Dstv Tanzania inasikitisha sana; Channel za news 7 za Kenya, channel ya news 1 ya Tanzania

stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
12,520
2,000
Kwa watumiaji wa Dstv tunapata tabu sana kwenye upande wa local news. Inashangaza Dstv kuna channel 7 za local news za kenya KBCTV, NTV, KTN, Citizen TV, KTN News, K24 na kisomali ya Kenya STN TV, hizi zote zinaonesha local news za Kenya ila Tanzania mnatuwekea TBC1 peke yake. Hayo mazagazaga mengine mliyotuzuga nayo sijui Wasafi, Cloudplus, TVe, Safari TV, hayana tofauti na machannel ya YouTube au online streaming ni utopolo.

Tunaomba mtuheshimu subscribers wenu turudishieni local channel zinazoeleweka ITV, Channel 10, Star TV, Clouds TV, EATV, Capital TV.
Tumechoka huu upuuzi tutahamia Azam na Startimes kama kama mtaendelea na hizi hujuma zenu Dstv.
Naona sasa hivi hata chanel za superspot 10,9 na 7 kwenye kifurushi cha 19,900/- wamezitoa,hawa jamaa ukishaingia nao tu mkataba wanaanza mbwembwe...
 
stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
12,520
2,000
Unajua FTA channels ni za free hazitakiwi kulipiwa kwakuwa ziko free kwa yeyoye mwenye dishi kubwa zamani ilikua ukiwa na antennae yako ya mwiba unaipata. Sasa Dstv walikua wanaziweka izo ITV nk, lakini ukimaliza muda wako wa kulipia huzioni hata hizo FTA channel mpaka ulipie upya. Nakumbuka startimes wao kifurushi chako kikiisha channel zingine zinaondoka ila zinabaki za FTA kama ITV, star tv nk. Ila dstv wao kifurushi kikiisha wanakata zote. Tcra wakawalima fine kwakuwa wanawalazimisha wateja kulipia hadi kuoma channel za FTA ambazo zipo kwenye vifurushi vyao kwenye vingamuzi walivyowauzia. Sasa dstv wakaona kuliko wawaachie wateja waendelee kuona channels za FTA hata kama vifurushi vimeisha ngoja waviondoe kabisa kwenye package zao.
Uko sahihi kabisa,waliamua FTA ibakia TBC pek yake...
 
Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
10,106
2,000
Ndio. Hilo la kuuliza tena? Bnyeza link HII HAPA uone channels zilizopo. Mie na deal na mambo hayo, naongea uhakika

Duuh, roho imeniuma nimekuwa nikipigwa pesa kila mwezi... tatizo yale madishi makubwa kwenye nyumba za kupanga sio poa!
 
Patra31

JF-Expert Member
Apr 24, 2020
3,597
2,000
Usiwalaumu DStv ilaumu serikali yako.

Ndo iliyowazuia DStv kwa madhumuni maalum ambayo sasa hv yanakutafuna.

Saa ya "UKOMBOZI NI SASA" slogan ya famous late Christopher Mtikila

na kwa sasa ni "UHURU, HAKI NA MAENDELEO YA WATU" ukifuata haya hizo missing channels utaziona vinginevyo sahau.
Acheni kulete siasa kwenye mambo yasiyo hitaji siasa. Uwezi kata driving licence class b alafu ukataka uendesha Gari ya mizigo kwa vile unaweza kuendesha gari kubwa.

DSTV leseni yake hairuhusu kuonyesha channel za ndani zaid ya channel zinazomilikiwa na jamhuri tu. Na haimzui kukata lesen itakayo mruhusu kuonyesha channel za ndani (free to air channel) bali ni ukaidi wake aligoma kuzionesha bure nao waka mwambia azitoe.
 
Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
37,699
2,000
Mi nilishangaa eti ITV haipo dstv,,siku hizi dstv naingia kuangalia series tu za Telemundo au action za studio universal.
 
instagram

JF-Expert Member
May 27, 2014
1,620
2,000
Acheni kulete siasa kwenye mambo yasiyo hitaji siasa. Uwezi kata driving licence class b alafu ukataka uendesha Gari ya mizigo kwa vile unaweza kuendesha gari kubwa.

DSTV leseni yake hairuhusu kuonyesha channel za ndani zaid ya channel zinazomilikiwa na jamhuri tu. Na haimzui kukata lesen itakayo mruhusu kuonyesha channel za ndani (free to air channel) bali ni ukaidi wake aligoma kuzionesha bure nao waka mwambia azitoe.

Kama leseni haimruhusu kurusha channel za ndani mbona kaweka wasafi, clouds plus na tve? Ambazo siyo za jamhuri? Au ni FTA tu ndo haruhusiwi? Tunachanganyana
 
Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
10,106
2,000
DSTV leseni yake hairuhusu kuonyesha channel za ndani zaid ya channel zinazomilikiwa na jamhuri tu. Na haimzui kukata lesen itakayo mruhusu kuonyesha channel za ndani (free to air channel) bali ni ukaidi wake aligoma kuzionesha bure nao waka mwambia azitoe.

Nani alikubali kuzionesha bure?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom