetokana na maombi ya watanzania kwa Mungu wala
sio anayesubiri ndoto zake(mara nyingi unachofikiria kichwani ndicho kinakuja kwenye
ndoto na pia shetani anaweza kupitia kwa njia ya ndoto).

Tuombe kiongozi anayetambua kuwa rushwa itapungua sana kwa kuimarisha huduma
muhimu za umma ( kama elimu na afya) na kuweka matumaini mazuri ya maisha ya
watumishi wa umma waminifu watakapo staafu utumishi na wala sio majigambo ya
majukwaani. Tunaomba Mungu atuondolee woga wa mabadiliko na kuomba kwamba
mabadiliko yaje kwa njia ya amani(maana tukitaka kuondokana na ombwe hili lilipo
lazima tufanye mabadiliko).

Tunaomba Mwenyezi Mungu aibariki tanzania na watu wake, atupe hekima ili mabadiliko
yanayokuja (naamini yanakuja)

yambatane na amani, amina
 
Shauri yako, kuna tangazo la kazi nzuri humo (ukitaka kumficha maarifa mtz yeweke kwenye maandishi)
 
kamanda yote kwa yote! Kudos........

Naomba ukaitoe kwenye gazeti pia.....tittle iwe "watanzania nani katuloga"?
 
Uliyoyasema ni sahihi viongozi wanalalamika sawa na wananchi sijui nani wa kumsaidia mwingine.wanasaini mikataba mibovu baadae wanalalamika migodi inanyonya wananchi na hawalipi kodi wakati mikataba imesainiwwa na wao na imeacha mianya ya kukwepa kodi.Tuanahitaji kiongozi anayejali maslahi ya Watanzania na kuelewa kuwa nchi hii ni tajiri ni sisi wananchi kutumia fursa na kuhakikisha fursa zilizopo zinatumika kwa maslahiya wengi na siowachache kama ilivyo sasa. TUMWOMBE MUNGU SANA KWA HILI, ATUPATIE KIONGOZI KWA KUWA NDIE MWENYE MAMLAKA.
 
Du ni ndefu sana lakini kwa kuwa imekandia sana imebidi niimalize maana sina jinsi
 
umeanza vizuri ila ukaamua kurudiarudia maneno ili iwe ndef ila kilichomo ni p..u..m..b..a tupu, andiki habari ndefu yenye maana na sio kuchosha watu kwa kurudiarudia maneno na km hauwezi kuanzisha uzi wenye maana changia uzi wa webgine
 
Ulichoandika ni kweli tupu mkuu,
lakini sababu lazima uzijueee........ziko wazi wazi kabisa...... Umaskini......

Wengi tunaingia jf kwa kulipia internet cafee, unalipia nusu saa sh. 1000/ kwa muda huo maandishi mareeefu huwezi kushughulika nayoooooo. Lazima utadili na post fupi fupi ili kupata taarifa nyingi kwa mpigo. Kubali kataaa huo ndio ukweli.

Pili ni aina ya watu wanaoingia jf, wengi ni graduates na wafanyakazi ambao wako bize muda woote huku wakitoa huduma kwa wananchi, so wanafanya vitu viwili kwa wakati mmoja. Kwa jinsi hii hawawezi kukaaa kusoma vitu ambavyo si sehemu yao ya kazi kwa zaidi ya dakika kumi...wanaogopa kuliibia taifa kuoitia post zetu ndefu ndefu. Upande wa graduates bado wanarudi kundi la mwanzo hawana mshiko pili wako bize kusaka kibarua.

Kwa mantiki hii unabaki na audience wachache ambao wako tayari kusoma post ndefundefu.... Ambazo hata mimi nazisomo during weekends ama usiku but mchana nahudumia watanzania mkuu.
Ni mtizamo tuu... Hatujalogwa wote mkuu
 
Nimejua kwanini uliweka utangulizi wa uvivu wa kusoma ha ha na sio kwamba haya uliyoiaweka hapa watu hawayajui wanayajua sana kinichowavunja watu moyo ni mfumo ambao unawakandamiza hata kuwachangua viongozi wanaowataka ni ngumu sana so kama kibinadamu wanachoka na hasa kama demokrasia inapo kandamizwa for the maximum watu wanakata kata tamaa wanajikuta wanahitaji mkombozi ambaye ni mimi na wewe kwani hauwezi kuwawaka watu kwenye kipimo sawa cha uelewa na uchambuzi kwahiyo badala ya kuwalaumu tujaribu kiwaonyesha njia ya matumaini ingwa si wote wanaweza kuucatch kwa wakati mmoja tuwe na subra.
 
Ni mfumo wa akili zetu (mind set) ndio unatuangusha, kwani umejengwa na mazingira yetu ya kitanzania, familia zetu za kitanzania na mfumo wa elimu yetu tanzania.
 
Watz walio wengi siku hizi wanataka usanii sanii tu(msinielewe vibaya wale wasanii wa fani-hii ni lugha ya mtaani) ati maandiko yakiwa marefu kidogo tu humu jf utasikia wachangiaji wanasepa " ooh nitaruda baadaye, ooh sina muda, ooh acha ngonjera" leo nawatolea uvivu. Mnajenga mapokeo mabaya kwa wadogo zenu, acheni uvivu bwana jaribu kukitumia vizuri kichwa kisiwe kinabeba nywele tu.

Hasa wewe unaependa kupiga porojo kijiweni bila hata kujua ulimwengu unaendaje kwa kusoma maandiko. Ukiangalia tv wewe ni tamthilia tu, tamthilia ni maigizo yaliyokolezwa uwongo, ndio maana utakuta kijana anafanya mambo ya ajabu ajabu ati anaiga ulaya wakati hata mguu wake haujagusa huko. Wazungu wangekua hivyo unafikiri wangendelea, thubutu!!!!.

Lazima niwe mkali kwa sababu inauma sana, utasikia kijana wa ki tz hataki kusunbua kichwa chake, mfano, kuna mada humu jf huwa zinajenga sana lkn ikiwa ndefu tu utaona vijana wavivu wanaanza kusema, ‘eh unatuchosha, andika kwa kifupi, hatutaki ngonjera n.k',watz wanataka vitu rahisi rahisi tu, kisa hatuna muda, lkn ukiangalia ubize wenyewe huoni, mara utaona mchana kutwa anashinda kwenye komputa kuangalia vitu vya ajabu ajabu, akitoka kazini anaenda vijiweni kuongea mambo yale yale ya siku zote, simaanishi kwamba usijichanganye la hasha ila ujue kwamba chanzo kikubwa cha maarifa ni kwenye maandishi, na wala sio maandishi rahisi rahisi tu hapana lazima kichwa au ubongo vifanye kazi ile inayokidhi haja ya uwepo wake, na unapoenda kijiweni uwe na kitu kipya cha kuongea na wenzako.

Nani kakuambia maendeleo au mambo mazuri yanakuja kwa urahisi rahisi tu. Ndio maana ufisadi umeshinda uadilifu tz kwa sababu wanaofanya ufisadi wanachemsha bongo zao kujua mbinu za kuwaibia watz lkn waadilifu wanalaza bongo na kulalamika tu. Hivi unajua maisha ni mafupi hapa duniani hivyo tunatakiwa kwa muda wa uhai wetu tudhihirishe uwepo wetu.

Hiyo ilikua trela tu, na wengine tayari wamechoka kusoma ‘hivi ni kweli kwamba mtz ukitaka kumficha kitu kiweke kwenye maandishi?' ngoja nianze kuandika nilichokusudia sasa.

Sichukii chama chochote cha siasa ila nawachukia watz (pamoja na mimi mwenyewe najichukia sababu ni mtz pia). Hivi ulitarajia chama tawala wasifie juhudi za vyama mbadala vishike dola, yaani kwa mawazo yako chama tawala wachekelee pale vyama
mbadala vipopata ungwaji mkono, kama mawazo yako ni hayo pole sana kwa sababu utachanganyikiwa na kuanza kuchukia kila mtu. Hebu amka timiza wajibu wako. Sio lazima iwe majukwaani, fanya unachokiweza km kufanya maombi, kuelimisha wale uliokaribu nao, kutimiza majukumu yako ikiwa ni pamoja na kupiga na kuhamasisisha watu kupiga kura.

Vijana hii ni nafisi yenu (simaanishi vijana wa umri ila wa kimtazamo, maana wazee wengine wanafagilia mabadiliko). Hapa tulipofikia tunahitaji mabadiliko, nani kakuambia chakula kilichochacha kikiwekwa kwenye chungu kizuri kitakua kitamu? Tumia akili yako vizuri mtz wewe.

Utasikia waoga wa mabadiliko wanasema hata chama kingine kikishika dola mambo yatakua yale yale tu, nani kakuambia wanaongoza hivyo vyama ni malaika, si umesikia maneno ya baadhi yao baada ya kupata umaarufu tu wameanza kusema wao ni mwarobaini wa umaarufu wa hivyo vyama vyao, utasikia ati yeye na mwenyekiti ndio wamekifikisha chama hapo kililpo, wanasahaua kujua ukweli kwamba kuna watz hawana nafasi ya majukwaa ya kisiasa lkn muda wote wanaomba kwa mungu ili mabadiliko ya kweli yaje na mungu anajibu kwa njia moja au nyingine, hivi hawajui kwamba kuna watz wanavitangaza hivyo vyama nyumba kwa nyumba bila hata kuwa wanachama.

Umaarufu kidogo tu keleleee, hata wananza kutoa kejeli kwa wakubwa wao. Naomba mnaongoza vyama mjua kwamba umaarufu wa chama unatokana na maombi ya watz na mungu huchagua kuwatumia wachache wasimame kuwa viongozi kwa niaba ya wengine, hivi wote tungetaka tuwe viongozi kwenye chama hivi hii nchi ingekua na amani? Ingekua busara sifa zitoke kwa wanokutazama na wala sio ujikweze mwenyewe.

Kinachoniuma sana ni pale ninaposikiliza hata wasomi wa tz wanaposema hata chama kingine kikija mambo yatakua yale yale, kwa mtazamo wa mtu asiyetaka kutumia akili yake vizuri ni kweli. Hebu nikuambie, kinachotafutwa na watz sio chama gani kizuri ila namna gani madaraka ya kuiajiri serikali yawe mikononi mwao (na wajue hivyo) na pale wasipotimiziwa matakwa yao kama waajiri waweke chama kingine. Na hata hicho kingine, mfano, chadema au cuf au nccr n.k kikishika dola na baadaye kisipotenda yale kilichotuahidi, tuwe na utashi na uwezo wa kukishikishe adabu kwa kukinyima kura .

Hapo kutakua na adabu kwa chama chochote tawala kwa kutenda yale yaliyo na manufaa kwa mwajiri(wananchi). Kwani si mnajua wenye kampuni wanapomwajiri mkurugenzi wanataka afanye kazi kwa maslahi yao ( kuzalisha faida kama ni kampuni ya biashara) na kama hajatimiza bila sababu za msingi hufukuzwa kwenye ajira ( mfano huu, watz ni wenyewe kampuni na wakurugenzi ni serikili iliyoko madarakani).

Hapa nieleze vizuri; janja ya mkurugenzi akishindwa kutekeleza matakwa ya mwajiri lazima afanye mambo ya aja ajabu ili waliomwajri wasijue udhaifu wake haraka, ataanza kujipendekeza kwa wakaguzi wa kampuni ili wasiandike ripoti mbaya hata kufikia kuwapa hongo (tunashuhudia rushwa za uchaguzi).

Kuwagawa wamiliki kwa njia za hila ili apate kuungwa mkono na baadhi (tunashuhudia propaganda za udini na ukabila), kujikusanyia mali nyingi isivyo halali –vikao vingi, kusafiri kwingi kwa ajili ya masurufu (tunashudia ufisadi wa kutisha), kujenga uraki wa mashaka na wale wenye uhusiano wa kiabiashara na kampuni ili achukue fedha isivyo halali na kizificha kwao (tunashuhudia jinsi kampuni zinavyoibuka/na zingine kufufuliwa lkn uwazi wa chanzo cha mitaji hakuna), kuhujumu kampuni kwa makusudi ili akifukuzwa wamiliki wapate shida ( tunashuhudia jinsi fedha zinavyofichwa nje ya nchi huku watz wakifa kwa kukosa huduma za tiba, wakilala njaa, wakikosa ajira kwa sababu fedha zimetoka nje ya mzunguko wa kutoa ajira).

Ngoja nikuambie, usiwe mwoga sana kwa sababu hakuna aliye juu ya mungu wetu aliye mbinguni, hivyo usimtegemee wala kumwogopa sana binadamu, huyo binadamu unayemtegemea au kumwogopa sana, leo yupo kesho hayupo lakini muumba wetu wa mbinguni ni wa milele, mungu akisema hutapata madhara au hutakufa mpaka utimize malengo fulani, amini amini hufi hadi hapo yeye atataka upumzike milele (si umeona huyu mnyambala nanii... Kama kweli alitegeshewa sumu hatari na hajafa, anadunda tu na anaendelea kuwahudumia watz). Badilika, tetea watz wenzio kwa namna yeyote ile.

Tatizo lipo hivi; kuna watu wakikaa muda mrefu sehemu fulani wanajiona wao ndio wenye haki miliki ya nahali pale. Angalia ccm ilivyo kwa sasa bila kuwa na mtu wa kukupigia debe(baba,mama, mjomba, shangazi, binamu, jirani au rafiki wa hao niliowataja) huna nafasi hata kama wewe ni mahiri kiasi gani(hasa hasa kama ni mkweli). Na hicho ndicho kinachowachosha watu wengine. Wengi wako humo kwa sababu ya maslahi na uwoga tu.

Woga unajidhihirisha unavyowasikia na kuwaona hata viongozi waliokuwa waandamizi na hata ambao wako ndani ya mfumo wanavyolalamikia mambo yanavyokwenda, hawana lolote hao ni waoga tu, wanadhani nje ya chama tawala cha sasa hakuna maisha, badilika acha kulalama lalama kama kweli ni mzalendo.

Baba wa taifa (r.i.p) mwenyewe alisema ccm sio mama yake, maanake angekuwa hai leo isingekuwa ndani ya ccm (hili liko wazi kabisa sababu hata viongozi wa chama wenye uwezo na mamlakaya kufanya mamuzi wanalalamika). Kwa hali hiyo, muda sasa umefika wa kufanya mabadiliko ili watoke nje wakatafakari na wakajipange upya.

Hapo juu nimesema hata vyama mbadala viongozi wake sio malaika, hivyo wanamapungufu yao. Wengine wako kwenye vyama mbadala lakini mawazo yao, wasiri wao, mienendo yao, majigambo yao wanachukua toka chama tawala. Si umewakia miongoni mwao wanavyosema ati chadema kisingekua maarufu bila ya yeye(wao) na m/kiti. Wanasahau kwamba kinachofanya chama kiwe maarufu inatokana na udhaifu wa chama kinachotawala na hivyo maombi mengi ya waja wake mungu yanaelekezwa kwenye mabadiliko. Hawa viongozi nawaheshimu sana kwa sababu ni mahiri na weledi sana, lakini fikra zao ni za ki-ccm sijui kwa nini,sijui washauri wao ni akina nani. Najua wamepotoka kidogo tu watabadilika na w ataonekana wapo pamoja na wenzao kwenye mapambano ya mabadiliko.

Jamani hakuna aliye mkamilifu, si kila binadamu aliyezaliwa na mwanamke amewahi kufanya makosa? Muhimu ni kwamba mtu akifanya
kosa na akashauriwa kujirekebisha afanya hivyo. Nieleweke hivi, tatizo sio kutaka ukiranja(urais), inawezekana kweli wana uwezo wa kuwa viranja wa tz, kinachotakiwa kwa sasa ni namna gani mhitaji wa huo utukufu anashirikiana na wenziwe kufika hapo bila kuathiri umoja na mshikamano wa chama, nje ya hapo tunaona kama ni ubinafsi na usaliti, ni wazi kwamba ndani ya chama hicho kuna vijana wengi wenye uwezo wa kuongoza na pia wanatamani siku moja waje kugombea ukiranja lkn busara inatumika na wamekua watulivu.

Hivi kila mtu ndani ya chama anayejiona unaweza kuongoza atangaze kugombea ukiranja umoja ndani ya chama utakuwepo? Muda wa sasa sio kuanza kulumbana nani agombee ukiranja bali kuimarisha chama. Kila kiongozi akianza kutangaza kugombea chama kitapoteza mwelekeo.

Namfagilia sana huyu mzee anayetoka kwa wafugaji,sijamsikia hata siku moja kujisifia. Nani hajui alivyokibeba chadema kwenye uchaguzi wa 2010,angekua mtu wa misifa si angepasuka kwa masifa, naomba mungu wetu wa mbinguni ampe maisha marefu na afya njema kimwili na kiakili pia kwa sababu hata kama hatakuwa raisi lakini ana mambo mengi na uwezo mkubwa wa kuitendea nchi hii. Samahani simfugilii huyu mzee kwa hila na wala hata hanifahamu na sihitaji anifahamu, lkn kusema kweli huu upepo wa mabadiliko uliopo umerutubishwa na mzee huyu.

Simpigii kampeni ili chadema wamteue kugombea 2015 mungu akimpa afya njema kwa sababu naamini kama chama wamejipanga vyema namna ya kumpata mgombea kwa njia ya uwazi na umakini. Huyu mzee tumwombee afya njema na mungu amwongezee hekima na unyenyekevu (low profile).

Kwa sababu ya propaganda tu na ubinafsi baadhi ya watu waliofilika kimtazamo na maadili wanawatia hofu ndugu zangu waislamu ati kwa sababu ni padri hawezi kuwatendea haki, sio kweli, nimejaribu sana kumfuatilia maongeze yake pamoja na hoja zake sio mtu wa kuendekeza udini, anajali sana ustawi wa watz bila kuegemea imani yake. Naomba ndugu zangu waislamu na wakristo tumpime mtu kwa matendo yake na wala sio kwa hisia tu na kusikiliza propaganda.

Ni ukweli ulio wazi kwamba chadema wasipotumia vizuri huu mwamko watavuna dhambi. Watavuna dhambi kwa sababu watz angalau wameweka matumaini kwao (baada ya nccr 1995 na cuf 2005). Wakishindwa kuonyesha bayana kwamba wana nia ya kuleta mageuzi, ni imani yangu kwamba itachukua muda mrefu wananchi kuamini tena kwamba chama mbadala kitatawala nchi hii. Hakuna kisingizio cha kuibiwa kura, si mnajua hilo? Kujua tatizo ndio msingi wa kutatua tatizo,hatutasikia tena tatizo la ‘ooh usalama wa taifa wamechakachua, ooh polisi wanawabeba n.k'.

Hawa usalama wa taifa kwani wanafurahia ufidi unaoendelea, si tunaishi nao mtaani hawa, wanapigika kama sisi na wanalalamika
kama sisi, ndugu zao wanakosa dawa wakienda hospili kama sisi, binamu zao wanakula mlo mmoja kama sisi. Nawashauri hao usalama wa watz na polisi kwamba wasimamie mabadiliko hayo kwa uaminifu mkubwa ili nchi yet isingie kwenye machafuko, hivi kwa jinsi watz tunavyoishi kwa udugu nyie walinda usalama mtapata wapi ujasiri wa kuwakandamiza watz wenzenu, si tunakua na nyinyi misikitini na makanisani, hivi utamwambia nini mumba wako akikuliza kuhusu kuwatumikia mafisadi badala ya kutumikia nchi.

Mimi sijui wanajifunza nini kuhusu usalama wa taifa ila nadhaniwanafundishwa kuwatamikia watz kwa jinsi hiyo ni lazima wawalinde kwa gharama yoyote wanao simamia ustawi wa watz, for that matter viongozi wanaosimamia rasilimali za nchi kwa uadilifu, kiongozi amepewa kipaumbele cha ulinzi kwa sababu inaminika kwamba anasimamia ulinzi wa mali na maisha ya watz wengine kwa ustawi wa nchi na wala sio yule anayehujumu ustawi wa nchi.

Hapa nasisitiza , karibu wanausalama wote ni waadilifu na weledi isipokua wachache tu wenye maslahi binafsi na waroho. Huku ndio kulogwa sasa, ati inakuwaje wachache wanaosaidia uovu wawashinde wengi wenye uchungu na ndugu zao watz, itabidi nimtafute profesor wangu mmoja tutengeneze theory ya kusapoti hicho kitu na tutafute evidence za kusapoti (si unajua wazungu wametupumbaza, ati hamna kitu kipya mwafrika anaweza gundua, yaani yeye ni kukopi tu ya waliyogundua wazungu au akitaka kufanya kitu lazima kuwe na reference ya kitu kilichofanyika yaani hamna kitu kipya tena hapa duniani.

Lkn mbona mazingira ni tofauti sana na ya kwao). Hebu imarisheni njia ya kushirikiana hao wanausalama wenye nia njema na nchi hii hata kwa siri, si wapo jamani wenye uchungu wa kweli na nchi hii, tena ni wengine tu, si hata shule waliyoenda kwa kiwango chochote wamelipiwa na kodi za wananchi hohehahe, nina amini wadilifu wapo tena wengi sana. Hata police wazalendo wapo wengi tu, si tunaishi nao mtaani, tunakunywa nao, ni ndugu zetu, kwani wenyewe hawaoni jamanikwamba njia nzuri ni kumpa madaraka mwananchi ya kuajari serikali na kuitimua (hire and fire –sijui vizuri kithungu usinicheke).

Kitu kingine kinachokera, ati baba ndani ya nyumba analalamika lalamika kwamba kwanini watoto wake wanakosa chakula wakati mwenyezi mungu amempa afya, akili,madaraka na mamlaka kuongoza familia. Watoto wakilalamika kwamba tunalala njaa anawashangaa ati kwa nini wanalalamika (nadhani yeye hasikii njaa kwa sababu akiwa huko baa anapata supu). Kama baba ana shamba si awambie watoto kwamba shamba liko na andae pembejeo wakalime, sasa unashangaa nini, unataka watoto wafurahie kushinda njaa.

Siku hizi viongozi ndio wa kwanza kulalamika kuhusu mambo yanavyokwenda hovyo, hata wale tuliowapa mamlaka na madaraka ya kufanya maamuzi nao wanalalamika. Imekua nchi ya walalamikaji tu, wewe kiongozi unalalamika unafikiri wananchi watashindwa kulalamika, kiongozi maana yake tumekuamini uwe mbele yetu utuonyeshe mwelekeo. Ati wananchi wakilalamika viongozi wanashangaa na kuwabeza, kwa nini kama kiongozi usiwaelekeze njia maana kazi ya kiongozi ni kuonyesha njia. Kama umeshindwa kuonyesha njia si upishe wengine watuelekeze njia.

Kila mtu akifanya kila anavyotaka si itakua vurugu. Matokea ya kila mtu kufanya atakavyo ndio tunaona biashara zinafanyika barabarani bila utaratibu, kwa nini baada ya uchaguzi mnawatimua wamachinga sehemu wanazofanyia biashara (barabarani) si mnasema kila mtu afanye kinachomfaa, mnafikiri watu wengi wanajua sheria?

Maana ya kiongozi ni kuwasikiliza anaowangoza na kuonyesha zilipo fusa kwa ajili ya ustawi wa maisha ya walio mwamini kuwaongoza. Tatizo zaidi ni kwamba ukiwa kiongozi tz unajua kila kitu, hawataki ushauri, wanafanya vile wanavyotaka hadi tumefikia hatua ya wataalamu kukata tamaa, ndio maana wataalamu nao wameamua kuingia kwenye siasa kwa kasi.

Hivi nani katuloga watz? Tumekua watu wa kutegeana tegeana tu, viongozi wengi kwenye sehemu za kazi wanaogopa kufanya maamuzi magumu, wanafalsafa wanasema afadhali kufanya maamuzi mabaya kuliko kutofanya kabisa, bila kufanya maamuzi utajifunzaje? Inawezekana inatokana na kukatishwa tamaa na namna ya maamuzi yanavyopokelewa na walio juu yao, lakini mbona hata hao walio juu kabisa wanakua waoga wa kufana maamuzi. Nadhani tatizo ni kwamba viongozi wanataka kumfurahisha kila mtu na hivyo kubaki njia panda (vua gamba).

La mwisho kwa leo lkn muhimu sana; naomba watz kwa ujumla wetu na kila mmoja na dini yake tumwombe mwenyezi mungu ifikapo 2015 atupe kiongozi(raisi) makini anayejua kwamba nchi ya tz ina kila aina ya utajiri kwa ustawi wa watz. Ni nguvu kidogo tu zinahitajika kuamsha uchumi uliolala na kuwaongozi watz kutambua kuwa nguvu zao, akili zao na maarifa yao ndio msingi wa maisha mazuri.

Hatuhitaji tena kuendlea kuwa omba omba (inakera), hatuhitaji kiongozi anaye lalamika lalamika (maana anawakatisha tamaa anaowaongoza), tunahitaji kiongozi ambaye ni mnyenyekevu lakini jasiri wa maamuzi, sio kiongozi anayekimbilia ikulu kwa nguvu yake mwenyewe na wapambe wake, tunahitaji maombi ili mungu atupe hekima ya kutambua hila zinazotumika za kutugawa kwa makusudi kwa kutumia propaganda za udini, ukabila na ukanda. Tunahitaji kiongozi anayetokana na maombi ya watanzania kwa mungu wala sio anayesubiri ndoto zake(mara nyingi unachofikiria kichwani ndicho kinakuja kwenye ndoto na pia shetani anaweza kupitia kwa njia ya ndoto).

Tuombe kiongozi anayetambua kuwa rushwa itapungua sana kwa kuimarisha huduma muhimu za uma ( kama elimu na afya) na kuweka matumaini mazuri ya maisha ya watumishi wa uma waminifu watakapo staafu utumishi na wala sio majigambo ya majukwaani. Tunaomba mungu atuondolee woga wa mabadiliko na kuomba kwamba mabadiliko yaje kwa njia ya amani(maana tukitaka kuondokana na ombwe hili lilipo lazima tufanye mabadiliko).

Tunaomba mwenyezi Mungu aibariki tanzania na watu wake, atupe hekima ili mabadiliko yanayokuja (naamini yanakuja)
yambatane na amani, amina
kama muumini tu alishidwa kuwatendea haki itakuwa kwa kiongozi? no body is ready to risk again. otherwise is fool.
 
Watanzania walio wengi siku hizi wanataka usanii sanii tu(msinielewe
vibaya wale wasanii wa fani-hii ni lugha ya mtaani) ati maandiko
yakiwa marefu kidogo tu humu jf utasikia wachangiaji wanasepa
"ooh nitaruda baadaye, ooh sina muda, ooh acha ngonjera". Leo
nawatolea uvivu. Mnajenga mapokeo gani mabaya kwa wadogo zenu?,
acheni uvivu bwana jaribu kukitumia vizuri kichwa kisiwe kinabeba
nywele tu.

Hasa wewe unaependa kupiga porojo kijiweni bila hata kujua ulimwengu
unaendaje kwa kusoma maandiko. Ukiangalia tv wewe ni tamthilia tu,
tamthilia ni maigizo yaliyokolezwa uwongo, ndio maana utakuta kijana
anafanya mambo ya ajabu ajabu ati anaiga ulaya wakati hata mguu
wake haujagusa huko. Wazungu wangekua hivyo unafikiri wangendelea,
thubutu!!!!.

Lazima niwe mkali kwa sababu inauma sana, utasikia kijana wa ki tz hataki
kusunbua kichwa chake, mfano, kuna mada humu jf huwa zinajenga sana
lkn ikiwa ndefu tu utaona vijana wavivu wanaanza kusema, ‘eh unatuchosha,
andika kwa kifupi, hatutaki ngonjera n.k',watanzania wanataka vitu rahisi rahisi tu,
kisa hatuna muda, lkn ukiangalia ubize wenyewe huoni, mara utaona mchana
kutwa anashinda kwenye komputa kuangalia vitu vya ajabu ajabu, akitoka
kazini anaenda vijiweni kuongea mambo yale yale ya siku zote, simaanishi
kwamba usijichanganye la hasha ila ujue kwamba chanzo kikubwa cha maarifa
ni kwenye maandishi, na wala sio maandishi rahisi rahisi tu hapana lazima kichwa
au ubongo vifanye kazi ile inayokidhi haja ya uwepo wake, na unapoenda kijiweni
uwe na kitu kipya cha kuongea na wenzako.

Nani kakuambia maendeleo au mambo mazuri yanakuja kwa urahisi rahisi tu.
Ndio maana ufisadi umeshinda uadilifu hapa Tanzania kwa sababu wanaofanya ufisadi
wanachemsha bongo zao kujua mbinu za kuwaibia watz lkn waadilifu wanalaza
bongo na kulalamika tu. Hivi unajua maisha ni mafupi hapa duniani hivyo tunatakiwa
kwa muda wa uhai wetu tudhihirishe uwepo wetu.

Hiyo ilikua trela tu, na wengine tayari wamechoka kusoma ‘hivi ni kweli kwamba mtz
ukitaka kumficha kitu kiweke kwenye maandishi?' Ngoja nianze kuandika nilichokusudia
sasa.

Sichukii chama chochote cha siasa ila nawachukia watanzania (pamoja na mimi mwenyewe
najichukia sababu ni mtanzania pia). Hivi ulitarajia chama tawala wasifie juhudi za vyama
mbadala vishike dola, yaani kwa mawazo yako chama tawala wachekelee pale vyama
mbadala vipopata ungwaji mkono, kama mawazo yako ni hayo pole sana kwa sababu
utachanganyikiwa na kuanza kuchukia kila mtu. Hebu amka timiza wajibu wako.
Sio lazima iwe majukwaani, fanya unachokiweza km kufanya maombi, kuelimisha
wale uliokaribu nao, kutimiza majukumu yako ikiwa ni pamoja na kupiga na kuhamasisisha
watu kupiga kura.

Vijana hii ni nafisi yenu (simaanishi vijana wa umri ila wa kimtazamo, maana wazee
wengine wanafagilia mabadiliko na kuna vijana wanawaza kama wazee). Hapa tulipofikia
tunahitaji mabadiliko, nani kakuambia chakula kilichochacha kikiwekwa kwenye chungu
kizuri kitakua kitamu? Tumia akili yako vizuri mtz wewe.

Utasikia waoga wa mabadiliko wanasema hata chama kingine kikishika dola mambo
yatakua yale yale tu, nani kakuambia wanaongoza hivyo vyama ni malaika, si umesikia
maneno ya baadhi yao baada ya kupata umaarufu tu wameanza kusema wao ni
mwarobaini wa umaarufu wa hivyo vyama vyao, utasikia ati yeye na mwenyekiti ndio
wamekifikisha chama hapo kililpo, wanasahaua kujua ukweli kwamba kuna watz hawana
nafasi ya majukwaa ya kisiasa lkn muda wote wanaomba kwa Mungu ili mabadiliko ya
kweli yaje na Mungu anajibu kwa njia moja au nyingine, hivi hawajui kwamba kuna watz
wanavitangaza hivyo vyama nyumba kwa nyumba bila hata kuwa wanachama.
Umaarufu kidogo tu keleleee, hata wananza kutoa kejeli kwa wakubwa wao. Naomba
mnaongoza vyama mjua kwamba umaarufu wa chama unatokana na maombi ya watz
na Mungu huchagua kuwatumia wachache wasimame kuwa viongozi kwa niaba ya
wengine, hivi wote tungetaka tuwe viongozi kwenye chama hivi hii nchi ingekua na
amani? Ingekua busara sifa zitoke kwa wanokutazama na wala sio ujikweze mwenyewe.

Kinachoniuma sana ni pale ninaposikiliza hata wasomi wa tz wanaposema hata chama
kingine kikija mambo yatakua yale yale, kwa mtazamo wa mtu asiyetaka kutumia akili
yake vizuri ni kweli. Hebu nikuambie, kinachotafutwa na watz sio chama gani kizuri ila
namna gani madaraka ya kuiajiri serikali yawe mikononi mwao (na wajue hivyo) na pale
wasipotimiziwa matakwa yao kama waajiri waweke chama kingine. Na hata hicho kingine,
mfano, chadema au cuf au nccr n.k kikishika dola na baadaye kisipotenda yale kilichotuahidi,
tuwe na utashi na uwezo wa kukishikishe adabu kwa kukinyima kura .

Hapo kutakua na adabu kwa chama chochote tawala kwa kutenda yale yaliyo na manufaa
kwa mwajiri(wananchi). Kwani si mnajua wenye kampuni wanapomwajiri mkurugenzi wanataka
afanye kazi kwa maslahi yao ( kuzalisha faida kama ni kampuni ya biashara) na kama hajatimiza
bila sababu za msingi hufukuzwa kwenye ajira ( mfano huu, watz ni wenyewe kampuni na
wakurugenzi ni serikili iliyoko madarakani).

Hapa nieleze vizuri; janja ya mkurugenzi akishindwa kutekeleza matakwa ya mwajiri lazima
afanye mambo ya aja ajabu ili waliomwajri wasijue udhaifu wake haraka, ataanza kujipendekeza
kwa wakaguzi wa kampuni ili wasiandike ripoti mbaya hata kufikia kuwapa hongo (tunashuhudia
rushwa za uchaguzi).

Kuwagawa wamiliki kwa njia za hila ili apate kuungwa mkono na baadhi (tunashuhudia
propaganda za udini na ukabila), kujikusanyia mali nyingi isivyo halali –vikao vingi, kusafiri
kwingi kwa ajili ya masurufu (tunashudia ufisadi wa kutisha), kujenga uraki wa mashaka na
wale wenye uhusiano wa kiabiashara na kampuni ili achukue fedha isivyo halali na kizificha
kwao (tunashuhudia jinsi kampuni zinavyoibuka/na zingine kufufuliwa lkn uwazi wa chanzo
cha mitaji hakuna), kuhujumu kampuni kwa makusudi ili akifukuzwa wamiliki wapate shida
( tunashuhudia jinsi fedha zinavyofichwa nje ya nchi huku watz wakifa kwa kukosa huduma
za tiba, wakilala njaa, wakikosa ajira kwa sababu fedha zimetoka nje ya mzunguko wa
kutoa ajira).

Ngoja nikuambie, usiwe mwoga sana kwa sababu hakuna aliye juu ya Mungu wetu
aliye Mbinguni, hivyo usimtegemee wala kumwogopa sana binadamu, huyo binadamu
unayemtegemea au kumwogopa sana, leo yupo kesho hayupo lakini Muumba wetu wa
Mbinguni ni wa milele, Mungu akisema hutapata madhara au hutakufa mpaka utimize
malengo fulani, amini amini hufi hadi hapo yeye atataka upumzike milele (si umeona
huyu mnyambala nanii... Kama kweli alitegeshewa sumu hatari na hajafa, anadunda tu
na anaendelea kuwahudumia watz). Badilika, tetea watz wenzio kwa namna yeyote ile.

Tatizo lipo hivi; kuna watu wakikaa muda mrefu sehemu fulani wanajiona wao
ndio wenye haki miliki ya nahali pale. Angalia ccm ilivyo kwa sasa bila kuwa na
mtu wa kukupigia debe(baba,mama, mjomba, shangazi, binamu, jirani au rafiki wa
hao niliowataja) huna nafasi hata kama wewe ni mahiri kiasi gani(hasa hasa kama
ni mkweli). Na hicho ndicho kinachowachosha watu wengine. Wengi wako humo kwa
sababu ya maslahi na uwoga tu.

Woga unajidhihirisha unavyowasikia na kuwaona hata viongozi waliokuwa waandamizi
na hata ambao wako ndani ya mfumo wanavyolalamikia mambo yanavyokwenda, hawana
lolote hao ni waoga tu, wanadhani nje ya chama tawala cha sasa hakuna maisha, badilika
acha kulalama lalama kama kweli ni mzalendo.

Baba wa taifa (r.i.p) mwenyewe alisema ccm sio mama yake, maanake angekuwa hai leo
isingekuwa ndani ya ccm (hili liko wazi kabisa sababu hata viongozi wa chama wenye uwezo
na mamlakaya kufanya mamuzi wanalalamika). Kwa hali hiyo, muda sasa umefika wa
kufanya mabadiliko ili watoke nje wakatafakari na wakajipange upya.

Hapo juu nimesema hata vyama mbadala viongozi wake sio malaika, hivyo wanamapungufu
yao. Wengine wako kwenye vyama mbadala lakini mawazo yao, wasiri wao, mienendo yao,
majigambo yao wanachukua toka chama tawala. Si umewakia miongoni mwao wanavyosema
ati chadema kisingekua maarufu bila ya yeye(wao) na m/kiti. Wanasahau kwamba kinachofanya
chama kiwe maarufu inatokana na udhaifu wa chama kinachotawala na hivyo maombi mengi
ya waja wake Mungu yanaelekezwa kwenye mabadiliko. Hawa viongozi nawaheshimu sana
kwa sababu ni mahiri na weledi sana, lakini fikra zao ni za ki-ccm sijui kwa nini,sijui washauri
wao ni akina nani. Najua wamepotoka kidogo tu watabadilika na w ataonekana wapo pamoja
na wenzao kwenye mapambano ya mabadiliko.

Jamani hakuna aliye mkamilifu, si kila binadamu aliyezaliwa na mwanamke amewahi kufanya
makosa? Muhimu ni kwamba mtu akifanya kosa na akashauriwa kujirekebisha afanya hivyo.

Nieleweke hivi, tatizo sio kutaka ukiranja(urais), inawezekana kweli wana uwezo wa kuwa
viranja wa tz, kinachotakiwa kwa sasa ni namna gani mhitaji wa huo utukufu anashirikiana
na wenziwe kufika hapo bila kuathiri umoja na mshikamano wa chama, nje ya hapo tunaona
kama ni ubinafsi na usaliti, ni wazi kwamba ndani ya chama hicho kuna vijana wengi wenye
uwezo wa kuongoza na pia wanatamani siku moja waje kugombea ukiranja lkn busara inatumika
na wamekua watulivu.

Hivi kila mtu ndani ya chama anayejiona unaweza kuongoza atangaze kugombea ukiranja
umoja ndani ya chama utakuwepo? Muda wa sasa sio kuanza kulumbana nani agombee
ukiranja bali kuimarisha chama. Kila kiongozi akianza kutangaza kugombea chama kitapoteza
mwelekeo.

Namfagilia sana huyu mzee anayetoka kwa wafugaji,sijamsikia hata siku moja kujisifia.
Nani hajui alivyokibeba chadema kwenye uchaguzi wa 2010,angekua mtu wa misifa si
angepasuka kwa masifa, naomba Mungu wetu wa Mbinguni ampe maisha marefu na afya
njema kimwili na kiakili pia kwa sababu hata kama hatakuwa raisi lakini ana mambo mengi
na uwezo mkubwa wa kuitendea nchi hii. Samahani simfugilii huyu mzee kwa hila na wala
hata hanifahamu na sihitaji anifahamu, lkn kusema kweli huu upepo wa mabadiliko uliopo
umerutubishwa na mzee huyu.

Simpigii kampeni ili chadema wamteue kugombea 2015 Mungu akimpa afya njema kwa
sababu naamini kama chama wamejipanga vyema namna ya kumpata mgombea kwa njia
ya uwazi na umakini. Huyu mzee tumwombee afya njema na Mungu amwongezee hekima
na unyenyekevu (low profile).

Kwa sababu ya propaganda tu na ubinafsi baadhi ya watu waliofilika kimtazamo na
maadili wanawatia hofu ndugu zangu waislamu ati kwa sababu ni padri hawezi kuwatendea
haki, sio kweli, nimejaribu sana kumfuatilia maongeze yake pamoja na hoja zake sio mtu
wa kuendekeza udini, anajali sana ustawi wa watz bila kuegemea imani yake. Naomba ndugu
zangu waislamu na wakristo tumpime mtu kwa matendo yake na wala sio kwa hisia tu na
kusikiliza propaganda.

Ni ukweli ulio wazi kwamba chadema wasipotumia vizuri huu mwamko watavuna dhambi.
Watavuna dhambi kwa sababu watz angalau wameweka matumaini kwao (baada ya nccr
1995 na cuf 2005). Wakishindwa kuonyesha bayana kwamba wana nia ya kuleta mageuzi,

ni imani yangu kwamba itachukua muda mrefu wananchi kuamini tena kwamba chama
mbadala kitatawala nchi hii. Hakuna kisingizio cha kuibiwa kura, si mnajua hilo? Kujua tatizo
ndio msingi wa kutatua tatizo,hatutasikia tena tatizo la ‘ooh usalama wa taifa wamechakachua,
ooh polisi wanawabeba n.k'.

Hawa usalama wa taifa kwani wanafurahia ufidi unaoendelea, si tunaishi nao mtaani hawa,
wanapigika kama sisi na wanalalamika kama sisi, ndugu zao wanakosa dawa wakienda
hospili kama sisi, binamu zao wanakula mlo mmoja kama sisi. Nawashauri hao usalama
wa watz na polisi kwamba wasimamie mabadiliko hayo kwa uaminifu mkubwa ili nchi yet
isingie kwenye machafuko, hivi kwa jinsi watz tunavyoishi kwa udugu nyie walinda usalama
mtapata wapi ujasiri wa kuwakandamiza watz wenzenu, si tunakua na nyinyi misikitini na
makanisani, hivi utamwambia nini Muumba wako akikuliza kuhusu kuwatumikia mafisadi badala
ya kutumikia nchi.

Mimi sijui wanajifunza nini kuhusu usalama wa taifa ila nadhaniwanafundishwa
kuwatamikia watz kwa jinsi hiyo ni lazima wawalinde kwa gharama yoyote wanao
simamia ustawi wa watz, for that matter viongozi wanaosimamia rasilimali za nchi
kwa uadilifu, kiongozi amepewa kipaumbele cha ulinzi kwa sababu inaminika kwamba

anasimamia ulinzi wa mali na maisha ya watz wengine kwa ustawi wa nchi na wala
sio yule anayehujumu ustawi wa nchi.

Hapa nasisitiza , karibu wanausalama wote ni waadilifu na weledi isipokua wachache
tu wenye maslahi binafsi na waroho. Huku ndio kulogwa sasa, ati inakuwaje wachache
wanaosaidia uovu wawashinde wengi wenye uchungu na ndugu zao watz, itabidi
nimtafute profesor wangu mmoja tutengeneze theory ya kusapoti hicho kitu na tutafute
evidence za kusapoti (si unajua wazungu wametupumbaza, ati hamna kitu kipya mwafrika
anaweza gundua, yaani yeye ni kukopi tu ya waliyogundua wazungu au akitaka
kufanya kitu lazima kuwe na reference ya kitu kilichofanyika yaani hamna kitu kipya
tena hapa duniani. Lkn mbona mazingira ni tofauti sana na ya kwao). Hebu imarisheni njia ya kushirikiana
hao wanausalama wenye nia njema na nchi hii hata kwa siri, si wapo jamani wenye
uchungu wa kweli na nchi hii, tena ni wengine tu, si hata shule waliyoenda kwa kiwango
chochote wamelipiwa na kodi za wananchi hohehahe, nina amini wadilifu wapo tena wengi
sana. Hata police wazalendo wapo wengi tu, si tunaishi nao mtaani, tunakunywa nao, ni
ndugu zetu, kwani wenyewe hawaoni jamanikwamba njia nzuri ni kumpa madaraka
mwananchi ya kuajari serikali na kuitimua (hire and fire –sijui vizuri kithungu usinicheke).

Kitu kingine kinachokera, ati baba ndani ya nyumba analalamika lalamika kwamba
kwanini watoto wake wanakosa chakula wakati mwenyezi Mungu amempa afya,

akili,madaraka na mamlaka kuongoza familia. Watoto wakilalamika kwamba tunalala
njaa anawashangaa ati kwa nini wanalalamika (nadhani yeye hasikii njaa kwa sababu
akiwa huko baa anapata supu). Kama baba ana shamba si awambie watoto kwamba
shamba liko na andae pembejeo wakalime, sasa unashangaa nini, unataka watoto
wafurahie kushinda njaa.

Siku hizi viongozi ndio wa kwanza kulalamika kuhusu mambo yanavyokwenda hovyo,
hata wale tuliowapa mamlaka na madaraka ya kufanya maamuzi nao wanalalamika.
Imekua nchi ya walalamikaji tu, wewe kiongozi unalalamika unafikiri wananchi watashindwa
kulalamika, kiongozi maana yake tumekuamini uwe mbele yetu utuonyeshe mwelekeo.
Ati wananchi wakilalamika viongozi wanashangaa na kuwabeza, kwa nini kama
kiongozi usiwaelekeze njia maana kazi ya kiongozi ni kuonyesha njia. Kama umeshindwa
kuonyesha njia si upishe wengine watuelekeze njia.

Kila mtu akifanya kila anavyotaka si itakua vurugu. Matokea ya kila mtu kufanya
atakavyo ndio tunaona biashara zinafanyika barabarani bila utaratibu, kwa nini
baada ya uchaguzi mnawatimua wamachinga sehemu wanazofanyia biashara
(barabarani) si mnasema kila mtu afanye kinachomfaa, mnafikiri watu wengi wanajua
sheria?

Maana ya kiongozi ni kuwasikiliza anaowangoza na kuonyesha zilipo fusa kwa ajili ya
ustawi wa maisha ya walio mwamini kuwaongoza. Tatizo zaidi ni kwamba ukiwa kiongozi
tz unajua kila kitu, hawataki ushauri, wanafanya vile wanavyotaka hadi tumefikia hatua
ya wataalamu kukata tamaa, ndio maana wataalamu nao wameamua kuingia kwenye
siasa kwa kasi.

Hivi nani katuloga watz? Tumekua watu wa kutegeana tegeana tu, viongozi wengi
kwenye sehemu za kazi wanaogopa kufanya maamuzi magumu, wanafalsafa wanasema
afadhali kufanya maamuzi mabaya kuliko kutofanya kabisa, bila kufanya maamuzi
utajifunzaje? Inawezekana inatokana na kukatishwa tamaa na namna ya maamuzi
yanavyopokelewa na walio juu yao, lakini mbona hata hao walio juu kabisa wanakua
waoga wa kufana maamuzi. Nadhani tatizo ni kwamba viongozi wanataka kumfurahisha
kila mtu na hivyo kubaki njia panda (vua gamba).

La mwisho kwa leo lkn muhimu sana; naomba watz kwa ujumla wetu na kila mmoja na
dini yake tumwombe mwenyezi Mungu ifikapo 2015 atupe kiongozi(raisi) makini anayejua
kwamba nchi ya tz ina kila aina ya utajiri kwa ustawi wa watz. Ni nguvu kidogo tu
zinahitajika kuamsha uchumi uliolala na kuwaongozi watz kutambua kuwa nguvu zao,
akili zao na maarifa yao ndio msingi wa maisha mazuri.

Hatuhitaji tena kuendlea kuwa omba omba (inakera), hatuhitaji kiongozi anaye lalamika

lalamika (maana anawakatisha tamaa anaowaongoza), tunahitaji kiongozi ambaye ni
mnyenyekevu lakini jasiri wa maamuzi, sio kiongozi anayekimbilia ikulu kwa nguvu yake
mwenyewe na wapambe wake, tunahitaji maombi ili Mungu atupe hekima ya kutambua
hila zinazotumika za kutugawa kwa makusudi kwa kutumia propaganda za udini, ukabila
na ukanda. Tunahitaji kiongozi anayetokana na maombi ya watanzania kwa Mungu wala
sio anayesubiri ndoto zake(mara nyingi unachofikiria kichwani ndicho kinakuja kwenye
ndoto na pia shetani anaweza kupitia kwa njia ya ndoto).

Tuombe kiongozi anayetambua kuwa rushwa itapungua sana kwa kuimarisha huduma
muhimu za umma ( kama elimu na afya) na kuweka matumaini mazuri ya maisha ya
watumishi wa umma waminifu watakapo staafu utumishi na wala sio majigambo ya
majukwaani. Tunaomba Mungu atuondolee woga wa mabadiliko na kuomba kwamba
mabadiliko yaje kwa njia ya amani(maana tukitaka kuondokana na ombwe hili lilipo
lazima tufanye mabadiliko).

Tunaomba Mwenyezi Mungu aibariki tanzania na watu wake, atupe hekima ili mabadiliko
yanayokuja (naamini yanakuja)

yambatane na amani, amina
Nitarudi baadae kulisoma hili gazeti, sina muda sasa hivi

au hauna summary kidogo
 
Kuna mambo ya msingi,Ila uandishi ndio shida.
 
Back
Top Bottom