Dstv, Punguzeni Bomba kutoka 70+ch hadi 10k kwa 50+ch...

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
994
821
Sasa ipo rasmi Septemba Mosi, 2019 mtashusha bei baadhi ya vifurushi, inatakiwa mfahamu sio wote wanaomiliki ving'amuzi vya Dstv ni wapenda kandanda, yupo mteja analipia kifurushi cha Bomba 19,000. lakini chaneli anayoipenda ni Nat Geo Wild #182 au Nickelodeon #305, Disney #309.

Punguzeni wingi wa chaneli kutoka 70+ hadi chaneli 50+ na bei muweke 10,000. Bila chaneli za michezo, endapo mteja atazitaka chaneli za michezo (Supersport ) itambidi aongeze 9,000. Watazameni washindani wenu kama Azam Tv (45+ch kwa 10,000.) StarTimes (33+ch kwa 11,000) wote hawaungi chaneli za michezo.

Kwa sasa hivi chaneli inayoongoza Tanzania kupendwa na watu wenye rika mbalimbali watoto hadi wakubwa tena inayotuhusu sisi Watanzania sio nyingine Maisha Magic Bongo #160, hapo ndio penye shida hata kama mtatoa ofa ya kulipia miezi sita, je baada ya hapo gharama za kifurushi ni rafiki?

Nina imani kama mtalijadili hili la wingi wa chaneli na ukubwa wa bei ya kifurushi 19,000. Mtaweza kuwashawishi hata wale ambao walinunua Dstv kwaajili ya Ofa, ilivyoisha ofa amekitelekeza, mkumbuke Azam Tv amepata leseni ya Chaneli za ndani na tayari amezirudisha Clouds TV, Chanel 10 na ITV, fanyeni maamuzi magumu kuweza kupata wateja wapya.

Nipo tayari kurekebishwa.
 
Mkuu unachotakiwa kujua ni usifananishe dstv na hao wengine kila kampuni na bei zake na huduma zake pia.
labda useme tu hiyo Bomba ya19,000 haina value for money?
 
Mitanzania ndo maana inauziwa feki
Mtu anataka kizuri kwa hela ndogo
 
Acha kulialia, chagua kisimbuzi unachotaka.... kwani Azam TV akiteka soko wewe unateseka..!!
 
Mimi na family yangu ni wapenzi sana as wrestling, ni mteja wa Dstv Bombs shida ni pale ambapo naona Chanel zinapinguzwa kila siku. Mwezi huu kulikuwa na chanel exclusive kwa wrestling mkaitoa hata kabla ya mwezi kwisha. Nimelipia jana siioni tena. Chanel za sports kulikuwa na supersport 4, 7, 8, 9 na 10 lkn sasa naona mnahangaika sana jana nilipolipia kulikuwa na super sport 3, 4, 8, 9, 10 na max. Lkn Leo nimeamka zipo 3, 9 na 10. Sijui mnamaanisha nini hapo. Kuna Chanel zipo tu huwa siziangalii kama za.movies za Nigeria, zile za kichina. Tengenezeni basi vifurushi tofauti tofauti kama channel za sports tu ziwe na bei yake! Kuweni wabunifu
 
Enzi zote za msoto wa Local channel nimekua natumia Azam Malawi. Napata channels zote Local za Azam Kwa Bei ndogo ya elfu 6 ya Tz. Ki ufupi nina Visimbuzi vitatu. DsTv, Azam na Star times.

Ninachofanya Ni Kugeuza Dish na kuweka Kingamuz ninachotaka.

Mfano: Mama yenu mdogo akinitembelea huwa namuwekea DsTV ili aangalie Kapuni, sijui na upuuzi gani wa Maisha Magic Bongo. Akisha ondoka, narudisha Azam kama kawaida napata ITV, Star Tv Clouds, Ch. 10, Wasafi, Etv, na Nyingine Kibao
 
Kweli siwezi fananisha Dstv na king'amuzi kingine lakini ulitegemea Dstv kutembezwa mitaani!!!

Mkuu unachotakiwa kujua ni usifananishe dstv na hao wengine kila kampuni na bei zake na huduma zake pia.
labda useme tu hiyo Bomba ya19,000 haina value for money?
 
Enzi zote za msoto wa Local channel nimekua natumia Azam Malawi. Napata channels zote Local za Azam Kwa Bei ndogo ya elfu 6 ya Tz. Ki ufupi nina Visimbuzi vitatu. DsTv, Azam na Star times.

Ninachofanya Ni Kugeuza Dish na kuweka Kingamuz ninachotaka.

Mfano: Mama yenu mdogo akinitembelea huwa namuwekea DsTV ili aangalie Kapuni, sijui na upuuzi gani wa Maisha Magic Bongo. Akisha ondoka, narudisha Azam kama kawaida napata ITV, Star Tv Clouds, Ch. 10, Wasafi, Etv, na Nyingine Kibao
Si unapata gharama ya kubadilisha uelekeo wa dish kila siku
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom