Dstv Tanzania inasikitisha sana; Channel za news 7 za Kenya, channel ya news 1 ya Tanzania

Hizo sio FTA ndio maana unaziona zimo.

Sizani kama ni tatizo la leseni. Ni ukaidi tu wa Dstv kukataa kuzionesha bure hizo FTA anataka watazamaji wazilipie au mmiliki alipie matangazo, au mmiliki alipie kuziweka Dstv. Kuna mgogoro wa kimaslahi Dstv sizani kama ni swala la leseni kwa sababu dstv wamekua na hizo channel za FTA miaka mingi sana tangu miaka ya tisini huko.
 
Tusiwalalamikie hao ni watu ni biashara zao una weza ukaamua ku-opt / kuacha wizi ni wa TCRA na TBC ambao tunawapa ruzuku kwa mwaka mzima alafu ikija kipindi cha worldcup watu wasio na Startimes wanangaganizwa wanunue bundle / wawe na bundle ili waweze kuangalia huu utani...

Yaani ni full usanii hii nchi ya wasaniii
 
asante sana mkuu nilitaka kununua kumbe na diesitivi nao ni utopolo, ngoja niendelee na kisimbuzi ninachotumia.HIvi kwa bongo kisimbuzi kipi ni bora, hapa na maanisha, ina channel za kueleweka na hata usipolipia local channels unazipata
Vyote inatakiwa vifanye hivyo startimes, continental n.k. leseni yao ni ya kuonyesha channels zote za free to air bure..., ila kipindi hiki cha worldcup wameamua kufanya umafia ili wapate mavuno (yaani huu ndio msimu wao wa mavuno unaotokea kila baada ya miaka minne)
 
Kwa watumiaji wa Dstv tunapata tabu sana kwenye upande wa local news. Inashangaza Dstv kuna channel 7 za local news za kenya KBCTV, NTV, KTN, Citizen TV, KTN News, K24 na kisomali ya Kenya STN TV, hizi zote zinaonesha local news za Kenya ila Tanzania mnatuwekea TBC1 peke yake. Hayo mazagazaga mengine mliyotuzuga nayo sijui Wasafi, Cloudplus, TVe, Safari TV, hayana tofauti na machannel ya YouTube au online streaming ni utopolo

Tunaomba mtuheshimu subscribers wenu turudishieni local channel zinazoeleweka ITV, Channel 10, Star TV, Clouds TV, EATV, Capital TV.
Tumechoka huu upuuzi tutahamia Azam na Startimes kama kama mtaendelea na hizi hujuma zenu Dstv.
Kwanza inatakiwa channels zote ziwe bure,, sisi wabongo hatujazoea kulipa lipa,, hizo pesa wanazokata tozo zilipie hadi DSTV😄🤷🏾‍♂️
 
tatizo umeisha jazwa ujinga wa kushadadia vya bure bure, kwenye dunia ya leo hakuna vya bure, hakuna kitu kama hicho sijui 'free to air' fikiria nje ya box
Mbona enzi za nyerere kila kitu kilikua bure na watu waliishi?,, Serikali itoe subsides kwa dstv ili tutizame bure banah😂
 
Binafsi siwalaumu Dstv, ila angalieni ukweli tu mwamko wa channel za habari za Kenya na Tanzania, Kenya wana media nying ambazo 24/7 zina cover habari ila sasa Tanzania media zetu nying ni cover za Mizik na michezo.. Sisi watanzania kufatilia Habari za Siasa na Uchumi mwamko ni mdogo sana, Ila wa Kenya vijana wanajua sana vitu wapo bright kuliko Sisi wabongo
 
Wakenya tuna exposure kubwa kuliko watanzania🤷🏽‍♂️
 
Kwa watumiaji wa Dstv tunapata tabu sana kwenye upande wa local news. Inashangaza Dstv kuna channel 7 za local news za kenya KBCTV, NTV, KTN, Citizen TV, KTN News, K24 na kisomali ya Kenya STN TV, hizi zote zinaonesha local news za Kenya ila Tanzania mnatuwekea TBC1 peke yake. Hayo mazagazaga mengine mliyotuzuga nayo sijui Wasafi, Cloudplus, TVe, Safari TV, hayana tofauti na machannel ya YouTube au online streaming ni utopolo

Tunaomba mtuheshimu subscribers wenu turudishieni local channel zinazoeleweka ITV, Channel 10, Star TV, Clouds TV, EATV, Capital TV.
Tumechoka huu upuuzi tutahamia Azam na Startimes kama kama mtaendelea na hizi hujuma zenu Dstv.
Package ipi hiyo ambayo haina hizi local channels: ITV, Channel 10, Star TV, Clouds TV, EATV, Capital TV?
 
Back
Top Bottom