DSTV waliniambia niwape elfu 30,000/= ili wanipe kingine au ninunue kipya kwa 50,000/=

mogulnoise

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
2,434
5,534
Wasalamu !! Nisipoteze muda ningie direct juu ya hii kampuni ya DstV hapa nchini mbali na madudu kibao wanayotufanyia wateja wao hili sasa ni la kitapeli.
Nilinunua king'amuzi chao hivi vipya nikapewa warranty ya mwaka mmoja

Kabla ya mwaka kuisha kimeharibika nilipowarudishia wakaanza ubabaishaji mara jina linaonyesha ni la mtu mwangine mara warranty yako imeisha nilipowapa documents nilizo nunua na kusaijili wakadai ohh tulikosea serial number.

Sasa wizi ni huu waliniambia niwape elfu 30,000/= ili wanipe kingine au ninunue kipya kwa 50,000/=
Nikawaambia king'amuzi changu kiko kwenye warranty kwa nini ninunue kipya au nilipie ela wakati ni haki yangu mnibadilishie kingine
Wakadai vyakubadilisha vimeisha nisubiri hadi vije ukiwauliza lini hawajui

Huu ni wizi wa wazi kwanini uwe na ving'muzi vya kuuza ila kubadilisha vimeisha
Dstv acheni wizi wa kijinga tubadilishieni ving'amuzi vyetu tena kwa wakati kwani hatukupewa promotion tulinunua tambueni values for money
 
Kwa maelezo yako bado Sijauona huo wizi wa DSTV. Tekeleza ulichoambiwa tu, wape 30,000 upewe kingine. Na kama ni mwanao ndio alifanya uharibifu, wewe nunua tu kingine.
 
Mkuu utakuwa hujala au hujashirikisha ubongo king'amuzi kiko within warranty time hakijaguswa kufunguliwa au kuchezewa chenyewe kimeharibika unataka nilipe nini?
Nilipaswa kirudishiwa kingine tena papohapo sio kusema cha kubadilisha vimeisha wakati vya kuuza vipo

Sikuokota hicho king'amuzi nilitoa ela
 
Wasalamu !! Nisipoteze muda ningie direct juu ya hii kampuni ya DstV hapa nchini mbali na madudu kibao wanayotufanyia wateja wao hili sasa ni la kitapeli.
Nilinunua king'amuzi chao hivi vipya nikapewa warranty ya mwaka mmoja

Kabla ya mwaka kuisha kimeharibika nilipowarudishia wakaanza ubabaishaji mara jina linaonyesha ni la mtu mwangine mara warranty yako imeisha nilipowapa documents nilizo nunua na kusaijili wakadai ohh tulikosea serial number.

Sasa wizi ni huu waliniambia niwape elfu 30,000/= ili wanipe kingine au ninunue kipya kwa 50,000/=
Nikawaambia king'amuzi changu kiko kwenye warranty kwa nini ninunue kipya au nilipie ela wakati ni haki yangu mnibadilishie kingine
Wakadai vyakubadilisha vimeisha nisubiri hadi vije ukiwauliza lini hawajui

Huu ni wizi wa wazi kwanini uwe na ving'muzi vya kuuza ila kubadilisha vimeisha
Dstv acheni wizi wa kijinga tubadilishieni ving'amuzi vyetu tena kwa wakati kwani hatukupewa promotion tulinunua tambueni values for money
Kimeharibika nn? Inawezekana wewe ndo ulikiharibu.
 
Kinaonyesha error no 48 na kudisplya sms ya kuset dish wakati dish signal ziko full na nilipowarejeshea wametest wameona ni kibovu wamebaki nacho wakadai watanipa kingine vikija
Kero yangu ni kwanini wasinipe papo hapo sasa ni wiki ya tatu wakati wanavyo vya kuuza au kureplace kwa tsh 30000 kwa wale warranty iliyoisha
 
Ndio zao wanakuambia vya kubadilisha vimeisha mara vya kubadilisha ni tofauti na hivi vya kawaida... na ukiwapa hiyo 30 hawakupi risiti hata startimes
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom