Dstv Tanzania inasikitisha sana; Channel za news 7 za Kenya, channel ya news 1 ya Tanzania

instagram

JF-Expert Member
May 27, 2014
1,532
2,000
Kwa watumiaji wa Dstv tunapata tabu sana kwenye upande wa local news. Inashangaza Dstv kuna channel 7 za local news za kenya KBCTV, NTV, KTN, Citizen TV, KTN News, K24 na kisomali ya Kenya STN TV, hizi zote zinaonesha local news za Kenya ila Tanzania mnatuwekea TBC1 peke yake. Hayo mazagazaga mengine mliyotuzuga nayo sijui Wasafi, Cloudplus, TVe, Safari TV, hayana tofauti na machannel ya YouTube au online streaming ni utopolo

Tunaomba mtuheshimu subscribers wenu turudishieni local channel zinazoeleweka ITV, Channel 10, Star TV, Clouds TV, EATV, Capital TV.
Tumechoka huu upuuzi tutahamia Azam na Startimes kama kama mtaendelea na hizi hujuma zenu Dstv.
 
Kenge (Eng)

JF-Expert Member
Dec 7, 2006
542
250
Usiwalaumu DStv ilaumu serikali yako.

Ndo iliyowazuia DStv kwa madhumuni maalum ambayo sasa hv yanakutafuna.

Saa ya "UKOMBOZI NI SASA" slogan ya famous late Christopher Mtikila

na kwa sasa ni "UHURU, HAKI NA MAENDELEO YA WATU" ukifuata haya hizo missing channels utaziona vinginevyo sahau.
 
Kwanini serikali iwazuie dstv pekeyao mbona startimes na azam channel nyingi zipo? Jamaa wanasingizia serikali ila tatizo ni uroho tu wanazani wakiweka iTv na zingine kwakua hazitakiwi kulipiwa basi watu hawatakua wanalipi kingamuzi. Ni uroho tu wa dstv wala usiilaumu serikali ndugu yangu
 
instagram

JF-Expert Member
May 27, 2014
1,532
2,000
Shida wasababishe TISIARAEI mzigo wabebe Dstv duh!

Tcra ilitupigania sisi watazamaji kwakuwa tulikua tunalipishwa hadi local channels ambazo ni za free to air mfano ITV. Jamaa baada ya kupigwa fine wakaziondoa badala waziachie ziwe free wakaona wakiziacha sisi hatutalipia vingamuzi. Jamaa ni waroho sana wanawaza pesa hawatujali sisi wateja wao.
 
G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,122

Kwahiyo hutaki kulipia king'amuzi vipi hujajua kuwa ili hiyo local channel ikufikie kwa uhakika kuna IT technicians wanaofanya kazi? Unataka wale nini? Au ndiyo mambo ya kichawi kukoseshana riziki? Halafu TCRA wangekuwa wanakupigania wangeshusha bei ya leseni ili upate hizo channel za bure.
 
samora10

JF-Expert Member
Jul 21, 2010
7,586
2,000
Kwa akili yako shida ni DSTV au CCM na vyombo vyake ikiwemo TCRA? DSTv wamepigwa pini, wanataka muangalie TBCCM tu ili wote muimbe mapambio na kusifu 24/7! wengine hata hiyo TBCCM tumeiblock tunaangalia vyombo vya nje tu

Mwaka wa uchaguzi huu fanya maamuzi sahihi...
 
instagram

JF-Expert Member
May 27, 2014
1,532
2,000
Kwahiyo hutaki kulipia king'amuzi vipi hujajua kuwa ili hiyo local channel ikufikie kwa uhakika kuna IT technicians wanaofanya kazi? Unataka wale nini? Au ndiyo mambo ya kichawi kukoseshana riziki? Halafu TCRA wangekuwa wanakupigania wangeshusha bei ya leseni ili upate hizo channel za bure.

Kwani mwanzoni tulipokua tunazipata hizo channel kupitia Dstv tulikua tunalipia mawe au? Au ndo una uchawi kichwani unashindwa kuchambua mambo.
 
instagram

JF-Expert Member
May 27, 2014
1,532
2,000
ilaumuni TCRA na serikali ya CCM kwa kuweka sharia na vitisho vinavyo wabana DSTV

Sheria ziko sahihi kabisa tumetoka analogia kwenda digitali channeli zilikua free to air unatakiwa uziache ziwe free siyo unawalipisha watazamaji. Makaburu wakaona hasara kuziweka hewani bure wakaziondoa.
 
Agenda1

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
1,698
2,000
Kwanini serikali iwazuie dstv pekeyao mbona startimes na azam channel nyingi zipo? Jamaa wanasingizia serikali ila tatizo ni uroho tu wanazani wakiweka iTv na zingine kwakua hazitakiwi kulipiwa basi watu hawatakua wanalipi kingamuzi. Ni uroho tu wa dstv wala usiilaumu serikali ndugu yangu
Wewe ndie umesema vema mkuu, cha kukera zaidi Kifurushi kinapoisha wanakuwa very busy kumpigia mteja anunue kifurushi as if kuna cha maana ktk huduma yao! hawa jamaa wajitathmini, badala ya kujificha kwenye kichaka cha serikali badala yake warudishie wateja wao local channels zenye umuhimu ili tuendelee kutumia huduma yao.
 
papason

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
4,097
2,000
Sheria ziko sahihi kabisa tumetoka analogia kwenda digitali channeli zilikua free to air unatakiwa uziache ziwe free siyo unawalipisha watazamaji. Makaburu wakaona hasara kuziweka hewani bure wakaziondoa.
acha kudanganywaa wewe vya bure vinaokotwa mtoni tuu, yaani uoneshwe ligi ya VPL, au Premium league, ndongaa bure?
 
The Initiator huru

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
1,349
2,000
asante sana mkuu nilitaka kununua kumbe na diesitivi nao ni utopolo, ngoja niendelee na kisimbuzi ninachotumia.HIvi kwa bongo kisimbuzi kipi ni bora, hapa na maanisha, ina channel za kueleweka na hata usipolipia local channels unazipata
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom