Du kumbe na jirani yangu ni changuduoa anajiuza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Du kumbe na jirani yangu ni changuduoa anajiuza

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by bornagain, Sep 28, 2012.

 1. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Jamani ukistaajabu ya Musa utaona sijui ya nani, mwenzio nimepata aibu ya mwaka nikiwa na mama mkwe wangu. Kwa kifupi ni kwamba nilikua nimetembelewa na mama yangu mkwe kutoka huko Katavi mkoa mpya na kwa bahati mbaya ndo mara yake ya kwanza kuja Dar. Kutokana na mihangaiko ya kazi za mchana na ratiba kuwa tight siku za weekend na siku za weekdays sikufanikiwa hata siku moja kumtoa dina, juzi usiku ikabidi twende zetu dina mimi mke wangu na mama mkwe maeneo ya posta maana yeye alikua anaondoka siku inayofuata yaani jana kurudi Katavi. Sasa tukawa tumechelewa kutoka mpaka kwenye saa nne na nusu usiku, wakati wa kurudi njiani maeneo ya Africa Sana – Sinza tukapata pancha nikawaambia mke wangu na mama mkwe wakae kwenye gari tu ili nitafute kijana maeneo ya standi ya daladala Africa sana au hata pale kwenye kituo cha mafuta anisaidie kubadilisha tairi hata kwa kumlipa maana sikutaka kuchafua suti yangu.

  Ile kushuka ndani ya gari kutembea tu hatua kama tano nikavamiwa na machangu kama wawili wote wakafikiri nataka huduma kumbe mimi natafuta kijana wa kunisadia kubadilisha tairi. Lakini kilichonistua ni kumwona dada ambae ni jirani yangu na pia tunafanya nae ofisi za karibu maeneo ya mjini nae akiwa miongoni mwa wale wasichana wawili waliokuwa wanafikiri nataka huduma.Alivoniona alijiskia vibaya alitamani ardhi ipasuke. Sasa mimi sielewi hivi wasichana wanajiuza for only finding satisfactions, au shida za maisha au ni hulka tu ya wasichana? Nasema hivo kwa sababu huyo dada ana kazi nzuri tu ingawa sijui mshahara wake lakini kazi yake inaweza kumfanya aishi mjini bila wasi wasi. Nimekutana nae leo wakati naelekea lunch yaani hana amani hata kidogo lakini mimi nayachukulia kama mapito.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  sasa wee aibu imekujaje?
  Mkeo huyo au nani yako??
   
 3. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kwa taarifa tu mleta mada na wale wengine, wale high class prostitutes ni wasomi na wana kazi zao tena za kulipa. Unaweza kukuta binti ameajiriwa kampuni ya simu na analipwa not less than 3m lakin ni changudoa. Hizi tabia wanazianza tangu wakiwa shuleni na wanakolea. Fumba macho tafakari maisha ya baadhi ya mabinti wa mabibo hostel in town, Ifm, St. Augustine and Tumaini. But IFM, UDSM especially mabibo wanaongoza!!! Akija kupata kazi hata ya 4m ataacha? Kumbuka hao pia wanatoka family well off!!!! Tabia ni kilema bora uondokane nayo mapema.
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  Hiyo extra curricula activity ndo inamfanya ajitutumue mjini hapa. Kupanga ni kuchagua.
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  jirani yako akiwa jambazi unaona aibu wewe?

   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  Badala niwe shosti nae ili nisiibiwe, aibu kwani nikitoka umang'atini kuja kusaka maisha nilijua nitamkuta?
  Badala amuweke akiba jirani, analeta za kuleta!
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  namshangaa.

  Hajui kuna siku atamfaa wakati wa jua afu kwa mkopo au offer ya promosheni tu.

   
 8. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  The oldest business in the world here comes again..
  I always find difficult to blame prostitutes while there are men all around looking for and hook them up..
  Stop chasing them and automatically this business will impulsively be limped off..
  But as long as you appreciate their work don't be surprised to see even King's daughters hustling!!!
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Wengine hufanya out of frustrations tu
   
 10. kbosho

  kbosho JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 4, 2012
  Messages: 12,505
  Likes Received: 3,314
  Trophy Points: 280
  ukistaajabu ya musa utaoyaona ya firauni
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  biashara afanye yeye aibu upate wewe?

  Halafu kwa nini usimuungishe jirani yako? (oooophs hii kichwa leo!!!!!)
   
 12. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hongera kwa kuvaa suti
   
 13. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kuna rafiki yangu mmoja anasifia sana changu wake ambaye nahisi karibia atamfanya permanent. alinambiaje? eti binti aliyempata kutoka kwenye kwaya moja ya kanisani ndiye huyohuyo alimpa gono, wakati uyu changu katembea naye karibia miezi mitatu hajadunga hata sindano moja ya gono. Upo hapo Bosi? Inakuwa kama vile kuna machangu wanajitunza kuliko wale wanafiki wa makanisani au misikitini. hiyo umewahi kuisikia?


   
 14. P

  Pumb JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 296
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wabongo kwa wivu! Yaani unaacha kumpongeza jirani yako kwa ubunifu wa ujasiliamali usio na ushuru wala vat eti unaona aibu! Muungishe jirani fimbo ya mbali haiui nyoka!
   
 15. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  very true
  ma cd ni weengi kuliko unavyoamini
   
 16. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Bora umemfahamu ukitaka kukata kiu utakuwa unamshtua tu unaenda kumaliza
   
 17. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,637
  Likes Received: 2,064
  Trophy Points: 280
  hiyo ni part time, kuna ambao hawatembei usiku kwa kujiuza lakini ukiwafanyia tathmini ni wanapiga kazi kushinda hao, hao approach wanayotumia (sales) anapeleka bidhaa bila kujua mteja wake ni nani lakini hawa wa majumbani ambao tunawaona ni wema wao wanatumia (marketing strategies) kwa kufanya utafiti mdogo wa wateja na kujipendekeza na kutokewa kisha anatoka nae kwa kawaida tulivyozoea lakini kesho yake anaibuka na kipaji kingine yaani kila siku lakini kwa kuwa hatembezi usiku wanaonekana poa
   
 18. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Ibilisi akiwa kafungwa mnyololo na kutupwa jehanum? Hapa kila abiria abebe mzigo wake na kuwashauri wale walobeba mizigo mizito waitue basi. Atayegoma shingo imbomoke.
   
 19. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Hahaaa, na kudrive pia. Atleast mama mkwe hakupanda dala dala japo alipata kero ya kubaki kwenye gari wakati jamaa akienda kutafuta 'kijana' wa kubadilisha tairi.
   
 20. client3

  client3 JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2012
  Joined: Aug 6, 2007
  Messages: 742
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  mi ningependa kujua nani alikaa mbele kati ya mama na mke hata mimi nina ugeni soon
   
Loading...